Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ni kweli anajua maana ya kunadi sera?

Makala josee

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
511
Reaction score
447
Inasikitisha katika nyakati kama hizi za Demokrasia komavu kukutana na hoja dhaifu au za ajabu

Akiwa Lindi mgombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi ya Urais ndugu John Magufuli ambae kwa mujibu wa sheria ni Rais hadi hivi sasa, amenukuliwa akitishia Wananchi kutokuwapelekea Maendeleo kwa sababu walimchagua mbunge mpinzani ndugu Bwege.

Haikutosha hata alipokuwa kwenye kampeni wilaya ya Bunda amenukuliwa akiwananga Watanzania kwamba hawatayaona Maendeleo ikiwa watamchagua wabunge wasio wa CCM au wawakilishi.

Imenisikitisha kwa kweli Kwa zama tulizonazo kunaweza kujitokeza mtu wa level ya PhD kuwa na hoja dhaifu kiwango hiki.

1. Wawakilishi hupatikana baada ya uchaguzi hivyo si hatia.
2. Kupeleka Maendeleo majimboni kwa serikali iliyoko madarakani ni wajibu na si hiari.
3. Walipa kodi wa nchi hii sio wote wapiga kura, wanasiasa, wanachama wa vyama.
4. Suala la kutishia wananchi kwamba hawatayaona Maendeleo na wewe ni mgombea ni taswira mbaya kwamba una kiburi, jeuri na uko tayari kufanya lolote ili mradi ushinde.

Hitimisho: Ni wazi chama cha mapinduzi kimevimbiwa madaraka kwa kudhani chenyewe au wanachama wake tu, wao ndio wenye haki dhidi ya wengine.
 
Magufuli ni mweupe sana. Yaani isingekuwa Lowassa kuchafuliwa ufisadi, 2015 Lowassa angeshinda. Leo anasema eti tuchague chama na siyo mtu. Anasahau kuwa akishinda yeye ndo Mwenyekiti na kwenye chama wote watasema ndiyo mzee.

Mara aseme maendeleo hayana chama. Mara anawaponda waliochagua vyama vingine.
 
Jiwe sijawai muelewa kabsa pia uwa nashangazwa na wanaomuelewa, only Tz jiwe anaweza kuwa rais, kwa wenzetu huyu angekatwa ngazi ya kata

Anafikirisha kwa kweli
Hajawahi shinda chochote bila kubebwa, safari hii Mkapa hayupo thus amejaa fully stress, Safari bado Kagera wanamngoja awarudishie chenji za rambirambi, kusini wanamngoja akawape majibu ya korosho.
Hili jiwe linawezapasuka kabla ya wakati.

CD ya SGR, mabeberu, flyover, ndege haizuiki
 
Mwaka anasema wachague chama wakati 2015 waliomba achaguliwe Magufuli, wamebanwa.
 
Magufuli ni mweupe sana. Yaani isingekuwa Lowassa kuchafuliwa ufisadi.2015 Lowassa angeshinda. Leo anasema eti tuchague chama na siyo mtu. Anasahau kuwa akishinda yeye ndo mwenyekiti na kwenye chama wote watasema ndiyo mzee...
Amepanick huko anaongea kisukuma tu na tume ya uchaguzi iko kimya kanuni zikivunjwa waziwazi. Magufuli ni mvunja sheria namba moja ndani ya nchi hii, na hiki kiburi ni kwakuwa katiba inakataza rais kushitakiwa.
 
Sera za ubaguzi waziwazi, anabagua wapinzani huku Kodi zao anachukua. Ingekuwa analeta maendeleo mbona Dodoma yote ni CCM why hawana maendeleo.
 
Huyu magu hajui anachokifanya, Kama watanzania tunajielewa na tunaipenda nchi yetu, huyu tulipaswa kumuondoa kwenye ofisi ya umma iwe kwa kura au nguvu.
 
Amepanick huko anaongea kisukuma tu na tume ya uchaguzi iko kimya kanuni zikivunjwa waziwazi. Magufuli ni mvunja sheria namba moja ndani ya nchi hii, na hiki kiburi ni kwakuwa katiba inakataza rais kushitakiwa.
Kali leo kasema atanunua ndege sijui zilete madawa,watalii.Hivi hizi zilizopo zilishawahi leta watalii ?leta madawa ?Nchi yenyewe hata leseni hawana. Juzi hapa walikodi Rwanda air kupeleka samaki Ubelgiji.
 
Wana mawazo ya ujima bado, eti kufanya Mambo kwa lengo la kukamilisha ndoto za Nyerere wakati ndoto zingine ziliotwa miaka ya 60 ambapo mazingira na mahitaji ya wakati ule Ni tofauti na ya wakati wa Sasa.
 
Kali leo kasema atanunua ndege sijui zilete madawa,watalii.Hivi hizi zilizopo zilishawahi leta watalii ?leta madawa ?Nchi yenyewe hata leseni hawana. Juzi hapa walikodi Rwanda air kupeleka samaki Ubelgiji.
Kuwaambia Wana ikungi au ukara utawaletea ndege au nimejenga flyover ni kuwatukana.
Kila eneo linavipaumbele vyao.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Alizoea vya kunyonga kuwatisha watu live kavukavu hawezi. Afrika mashariki had Sudani Ni Kenyatta tu pekee ndo mwenye uwezo wa kujibu hoja bila msaada wa polisi.

Hata speech zake kweli zimepangika haziboi hazichoshi kusikiliza zinavutia ni Kama JK vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…