Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ni kweli anajua maana ya kunadi sera?

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ni kweli anajua maana ya kunadi sera?

Inasikitisha katika nyakati kama hizi za Demokrasia komavu kukutana na hoja dhaifu au za ajabu

Akiwa Lindi mgombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi ya URAIS ndugu John Magufuli ambae kwa mujibu wa sheria ni Rais hadi hivi sasa, amenukuliwa akitishia wananchi kutokuwapelekea Maendeleo kwa sababu walimchagua mbunge mpinzani ndugu Bwege.../QUOTE]AKIWA LINDI, LINI TENA? MLETA HOJA MBONA UNA #KIHERERE WACHA SINDANO ZIKUINGIE.
 
Enzi tuna ndege 1 watalii walikuwa wanakataa kuja.

A mattwr of preority nadhani mradi wa ndege ni ufisadi..

Kuna mtu atainja gereza one day.
Kali leo kasema atanunua ndege sijui zilete madawa,watalii.Hivi hizi zilizopo zilishawahi leta watalii ?leta madawa ?Nchi yenyewe hata leseni hawana. Juzi hapa walikodi Rwanda air kupeleka samaki Ubelgiji.
 
Labisa hii ndio solution.
Ni wakati Sasa kila Jimbo liwe na mamlaka kamili yanayojitegemea haya ya kuchukua mapato ya Kodi toka upinzani then kuwanyima maendeleo huu Ni wizi
 
Tufanye kama kenya.. kila jimbo liqe na serikali yale.
Ni wakati Sasa kila Jimbo liwe na mamlaka kamili yanayojitegemea haya ya kuchukua mapato ya Kodi toka upinzani then kuwanyima maendeleo huu Ni wizi
 
Magufuli ni mweupe sana. Yaani isingekuwa Lowassa kuchafuliwa ufisadi.2015 Lowassa angeshinda. Leo anasema eti tuchague chama na siyo mtu. Anasahau kuwa akishinda yeye ndo mwenyekiti na kwenye chama wote watasema ndiyo mzee.
Mara aseme maendeleo hayana chama. Mara anawaponda waliochagua vyama vingine.
2015 alikuwa anatuambia tuchague Magufuli,yaani ccm sijui wanatumia uchawi?
 
Kenyatta miaka 6 : gdp imekua kwa 39 USD Bil

Magufuli niaka 5 GDP imekua kwa 3 USD Bil
Alizoea vya kunyonga kuwatisha watu live kavukavu hawezi. Afrika mashariki had Sudani Ni Kenyatta tu pekee ndo mwenye uwezo wa kujibu hoja bila msaada wa polisi.
Hata speech zake kweli zimepangika haziboi hazichoshi kusikiliza zinavutia ni Kama JK vile
 
Magufuli ni mweupe sana. Yaani isingekuwa Lowassa kuchafuliwa ufisadi.2015 Lowassa angeshinda. Leo anasema eti tuchague chama na siyo mtu. Anasahau kuwa akishinda yeye ndo mwenyekiti na kwenye chama wote watasema ndiyo mzee.
Mara aseme maendeleo hayana chama. Mara anawaponda waliochagua vyama vingine.
Magufuli ni mbaguzi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sera zake hizo za kutoa VITISHO na kuwadhalilisha Watanzania.




Inasikitisha katika nyakati kama hizi za Demokrasia komavu kukutana na hoja dhaifu au za ajabu

Akiwa Lindi mgombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi ya URAIS ndugu John Magufuli ambae kwa mujibu wa sheria ni Rais hadi hivi sasa, amenukuliwa akitishia wananchi kutokuwapelekea Maendeleo kwa sababu walimchagua mbunge mpinzani ndugu Bwege.

Haikutosha hata alipokuwa kwenye kampeni wilaya ya Bunda amenukuliwa akiwananga watanzania kwamba hawatayaona Maendeleo ikiwa watamchagua wabunge wasio wa CCM au wawakilishi.

Imenisikitisha kwa kweli Kwa zama tulizonazo kunaweza kujitokeza mtu wa level ya PhD kuwa na hoja dhaifu kiwango hiki.

1. Wawakilishi hupatikana baada ya uchaguzi hivyo si hatia.
2. Kupeleka Maendeleo majimboni kwa serikali iliyoko madarakani ni wajibu na si hiari.
3. Walipa kodi wa nchi hii sio wote wapiga kura, wanasiasa, wanachama wa vyama.
4. Suala la kutishia wananchi kwamba hawatayaona Maendeleo na wewe ni mgombea ni taswira mbaya kwamba una kiburi, jeuri na uko tayari kufanya lolote ili mradi ushinde.

