Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Natamani kufika kila eneo kufanya kampeni lakini siwezi

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Natamani kufika kila eneo kufanya kampeni lakini siwezi

Siku hizi hata mwili anacheza kwa Michael sana ni mikono tu anayoosha
 
Makundi yenye maslahi ndani ya CCM watakumbuka walivyomkejeli Mbowe, Lissu na CHADEMA
Anavuka tu
IMG_20201014_194645.jpeg
 
Akihutubia jimbo la Kawe, Rais Magufuli amesema yeye ni Binadamu hataweza kwenda lindi na Mtwara hivyo atamtuma Kassim Majaliwa Kassim

Mimi kama mwana CCM naunga mkono kumtumia Mama Salma Kikwete na Jakaya Kikwete mikoa ya lindi na Mtwara na tayari hilo limefanyika.

Kwa uamuzi huu Rais ameona mbali sana na hongera kwake sana sana,

Wale wa maeneo ya Ngende, Nanjilinji na Nkanared na wale wanaotamka mwana Nke badala ya Mwanamke na mnaotamka Ntoto badala ya mtoto wa mikoa ya Lindi na Mtwara tunawategemea sana kupiga kura ya ndio kwa JPM.

Kazi za serikali ni nyingi zinahitaji muda pia.
----
Nilipenda sana kupita maeneo mbalimbali. Nilipenda nifike Mbagala; nitamtuma Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Nilipanga niende mpaka Ukonga mwisho, napo nitamtuma Mh. Jakaya Kikwete na viongozi wengine.

Nilipanga kupita kila eneo, lakini mimi ni binadamu. Ningependa hata nifike Katavi na Rukwa lakini ilibidi nimtume Makamu wangu wa Rais, Mama Samia.

Ningependa nifike Mtwara na Lindi lakini nitamtuma kule Waziri Mkuu wangu, Ndugu Kassim Majaliwa.

Ningependa nifike Morogoro; ningependa nifike Pwani; ningependa nifike Pemba na maeneo mengine. Mimi ni binadamu, siwezi kuwa kila mahali na wakati huohuo nifanye kazi za serikali.

Kwa sababu serikali lazima iendelee kwenda, wafanyakazi wapate mishahara yao. Madawa lazima yapatikane hospitali. Na mengine mengi. Wakulima lazima wapate pembejeo. Haya yote unayasimamia wakati ukifanya kampeni.
Anaogopa kujibu dhuluma ya korosho ama pumzi imekata? 🚮 🚮 🚮 🚮
 
14 October 2020

Nyerere alitembelea majimbo yote ya Tanganyika 1959 bila kuchoka kampeni za Uhuru



Kumbukumbu ya Nyerere wazee wanatoa ushuhuda na wakumbuka jinsi Mwl. Nyerere alivyotembelea majimbo yote ya nchi ya Tanganyika kuwaeleza wananchi wasiwe na hofu, uhuru wa Tanganyika unaweza kupatikana na si jambo la kufikirika lisilowezekana kama wananchi wakati ule walivyofikiria.

Mwaka 1959 mwezi October Mwalimu alitembelea Iringa aliambatana na mzee John Mwakangale mwanasiasa......

Vijana nao waliokuwa shule ya msingi mwaka 1995 pia wanakumbuka...
 
Aletewe Gwajima wa nini?
Badala ya kushawishi watu anawafokea.
Kama yeye anamtaka Gwajima basi amchukue, sio kulazimisha wana Kawe wamchague mcheza Porn.
 
Back
Top Bottom