Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli kakataa treni ya umeme isifike Kigoma bali iende Mwanza?

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli kakataa treni ya umeme isifike Kigoma bali iende Mwanza?

Huruma siyo malezi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2020
Posts
1,433
Reaction score
3,210
Habari za humu wadau, poleni na hongereni na pilika za kampeni.

Juzi kati nimesikitishwa na kitendo cha mgombea kupitia kiti cha ccm ambaye kawaita watu wa kigoma kwamba wana akili sana,
nawakosoa kwa sababu,

Magufuli huyuhuyu kakataa katakata treni ya umeme isifike kigoma bali iende mwanza , huu mgogoro zitto kapiga kelele saaana akijaribu kuonesha umuhimu na utofauti uliopo kati ya reli kutoka mwanza na kigoma lakini huyo aliyewaita mna akili sana hakujali kwa ufupi hawatakii mema.

Bandari ilielezwa ijengwe kigoma kwa ajili ya kuimarisha shughuli nyingi kupitia ziwa Tanganyika lakini huyu anayewaita mna akili sana hilo nalo kakataa kapeleka mwanza.

Upande wa uwanja mkubwa wa ndege inasemekana na wenyew kakataa vilevile nadhani itakuwa ndo huo uliojengwa mbingu ya chato.

Siku zote ukiona mwanasiasa anakusifu wewe raia una akili sana au mwelewa shtuka mapema

N.B: Mtu asiyekubali kushindwa kwa chochote daima atapata lolote katika mda wowote.
 
Kuwaita mna akili sana ni mbinu ya kuwachota tu.

Jiwe kabadirisha plan ya awali ya reli ya SGR ambayo ilitakiwa iende Kigoma kwa ajili ya uwepo wa bandari ya Kigoma yenye kuhudimia Congo, Burundi etc, yeye kaipeleka mwanza ambako hakuna mzigo wowote wa maana kwenye bandari ya Mwanza.

Maamuzi ya kubadili plan ya uelekeo wa reli hiyo ni muendelezo uleule tu wa ukabila wa kutaka kupeleka reli "kwao" kama alivyojenga uwanja wa ndege Chato!
 
Kuwaita mna akili sana ni mbinu ya kuwachota tu

Tuna kazi nzito Chief tena yenye safari ndefu
 
Ngoja huyu tulie naye ajenge mpaka mwanza subiri atakaye kuja naye ata jenga kule mnapopataka, kama mama tibaijuka anavyosema "mnavyopanua ndivyo jinsi wanavyo tamani "ni vizuri kama mmeanza kuipenda treni.
 
Magufuli huyuhuyu kakataa katakata treni ya umeme isifike kigoma bali iende mwanza , huu

Kisiasa ilikuwa ni sawa reli ya umeme iende Kigoma lakini kibiashara reli ingeenda Kigoma ingekufa ndani ya mwaka kwa kushindwa kujiendesha.. Idadi ya abiria na mizigo wa Kigoma line hawatoshi kufidia hata robo ya running cost za reli ya SGR.. Kwa hiyo mradi ungekuwa white elephant kama reli ya nchi jirani.

Hiki ni kitu ambacho naamini hata wana Kigoma wenyewe wasingependa kitokee.

Hata hivyo, serikali imewekeza zaidi ya Bilioni mia tatu katika kukarabati reli ya Kigoma line sambamba na kutumia zaidi ya Bilioni hamsini kununua vichwa vipya katika kuboresha huduma za reli ya kati ambazo wana Kigoma ni wanufaika wakuu.

Hata hivyo reli ya SGR itarahisisha safari za wana Kigoma na wale wa Mpanda ambao bado wataweza kupandia treni za mwendo kasi kuanzia Tabora mpaka Dar.

Sambamba na hilo ujenzi wa bara bara ya lami kutoka Tabora mpaka Kigoma umeendelea japo sio kwa kasi inayotakiwa lakini naamini ipo siku bara bara hii itakamilika.

Sambamba na hayo serikali imehakikisha bara bara ya changarawe ya kutoka Tabora kwenda Dodoma (Manyoni) kupitia Itigi inapitika kipindi chote cha mwaka.. Bara bara hii ni kiungo muhimu katika kufupisha safari za kutoka Kigoma (Tabora) kuelekea Dodoma na hivyo mikoa mingine inayounganishwa na Dodoma.

