Alwatan Mabruki
Senior Member
- Sep 20, 2020
- 132
- 116
Ikiwa ni siku saba zimebaki kuelekea uchaguzi mkuu, mgombea wa Urais kupitia CCM Mhe. Dkt. John Magufuli, amewataka Watanzania kujitenga na propaganda za ubaguzi zinazoenezwa na baadhi ya wagombea.
Pia amewatahadhalisha Watanzania wakiona mtu anaongea kuhusu chuki, wafahamu kwamba hayupo kwa maslahi ya Taifa, bali ana malengo mabaya ya kuleta machafuko nchini.
Alitoa rai hiyo jana wilayani Korogwe mkoa wa Tanga wakati akihutubia wanachama wa CCM waliojitokeza kwenye viwanja vya chuo cha walimu Korogwe.