Wewe ndio kichwa panzi unayeandika usichokijua kuhusu Chato.
Yaani wewe unajua kuliko wenye mji wenyewe!!.
Haya ni matatizo yetu watanzania, kujua kila kitu kuliko hata wenye mamlaka wenyewe.
Umeongelea kujipendelea kwa rais na mimi nimekupa mfano halisi wa Mzee Msuya aliyejiwekea umeme jimboni kwake Mwanga miaka ile ya 1980 mwanzoni na hakuna mtu aliyelalamika.
Kujipendelea kwingine ni pale TRA ilipokuwa na wakurugenzi nane wote kabila moja tena wakimuita RIP Mkapa shemeji.
Nchi ni yetu sote na kila eneo linapaswa kujengewa miundo mbinu itakayochagiza maendeleo ya kesho na kesho kutwa.
Lissu akija kuwa rais halafu akajenga miundo mbinu pale Singida provided itakuwa ina lengo la kubadilisha maisha ya watu wa vizazi vijavyo mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono ujenzi wa hiyo miundo mbinu.
Kwahiyo CCM mnajua mna tatizo la upendeleo kwa viongozi wenu??Mbona Nyerere hakuwa hivyo?Hivi kungekuwa na kiwanja msoga au Butiama,halafu ingekuwaje?Usiwe mjinga!
Tuambieni tokea uwanja ukamilike,kuna route gani ya ndege inaenda Chato?Kama sio ndege ya Rais pekee!
Uwanja haukuwepo hata kwenye bajeti,halafu mnatuletea poroja hapa!
Kwahiyo Lissu akiingia madarakani akaenda kujenga kiwanja kijijina alikozaliwa utaona ni sawa?
Chato yamefanyika mengi kama barabara,shule,umeme,zahanati nk lakini hakuna anayeyasema hayo kwasababu yanalenga kuhudumia wanachato!Kwanini watu wanapigia kelele uwanja na si hayo mengine?Mfano Kasulu alipopita JPM juzi,pamechangamka na ni mji wa kibiashara sana kuliko kibondo na chato!Lakini kuna uwanja wa ndege wa vumbi tu,ni eneo limetengwa kwa ajili ya matumizi ya baadae!
Hebu angalia mji mkubwa kama Kahama kukosa uwanja wa ndege halafu eti chato ina uwanja!
Kwenye hili kulitetea mtaonekana wajinga!
Hayo ya kina Msuya sitaki kwani serikali ilikuwa ya chama gani?Si ndio ninyi wenyewe?
Tunaongelea ya JPM kwasababu ni ya sasa!