Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? Ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11, hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli


Hoja za Wadau, wapiga kura hawajaridhika

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka Mwanza airport mpaka Chato?
5. Baada ya yeye kumaliza urais, huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
waliompa nchi jiwe sijui walifikiria nini nahisi waliichoka tz,serikali yake yote kaipigisha magoti ,anafanya anachotaka anachofikiria kiwe na madhara hakina madhara kwake twende tu
 
Nadhani kila mvuta kamba huivutia kwake, hivyo ubinafsi ni silka ya wanadamu wote.
faida ya kununua ndege itachukua muda mrefu kupata faida, tena na hii corona ndo kabisaa hasara inaongezeka
KIONGOZI AKIWA MBINAFSI HAFAI.... don't give us some excuses mzee....
Nyerere was a good leader and he wasn't self_centered..
 
KWANI KUNASHIDA GANI KUJENGA UWANJA CHATO?
KWANI CHATO SIO TANZANIA?
KWANI UWANJA WA NDEGE CHATO SI UWANJA WAWATANZANIA WOTE?
KWANI UWANJA WA CHATO NI MALI YA MAGUFULU NA FAMILIA YAKEEE??
Creation of "white elephants" using tax payers has been a trend with irresponsible African leaders before him.
 
Jamaa anapenda ndege! Hebu afanye utafiti ni watanzania wangapi Wana uwezo wa kupanda ndege ,anakera.
Isitoshe, walifanya utafiti wakutosha wakijua kwamba kwenye karne hii ushindani wa soko la anga sio wa kitoto kihivyo? Au walitaka kuwafungia kina Emirates na wenzao pia? Kama fastjet walivyo fanyiwa... pia walitaka tujitenge kianga pia? Je, kwa kufanya hivyo na sisi tusingetengwa kwa kutopata ruhusa ya kushusha ATCL yetu kwenye viwanja vya ndege za kwao? Au tungeambiwa safari za ndani tu inatutosha?

Ukiacha hayo yote, ukigoogle tu, nina amini pasipo na shaka kwamba, ni mashirika ya ndege vichache sana duniani kote, ambazo zinapata faida...
 
"Mtu anazungumza eti nimejenga uwanja nyumbani, nikifa nitaenda nalo hilo liuwanja kaburini? Ni lazima upange mipango mipana, tumejenga na tunajenga viwanja vingi zaidi ya 11, hivyo viwanja vyote watu hawavioni wanakiona cha Chato tu, ashindwe akalegee kweli kweli". Rais Magufuli


Hoja za Wadau, wapiga kura hawajaridhika

1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka Mwanza airport mpaka Chato?
5. Baada ya yeye kumaliza urais, huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
Uwanja wa chato Airport hauna faida wala tija kwa Taifa ni kama ule uwanja wa marehemu Mabutu seseco aliojenga porini baada ya kufarika ukageuka kuwa magofu mazalia ya popo, chato Airport imejengwa kienyeji pasipo idhini ya bunge kuna ufisadi wa kutisha sana, kuanzia ununuzi Ndege, flyover, ujenzi wa reli, bwawa la umeme na miradi yote mikubwa
 
Kumbe sindano za Lissu huwa zinamuingia huyu mzee.
Hapati usingizi mpaka kutengeneza ushetani wa kupita bila kupingwa ili aweze kupata wabunge wagonga meza Bungeni wabadili katiba awe Rais wa milele kama china
 
Kufufua hakukosea,kinachozungumziwa ni jinsi gani ununuzi wa ndege ulivyofanyika,taratibu zinasemaje,zilifuatwa?
 