Sambamba na hayo, watu wa Kigoma wamenunuliwa ndege mpya za Bombadier (De Havilland) ambazo wanazitumia bila wasi wasi.. Ndege hizi zimereplace ndege chakavu za Bombadier zilizokuwa mbili ambapo ndege moja ilianguka Kigoma wakati ikijiandaa kupaa kutokana na kufeli kwa injini.

Yaliyofanywa kwa wana Kigoma ni makybwa pengine kuliko mikoa mingi ya nchi hii.

Pengine nisichokiunga mkono ni kukarabatiwa (remanufacturing) kwa meli ya mv Lihemba ambapo wataalam walishauri badala ya kukarabati meli hiyo, inunuliwe meli nyingine.

Serikali katika ngwe hii ya pili iwajibike kutafuta pesa za kujenga meli mpya yenye kubeba mizigo na abiria kwa viwango angalau vinavyokaribiana na meli ya Mv Lihemba ambayo kulingana na riport ya wataalam walisema iko beyond repair.
 
Hii SGR si haipaswi hata kuendelea? Au tushasahau kama hatuitaki?
Kuwaita mna akili sana ni mbinu ya kuwachota tu

Jiwe kabadirisha plan ya awali ya reli ya SGR ambayo ilitakiwa iende Kigoma kwa ajili ya uwepo wa bandari ya Kigoma yenye kuhudimia Congo, Burundi etc, yeye kaipeleka mwanza ambako hakuna mzigo wowote wa maana kwenye bandari ya Mwanza.

Maamuzi ya kubadili plan ya uelekeo wa reli hiyo ni muendelezo uleule tu wa ukabila wa kutaka kupeleka reli "kwao" kama alivyojenga uwanja wa ndege Chato!
 
Kisiasa ilikuwa ni sawa reli ya umeme iende Kigoma lakini kibiashara reli ingeenda Kigoma ingekufa ndani ya mwaka kwa kushindwa kujiendesha.. Idadi ya abiria na mizigo wa Kigoma line hawatoshi kufidia hata robo ya running cost za reli ya SGR.. Kwa hiyo mradi ungekuwa white elephant kama reli ya nchi jirani.
Hiki ni kitu ambacho naamini hata wana Kigoma wenyewe wasingependa kitokee.
Hata hivyo, serikali imewekeza zaidi ya Bilioni mia tatu katika kukarabai reli ya Kigoma line sambamba na kutumia zaidi ya Bilioni hamsini kununua vichwa vipya katika kuboresha huduma za reli ya kati ambazo wana Kigoma ni wanufaika wakuu.
Hivi kiongozi ulishawahi kuulizia takwimu za faida ya reli kutoka kigoma to dar na mwanza to dar? Acheni masihara
 
Bandari ya Kigoma ni muhimu kwani inasaidia biashara. Kuna mizigo mingi inayoingia Afrika kupitia bahari na hushukia Ghana ambayo husafirishwa mpaka Congo na kufika Ziwa Tanganyika. Baadhi ya bidhaa hizi ni Hollandaise Wax au Vitenge vya Wax kutoka Holland.
 
Zito atapeleka reli Kigoma si yeye huwa anaongea na world bank.
Ninavyojua reli itatoka Mwanza mpaka Isaka kama sikosei kuna bandari pale inajengwa kwa ajili ya meli kupeleka mizigo ya Kongo Karemii. Pia nilisoma humu kwamba Burundi na Kongo wataunganisha reli hiyo stesheni fulani na hapo ndipo tawi la Kigoma litakapounganishwa. Subirini nchi nzima itaunganishwa na SGR network
 
Kwanza tulishasema hatutaki maendeleo ya vitu, cha kushangaza leo tunalia eti maendeleo ya vitu hayajapelekwa sehemu fulani
 
Mkuu Ugobha , acha uongo, miradi mikubwa ni mipango, kama iko kwenye plan SGR ifike Kigoma, itafika tuu, ila inajengwa kwa phases, hakuna cha hoja kuwa Magufuli kakataa usifike Kigoma, bali phase ya SGR ya Kigoma bado muda wake.

Uamuzi SGR ipi ianze, iko determined na business viability ya SGR kubeba mzigo mkubwa, SGR kutangulia kufika Mwanza kwa ajili ya mizigo ya Uganda ni more viable kuliko Kigoma.
Priority ni SGR ya Dar Moro Makotupora, Isaka hadi Rusumo.

Then SGR ya Mwanza, ndipo Kigoma inafuatia.
P
 
Kwahiyo kwa mantiki hiyo madai ya zitto hayakuwa na msingi?
 
Jsmbeniii, lakini Magufuli ndio Rais tumtakae wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom