Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli hajawahi kushindwa, hatashindwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli hajawahi kushindwa, hatashindwa

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wakuu, salaam!

Nawakumbusha tu kwamba John Pombe Magufuli hajawahi kushindwa na haitatokea ashindwe - mara zote akiwa mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na baadae Chato iwe ndani ya CCM au uchaguzi mkuu hakuwahi kushindwa na haitatokea ashindwe.

Katika uchaguzi tunaoenda kuufanya tarehe 28 Oktoba, 2020 bado anapambana lkn usitegemee atashindwa - sababu za kutoshindwa ziko nyingi:-

(i). Uwezo binafsi na Ubunifu:-
Haikuwa kazi nyepesi kusimamia ongezeko la mapato ya Serikali kutoka takriban 800B - 1.3T kwa mwezi (ni fedha hizi zimewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa kwa midogo i.e viwanja vya ndege, ndege, meli, vivuko, maji, hospital na vituo vya afya, elimu bure nk nk);

(ii). Ziara za ndani:-
Wakati wote ametumia muda mwingi kufanya ziara za kikazi ndani ya mikoa tofauti na utamaduni wa viongozi wengi ambao leo wakinywa chai Ufaransa mchana hula UK - hii imemjengea sifa kubwa kwa wananchi na kuwa ktk orodha wa viongozi wanaoaminiwa;

(iii). Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma:-
Hapa kila mmoja ni shahidi kwamba hata zile kelele za ufisadi zilizokuwa zinapigwa zimepungua sana - ingawa anapaswa kuendelea kumulika zaidi kwa watendaji wake ili wasiingize masuala binafsi kwenye utendaji wa kila siku;

(iv). Ajali za barabani - zimepungua sana tofauti na miaka kadhaa ya nyuma;

Kwa ujumla sifa za kiungozi anazo nyingi, kama kuna kasoro sehemu basi ni zile za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo.

Rai yangu:-
Kwa kuwa amehiari kutuongoza kwa miaka mingine mitano (2020/2021 - 2024/2025) basi tukubali kwa wingi wetu kumchagua na kulinda kura zake ili zisihujumiwe na mahasimu wake wa kisiasa.

Nawasilisha kwa hatua zenu hapo 28/10

Nadhani:-
Wengi wenu mmeelewa kwa nini nilikuja na hoja hii siku takriban 18 kabla ya uchaguzi mkuu.

=========================
Ushindi mwingine wa Mhe Dkt Magufuli ni jinsi alivyoifanya Zanzibar kuwa kitu kimoja - Mhe Maalim Seif kukubali kuunganisha nguvu na Mhe Dkt Mwinyi ni ushindi kwa JPM
Ni ushindi kwa CCM
Ni ushindi kwa Tanzania

*****************
Ushindi wa tatu wa Dkt John Pombe Magufuli ni kuibadili sura ya wilaya ya Chato "hospitali ya rufaa, sgr, kivuko cha busisi, bandari nyamirembe, uwanja wa ndege, hifadhi ya Chato - burigi" - vyote hivi lzm viifanye Chato kama jiji la Tokyo miaka michache ijayo.

Baraka Obama alijisahau, Kenya ingekuwa kama WDC "

********************
18/01/2021
Umeshinda hisia za wana-bukoba kuhusu fedha za tetemeko - ungetugawia unga tungekuwa tumeula na kuumaliza. Lakini sasa hiyo miundombinu ya elimu Ihungo Sekondari itadumu kwa karne nyingi huku watoto wa maskini wakifaidi uwepo wake.

Dkt John Pombe Magufuli, kwa mara nyingine tena watanzania tunakupigia saluti wewe na wasaidizi wako!!

Msakila M Kabende
Kigoma
19/01
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo

1. Kuiba na kula rambirambi
2. Wizi wa 1.5 trillion
3. Ukandamizaji wa haki za binadamu
4. Ubaguzi
5. Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6. Utekaji na mauaji
7. Kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8. Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9. Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10. Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari
 
Dodoma alituahidi. 2017-20.

1. Ujenzi wa uwanja mkubwa wa kisasa wa michezo kushirikiana na mfalme wa Moroco ameshindwa.

2. Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko kuzunguka Dodoma jiji. Ring road Ameshindwa.

3Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato ameshindwa.

4. Ujenzi wa Hospital ya Uhuru baada ya kukata fedha za sherehe maazimisho ya uhuru day.

5.Kiingereza kimemshinda.