Anatakiwa kujibu hoja :
  1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
  2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?
  3. Kwanini hataki kuweka wazi mikataba ya manunuzi ya ndege?
  4. Kama anaweza kusafiri na gari nchi nzima wakati wa kampeni anashindwaje kusafiri kutoka mwanza airport mpaka Chato?
  5. Baada ya yeye kumaliza urais huo uwanja utatumika kwa kazi gani?
  6. Kwa kuwa makampuni yote duniani hayanunui ndege za abiria kwa hela taslimu ( commercial aircraft leasing agreement ) ili kuweza kumudu mtaji na gharama za uendeshaji. Je biashara hii inaweza kuhimili ushindani sokoni?
  7. Mbona anakuwa anatoa majibu kiukali kwani kuna nini vile?
  8. Asitufokee, lazima ajue sisi ndiyo tunamlipa mshahara na kiinua mgongo mara akistaafu.

Ukijibiwa usisahau kunitag
 
Nimekaaa na kutafakali juu ya haya malumbano juu ya huu uwanja wa ndege Chato ambao mimi kwa maoni yangu naona serikali iliyopo madarakani ilifanya jambo jema kuujenga.

Nasema ilifanya jambo jema sababu Geita sasa ni mkoa na ulikuwa hauna uwanja wa ndege. Na ndege zilizokuwa zinatua Geita zilikuwa zinatumia Airstrip ya Geita gold mine.Kwa hiyo ujenzi wa uwanja huu ni kwa manufaa ya wananchi wa Geita wote na wala sio mali ya rais JPM na familia yake.

Nilimsikikiza mbunge wa Geita vijijini akisema kuwa ujenzi wa uwanja ule ulipata baraka za baraza la halmasuri la Geita ambalo linakuwa na wabunge na madiwani. Na hivyo liliodhinisha uwanja huo ujengwe.

Pia nimemsikiliza katibu mwenezi wa Ccm juu ya ujenzi wa uwanja huu na nikamsikia akisema serikali ya Ccm iliridhia uwanja huu ujengwe na ulijengwa Chato sababu ya mikakati maalumu kama kuwa karibu na hifadhi ya taifa Rubondo na muinuko wa maeneo ya mkoa wa Geita.

Leo akiwa Mufindi ndugu Tundu Lissu nimesikia kama akijibu mashambulizi ya mgombea wa Ccm baada ya kuonekana anatetea ujenzi wa uwanja wa Chato kama ujenzi wa viwanja vya ndege vinavyojengwa mikoa mimgine. Mfano ni mkoa wa Rukwa ulijengewa kiwanja cha ndege mjini mpanda na ndege za Atcl zinaweza kutua.

Nimensikiliza Lissu akisema uwanja wa ndege Chato ulijengwa kwa utashi wa rais JPM na upendeleo kwa eneo analo tokea. Jambo ambalo wakazi wa mkoa wa Geita hawawezi kukubali sababu nao wanahitaji maendeleo kama kujengewa uwanja wa ndege. Lissu ameenda mbali na kusema kuwa mabilioni yaliyotumika kujenga uwanja wa ndege Chato yangeweza kujenga barabara nyingi tu za mji wa Mufindi. Swali langu kwa Lissu je watu wa Geita hawahitaji maendeleo ya kuwa na uwanja wa ndege? Je watu wa Mufindi na watu wa Geita wote si watanzania? Kama kuna kiwanja Chato kwa nini asiwaahidi kuwajengea hizo barabara ambazo anasema hazipo Mufindi! Kwa hiyo watu wa Geita kwa Lissu hawana umuhimu kisa tu JPM anatokea Geita?

Longo longo kibao.Ujenzi wa uwanja wa Chato ni matumizi mabaya ya madaraka ambayo utayakuta Afrika pekee yake.Mabara mengine huu upuuzi walishasahau tangu karne ya 20.
 
Creation of "white elephants" using tax payers has been a trend with irresponsible African leaders before him.
Kwani hizo hela zimetumika kujenga uwanja ambao ni mali yake?
Kwani chato hapafai kujenga uwanja??

Kwa nini huuu uwanja umewauma??
Shida iko wapiiii??
 
