Makala josee
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 511
- 447
Inasikitisha katika nyakati kama hizi za Demokrasia komavu kukutana na hoja dhaifu au za ajabu
Akiwa Lindi mgombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi ya Urais ndugu John Magufuli ambae kwa mujibu wa sheria ni Rais hadi hivi sasa, amenukuliwa akitishia Wananchi kutokuwapelekea Maendeleo kwa sababu walimchagua mbunge mpinzani ndugu Bwege.
Haikutosha hata alipokuwa kwenye kampeni wilaya ya Bunda amenukuliwa akiwananga Watanzania kwamba hawatayaona Maendeleo ikiwa watamchagua wabunge wasio wa CCM au wawakilishi.
Imenisikitisha kwa kweli Kwa zama tulizonazo kunaweza kujitokeza mtu wa level ya PhD kuwa na hoja dhaifu kiwango hiki.
1. Wawakilishi hupatikana baada ya uchaguzi hivyo si hatia.
2. Kupeleka Maendeleo majimboni kwa serikali iliyoko madarakani ni wajibu na si hiari.
3. Walipa kodi wa nchi hii sio wote wapiga kura, wanasiasa, wanachama wa vyama.
4. Suala la kutishia wananchi kwamba hawatayaona Maendeleo na wewe ni mgombea ni taswira mbaya kwamba una kiburi, jeuri na uko tayari kufanya lolote ili mradi ushinde.
Hitimisho: Ni wazi chama cha mapinduzi kimevimbiwa madaraka kwa kudhani chenyewe au wanachama wake tu, wao ndio wenye haki dhidi ya wengine.