Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Siyo upinzani, ni facts. Kiwanja hakijengwi kwa kazi hiyo, anyway. Ingekuwa ni private air strip, Sawa. Toka umekamilika ni almost 2 years, mbona hizo ndege haziendi huko. Au zitaanza safari za Chato lini!?
hivi mwalimu nyerere alinunua ndege, na kujenga miundo mbinu akitaka faida ya hapohapo??

Kumbe we we shida yako ulitaka mradi wa kuanzisha Leo kesho uwebilionea??

Umejifunza wapi we we biashara ya hivyo??

Kwahyo kwa akili yako huna atavission ya maendeleo ata kidogooo.
 
ATCL ina madeni mengi sana. Kama ndege zingeinyizwa huko lazima zingechukuliwa na wadai. Airline nyingi zina hasara. Ina maana sababu ya hasara ndio hatuhitaji ndege?
Ukisikia JPM anasema kwani kiwanja ni Chato tu mbona hamuongelei vingine; ujue chumvi iliyosuguliwa kwenye kidonda inauma!
 
Wewe unavutia wapi?
Nadhani kila mvuta kamba huivutia kwake, hivyo ubinafsi ni silka ya wanadamu wote.
faida ya kununua ndege itachukua muda mrefu kupata faida, tena na hii corona ndo kabisaa hasara inaongezeka
 
Chato ni sehemu ya Uganda au ni Burundi?.
Jibu jepesi kwa maswali magumu!!!!!Hata Mobutu Seseko alijenga ndani ya nchi yake,hakujenga nchi nyingine!Lakini unaelewa kwanini alivuma na ameandikwa kwenye historia!
Ukiacha mihemko,ndani ya nafsi yako mwenyewe unajua si sawa!
 
Watz muwe makin na hoja za uwanja wa ndege chato kwani hamjui rais kawawekea mbuga ya brig chato,kuna rubondo national park km 2 toka uwanja ulipojengwa ,kuna rumanyika nk mkuu anaanzisha utalii wa kanda nyingine bado hamwon faida ya badae shauri yenu huyu jamaa anaona mbali mno kwa mtu mwenye akili za tiamajitia maji macho yataona majungu tu
 
Hajajibu hoja yoyote!
Ameweka siasa tu
Kwani kabla ya yeye kununua hii midege isiyotoa faida hakukuwepo na ndege za mashirika mengine?
Lisu akienda Chato akawaulize Kama tangu wamejengewa uwanja na je biashara zao zimeimarika kwa kuzipeleka ulaya kuuza nk?
 
Huko muendako wapi? Jibu hoja hapo juu maana unaleta blaa blaa,nyie maccm mipango yenu inamnufaisha nani? Utasikia nchi,nchi ni nini bila watu? Acheni kuchezea kodi zetu kwa mipambo na matumizi ya kipuuzi.
Staili ya Jk ya kuacha private sector iendeshe sekta ya anga iliondoa mzigo kwa nchi na kuleta unafuu wa bei kwa ushindani uliokuwepo na hakuna hasara nchi ilipata
 
Kujenga kiwanja sio upotevu wa mapato,ni investment...miaka 50 toka sasa huo uwanja utawafaa vizazi vijavyo
Ndio maana maccm hamna akili,hamjui mfanye kipi wakati gani,kwamba ilikuwa lazima kujenga huo uwanja sasa ili uwafae watu baada ya miaka 50? Mbona reli za mzungu zilizojengwa miaka Mia iliyopita hazitufai sisi wa kizazi Cha saizi? Thinking ya maccm ni zero kabisa.
Vyoo tu vimewashinda ,kampeni ya nyumba ni choo inasema Kuna upungufu wa 60% ya matundu ya vyoo ,eti wewe unazungumzia mambo ya kizazi kijacho ..Kimsingi hakuna kitu ccm imekifaulu kwa usahihi toka uhuru
 
Uwanja wa Bukoba upo kama akiba ya Mwanza.

Gharama za kujenga Chato angepanua uwanja wa Mwanza au Bukoba au Kigoma.

Huko kote ni strategic kuliko huo uwanja wa Chato.
 

Hata mabutu aliojenga huko DRC Kwani alipokufa si aliuacha, kwahiyo kwakuwa aliuacha tusiseme aliujenga kwao. Hii hoja mbona haina mashiko
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja

Lakini hiyo corona ndo imekuwa sababu ATCL kuhamishiwa ikulu ili hesabu zake zisikaguliwe CAG kwanini anaficha kama ndege zinatengeneza faida. Atupe majibu sisi si ndiyo wananchi tuliolipa kodi za kununulia hizo Ndege ni za kwetu zikaguliwe na CAG ili tujuwe pesa zetu zinatengeneza faida kiasi gani narudi ni Ndege za umma siyo za mtu kwamba anaweza kuamua hesabu zake zikaguliwe au la.
 
Huyu jamaa ana hasira sana, sipati picha alivyokuwa mwalimu, wanafunzi walipata shida sana.
h
alikuwa moja kati ya walimu bora kabisa,kanifundisha kemia form 1na2, wala hakuwa na hasira somo lake tulimwelewa vizuri mno na hakuwa wakufuatiliafuatilia wanafunzi. sema ukiwa kiongozi mkuu wa nchi maskini hizi ili mambo yaende waru wengi wanaweza wasikuelewe na kweli hawatakuelewa
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Usijaribu uwe umejua unachopasa kukijibu, hiyo sheria iliyotajwa kasma no 20 umeielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…