Mwenye macho haambiwi ona. Mambo mengine sio yakubishana
Muda utaongea, loud and clear

Serekali siku zote ikijiingiza katika biashara tegemea majanga makubwa.Binafsi ningependa ATCL ishirikiane na sekta binafsi katika uendeshaji wake na hasa bodi wawepo watu binafsi.
 
Je huo uwanja ulipangiwa bajeti bungeni? Kwa nn asingejenga geita? In short ni ufisadi na upendeleo
 
Majibu rahisi kwa maswali magumu. Anyway he tried.
Kuna masomo yanaitwa Static na Dynamics. Ukipewa swali la haya masomo uka'solve' zaidi ya ukurasa mmoja wa A4 ujue umeishafeli swali hilo. Maswali yenyewe utata kipindi hicho. Sasa Mgombea urais, Dr. Magufuli anasolve hayo maswali kwa kutumia nusu ukrasa wa A4!
 
Kwani
Kwani wanaoishi chato hawana haki yakuwekewaa taaa barabaranii???

Au wewe umezuiliwa kupeleka gari kwenye hizoo taaa za chato??

Mbona mnabwabwaja tuuuu??
Duh....!
Yssni nitoke Dar nipeleke gari Chato kwa sababu ya taa? Sijui hata umewaza nini kuandika huu upupu!!
 
Duh....!
Yssni nitoke Dar nipeleke gari Chato kwa sababu ya taa? Sijui hata umewaza nini kuandika huu upupu!!
Sasa kama umeona chato kuna taa nzuri hadi zimekunyima usingizi, Si bora na we we upereke gari lako huko ili ufaidi. Maana umeona watu wa chato wanafaidi kukuzidi we we wa dar.
 
Jibu jepesi kwa maswali magumu!!!!!Hata Mobutu Seseko alijenga ndani ya nchi yake,hakujenga nchi nyingine!Lakini unaelewa kwanini alivuma na ameandikwa kwenye historia!
Ukiacha mihemko,ndani ya nafsi yako mwenyewe unajua si sawa!
Acha nongwa za kibaguzi mkuu. Viwanja 11 vya ndege vinajenga, vinakarabatiwa na kupanuliwa nchi nzima Ndio maana nimekwambia Chato sio Burundi.

KIA upo uwanja na Arusha upo ina maana viwanja vile kuwepo ni sawa lakini uwanja wa Chato kuwepo sio sawa!!.

Acheni akili za kibaguzi, acheni dharau za kipuuzi. Ina maana watakaokuja kuzaliwa Chato miaka ijayo watakuwa hawana hadhi ya kupanda ndege.
 
KWAHYO HUO UWANJA HAKUNA MTANZANIA WALA NDEGE YOYOTE ITAKAYO RUKA HAPO?
INAMAANA HAKUNA WAFANYABIASHARA WENYE UWEZO AU WAGONJWA WENYE UHITAJI WA HARAKA KWA KUTUMIA UWANJA HUO??

SHIIIDA KWELI KWELIII.
Huo uwanja umeshakamilika muda mrefu na tokea ukamilike ni ndege za magufuli akiwa anaenda kupumzika,ndege ya Uhuru kenyata na mseveni tu ndio zimetua hapo kuja kumsalimia dictator au kulazimisha kufanyia mambo ya kiserikali
Chato hakuna hakuna mzunguko wa fedha wa kuhitaji usafiri wa ndege
Uwanja huu Ni kama ule wa dictator Mobutu aliojenga kijijini kwake
 
Lissu titamrudisha kwa Amsterdam ikifika oktoba
Jibu hoja kwanini uwanja ulio harimu ma bilioni ya pesa za walipa kodi wakiwemo mama ntilie wamachinga na wengine unatua ndege moja tu tena kwa crismas na pasake kule kijijini chato jee akiondoka madarakani hule uwanja ninavojua mm patajengwa banda la kufugia punda

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom