Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

KWAHYO HUO UWANJA HAKUNA MTANZANIA WALA NDEGE YOYOTE ITAKAYO RUKA HAPO?
INAMAANA HAKUNA WAFANYABIASHARA WENYE UWEZO AU WAGONJWA WENYE UHITAJI WA HARAKA KWA KUTUMIA UWANJA HUO??

SHIIIDA KWELI KWELIII.
Ebu watajie hao CCM shirika la ndege linalofanya safari za Chato.
 
Msuya alitumia nafasi yake kupeleka umeme Mwanga miaka ile enzi za Nyerere na hakuna aliyelalamika.

Umeme ule unatumika mpaka kesho.

Magufuli kujenga uwanja utakaokuja kutumiwa na watu wa vizazi vijavyo imekuwa nongwa!!.

Kuna watakaotumia uwanja huo vizazi vingi vijavyo sijui kama kwa kuhoji ujenzi wa uwanja tunakuwa tumewafikiria au ubinafsi wetu ndio unaotunyima uwezo wa kutazama mbeleni.
 
Tatizo unapofushwa macho ya ndani ya nafsi yako ukiongozwa na akili za kisiasa kule kutazama muelekeo wa maisha halisi miaka mingi ijayo.

Lissu akiwa rais na ajenge chochote kule Ikungi na hakuna mtu atakayemlalamikia ili mradi tu hicho atakachokijenga kuwa na faida za kiuchumi zitakazowagusa watu wa vizazi vingi vijavyo.
 
Wazungu wangekuwa na mawazo kama yako ule Mnara wa New York na ule wa Paris usingejengwa kwani wakati ule ilionekana kama ni upotezaji wa pesa na muda.
 
Wewe kichwa panzi, hujui kwanini maeneo ya viwanja vya ndege huwa yanatengwa kwenye mipango miji? Hii ni kwasababu kama itatokea kuna uhitaji wa uwanja wa uwanja wa ndege basi ujengwe wakati huo! Mfano kila wilaya zina maeneo kwaajili hiyo ila siyo kwamba wanajenga tu kwa ajili ya matumizi ya miaka 20 ijayo, haiko hivyo!

Vinatengwa na miji ikikua na tathimini ikaonesha sasa wanahitaji kiwanja, ndioo hujengwa! Huko Chato palitakiwa pawe pametengwa tu eneo na baada ya hiyo miaka 20 mnayosema kama kutakuwa na uhitaji basi kiwanja kikajengwa!

Na uhaba huu wa pesa, bado tunaenda kuzika fedha sehemu ambazo hazina tija kwa sasa au miaka ya karibuni? Hii ni akili au matope??
 
Wazungu wangekuwa na mawazo kama yako ule Mnara wa New York na ule wa Paris usingejengwa kwani wakati ule ilionekana kama ni upotezaji wa pesa na muda.
Ebu onyesha wapi wakati ule ilionekana kama ni upotezaji wa pesa. Maadamu umeweza kujisajili JF na ku post, inatakiwa uweze kujua kutumia google kutafuta ukweli.
 
Kitakachofuata chini ya Phillipo Bukililo, watajenga hoteli ya nyota tano hapo kwa ajili ya kupokea wageni miaka ijayo 🙂
 
Wewe ndio kichwa panzi unayeandika usichokijua kuhusu Chato.

Yaani wewe unajua kuliko wenye mji wenyewe!!.

Haya ni matatizo yetu watanzania, kujua kila kitu kuliko hata wenye mamlaka wenyewe.

Umeongelea kujipendelea kwa rais na mimi nimekupa mfano halisi wa Mzee Msuya aliyejiwekea umeme jimboni kwake Mwanga miaka ile ya 1980 mwanzoni na hakuna mtu aliyelalamika.

Kujipendelea kwingine ni pale TRA ilipokuwa na wakurugenzi nane wote kabila moja tena wakimuita RIP Mkapa shemeji.

Nchi ni yetu sote na kila eneo linapaswa kujengewa miundo mbinu itakayochagiza maendeleo ya kesho na kesho kutwa.

Lissu akija kuwa rais halafu akajenga miundo mbinu pale Singida provided itakuwa ina lengo la kubadilisha maisha ya watu wa vizazi vijavyo mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono ujenzi wa hiyo miundo mbinu.
 
Ebu onyesha wapi wakati ule ilionekana kama ni upotezaji wa pesa. Maadamu umeweza kujisajili JF na ku post, inatakiwa uweze kujua kutumia google kutafuta ukweli.
Ujumbe wangu umeeleweka. Sio kila mradi una lengo la kuleta faida za kuonekana leo wala kesho wakati mwingine wafaidikaji wa kinachofanyika leo bado hawajazaliwa.
 
Ujumbe wangu umeeleweka. Sio kila mradi una lengo la kuleta faida za kuonekana leo wala kesho wakati mwingine wafaidikaji wa kinachofanyika leo bado hawajazaliwa.
Unapoweka vielelezo ku support hoja zako, hakikisha vielelezo hivyo havipingi hoja zako.

Mradi wowote unapoanzishwa, una lengo la kuleta faida mara tu umalizikapo. Kinyume na hapo, ni upotezaji wa fedha na utakufa au huduma kwa jamii ambayo lazima ifadhiliwe.
 
Sio kila mradi faida zake zinaonekana kesho yake.

Na mitizamo kama ya kwako ndio chanzo cha tija kutoonekana katika miradi mingi mikubwa haswa Afrika.
 
KWANI KUNASHIDA GANI KUJENGA UWANJA CHATO?
KWANI CHATO SIO TANZANIA?
KWANI UWANJA WA NDEGE CHATO SI UWANJA WAWATANZANIA WOTE?
KWANI UWANJA WA CHATO NI MALI YA MAGUFULU NA FAMILIA YAKEEE??
Lete faida ya airport chato
Tumetoa hasara kuwa uwanja hautumiki kibiashara
 
Kwahiyo CCM mnajua mna tatizo la upendeleo kwa viongozi wenu??Mbona Nyerere hakuwa hivyo?Hivi kungekuwa na kiwanja msoga au Butiama,halafu ingekuwaje?Usiwe mjinga!
Tuambieni tokea uwanja ukamilike,kuna route gani ya ndege inaenda Chato?Kama sio ndege ya Rais pekee!
Uwanja haukuwepo hata kwenye bajeti,halafu mnatuletea poroja hapa!
Kwahiyo Lissu akiingia madarakani akaenda kujenga kiwanja kijijina alikozaliwa utaona ni sawa?
Chato yamefanyika mengi kama barabara,shule,umeme,zahanati nk lakini hakuna anayeyasema hayo kwasababu yanalenga kuhudumia wanachato!Kwanini watu wanapigia kelele uwanja na si hayo mengine?Mfano Kasulu alipopita JPM juzi,pamechangamka na ni mji wa kibiashara sana kuliko kibondo na chato!Lakini kuna uwanja wa ndege wa vumbi tu,ni eneo limetengwa kwa ajili ya matumizi ya baadae!
Hebu angalia mji mkubwa kama Kahama kukosa uwanja wa ndege halafu eti chato ina uwanja!
Kwenye hili kulitetea mtaonekana wajinga!
Hayo ya kina Msuya sitaki kwani serikali ilikuwa ya chama gani?Si ndio ninyi wenyewe?
Tunaongelea ya JPM kwasababu ni ya sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…