Hii ni Dodoma sijui huko mikoani?
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo
1.kuiba na kula rambirambi
2.Wizi wa 1.5 trillion
3.Ukandamizaji wa haki za binadamu
4.ubaguzi
5.Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6.utekaji na mauaji
7.kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8.Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9.Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10.Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari
Acha vituko wewe!

Kama Lowasa mlimdekia hadi barabara, mtu ambae Lisu ma chadema nzima walimnanga kwa miaka 8, sembuse Magu?
 
Na atakayetaka kumkwamisha atakwama yeye

cc lisu na bavicha humu
 
Yeye ni nani asishindwe na umesema hatowahi kushindwa! Ana maagano na Mtukufu Mwenyezi Mungu? Au unafikiri kwa vile anapora mali za wanachi na anapofadhili mambo ya ajabu watendewe watu wengine ni jambo ambalo Mungu analikubari?
 
Wakuu, salaam!
Nawakumbusha tu kwamba John Pombe Magufuli hajawahi kushindwa na haitatokea ashindwe - mara zote akiwa mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na baadae Chato iwe ndani ya CCM au uchaguzi mkuu hakuwahi kushindwa na haitatokea ashindwe.

Katika uchaguzi tunaoenda kuufanya tarehe 28 Oktoba, 2020 bado anapambana lkn usitegemee atashindwa - sababu za kutoshindwa ziko nyingi:-
(i). Uwezo binafsi na Ubunifu:-
Haikuwa kazi nyepesi kusimamia ongezeko la mapato ya Serikali kutoka takriban 800B - 1.3T kwa mwezi (ni fedha hizi zimewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa kwa midogo i.e viwanja vya ndege, ndege, meli, vivuko, maji, hospital na vituo vya afya, elimu bure nk nk);

(ii). Ziara za ndani:-
Wakati wote ametumia muda mwingi kufanya ziara za kikazi ndani ya mikoa tofauti na utamaduni wa viongozi wengi ambao leo wakinywa chai Ufaransa mchana hula UK - hii imemjengea sifa kubwa kwa wananchi na kuwa ktk orodha wa viongozi wanaoaminiwa;

(iii). Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma:-
Hapa kila mmoja ni shahidi kwamba hata zile kelele za ufisadi zilizokuwa zinapigwa zimepungua sana - ingawa anapaswa kuendelea kumulika zaidi kwa watendaji wake ili wasiingize masuala binafsi kwenye utendaji wa kila siku;

(iv). Ajali za barabani - zimepungua sana tofauti na miaka kadhaa ya nyuma;

Kwa ujumla sifa za kiungozi anazo nyingi, kama kuna kasoro sehemu basi ni zile za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo.

Rai yangu:-
Kwa kuwa amehiari kutuongoza kwa miaka mingine mitano (2020/2021 - 2024/2025) basi tukubali kwa wingi wetu kumchagua na kulinda kura zake ili zisihujumiwe na mahasimu wake wa kisiasa.

Nawasilisha kwa hatua zenu hapo 28/10
Najua Magufuli ni mpenzi wa mungu na hasemagi uongo.Muulize 2015 ilikuwaje
 
Yeye ni nani asishindwe na umesema hatowahi kushindwa! Ana maagano na Mtukufu Mwenyezi Mungu..? Au unafikiri kwa vile anapora mali za wanachi na anapofadhili mambo ya ajabu watendewe watu wengine ni jambo ambalo Mungu analikubari?

.........Acha kula bangi hiyo inayochanganywa na ugoro mkuu..
Mwenzio mtoa mada anaamini Magugu maji ndio Mungu
 
Mkuu nadhani umekosea kwenye kichwa cha habari ilikuwa kisomeke "
Magufuli hajawahi kushinda, hatashinda". Moderator please msaidie mleta uzi kwa kuondoa herufi 'w' kwenye neno 'kushindwa' ili liwe 'kushinda' badala yake.
 
Sifa zingine zinatolewa na wasiojua kufikiri. Hebu fikiri... kuanzia aanze shule ufaulu wake ulikuwaje? Hajawahi kushindwa? Mialiko yote hajawahi kushindwa kufika? Matatizo yote anayoletewa kutatua, je hajawahi kushindwa? Hata kutongoza, hajawahi kataliwa na na mwanamke? Sio kushindwa? Hata alipoanza kugombea ubunge, alishindwa mara ngapi?

ACHA KUMKUFURU MUNGU....
 
Back
Top Bottom