Hitimisho: Ni wazi chama cha mapinduzi kimevimbiwa madaraka kwa kudhani chenyewe au wanachama wake tu, wao ndio wenye haki dhidi ya wengine.
 
Victoire usisahau alishajiita KICHAA. Sasa kauli yake kuhusu UKICHAA wake inazidi kuthibitika.

Magufuli ni mweupe sana. Yaani isingekuwa Lowassa kuchafuliwa ufisadi.2015 Lowassa angeshinda. Leo anasema eti tuchague chama na siyo mtu. Anasahau kuwa akishinda yeye ndo mwenyekiti na kwenye chama wote watasema ndiyo mzee.
Mara aseme maendeleo hayana chama. Mara anawaponda waliochagua vyama vingine.
 
Lisu anakosea Sana badala ya kunadi sera za Chadema anatupa account ya tukio lake la kushambuliwa kwa Risasi.

Wanachadema nao wanaitisha NEC kuwa wasipompa Ushindi Lisu kitanuka.

Lisu anawatisha wapiga kura kwa risasi zake Chama nacho kinatisha kuvuruga amani kama Lisu hatatangazwa mshindi,

Upinzani mnatutishia .
 
Wana mawazo ya ujima bado, eti kufanya Mambo kwa lengo la kukamilisha ndoto za Nyerere wakati ndoto zingine ziliotwa miaka ya 60 ambapo mazingira na mahitaji ya wakati ule Ni tofauti na ya wakati wa Sasa.
Kwa hiyo yeye badala ya kutekeleza ilani ya chama chake aliamua kutekeleza ndoto za Nyerere? Sasa leo hicho anachotuahidi toka kwenye ilani tutaamini vipi atakitekeleza? Siamini kuwa JK anaweza kujitokeza na kwenda kumpiga campaign mtu asiyejielewa Kama huyu
 
Lisu anakosea Sana badala ya kunadi sera za Chadema anatupa account ya tukio lake la kushambuliwa kwa Risasi.

Wanachadema nao wanaitisha NEC kuwa wasipompa Ushindi Lisu kitanuka.

Lisu anawatisha wapiga kura kwa risasi zake Chama nacho kinatisha kuvuruga amani kama Lisu hatatangazwa mshindi,

Upinzani mnatutishia .
Huna hata hoja ya kum-defend jiwe,unaishia kutapatapa..nikiangalia andiko lako naona kabisa wewe ni mtu aliyekatishwa tamaa na mgombea wake ambae anazidi kujiharibia kila kukicha.
 
Inasikitisha katika nyakati kama hizi za Demokrasia komavu kukutana na hoja dhaifu au za ajabu

Akiwa Lindi mgombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi ya Urais ndugu John Magufuli ambae kwa mujibu wa sheria ni Rais hadi hivi sasa, amenukuliwa akitishia Wananchi kutokuwapelekea Maendeleo kwa sababu walimchagua mbunge mpinzani ndugu Bwege.

Haikutosha hata alipokuwa kwenye kampeni wilaya ya Bunda amenukuliwa akiwananga Watanzania kwamba hawatayaona Maendeleo ikiwa watamchagua wabunge wasio wa CCM au wawakilishi.

Imenisikitisha kwa kweli Kwa zama tulizonazo kunaweza kujitokeza mtu wa level ya PhD kuwa na hoja dhaifu kiwango hiki.

1. Wawakilishi hupatikana baada ya uchaguzi hivyo si hatia.
2. Kupeleka Maendeleo majimboni kwa serikali iliyoko madarakani ni wajibu na si hiari.
3. Walipa kodi wa nchi hii sio wote wapiga kura, wanasiasa, wanachama wa vyama.
4. Suala la kutishia wananchi kwamba hawatayaona Maendeleo na wewe ni mgombea ni taswira mbaya kwamba una kiburi, jeuri na uko tayari kufanya lolote ili mradi ushinde.

Hitimisho: Ni wazi chama cha mapinduzi kimevimbiwa madaraka kwa kudhani chenyewe au wanachama wake tu, wao ndio wenye haki dhidi ya wengine.
MAFISI ya CCM yamepoteana katikati ya msitu.
 
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.



CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.



It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.



What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka mwaka huu wa 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

Tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na hawa kupe wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali!. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwaondoa CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba mtu akikudanganya mara ya kwanza utakuwa na nafasi ya kumjua alivyo kwa tabia; na akija kukudanganya mara ya pili usikubali katu! Tumia uzoefu wa danganyo la kwanza ili kumkatalia. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hujitafutia chakula mwenyewe kwenye vichaka bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watalalamika sana. Watadhani unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wakajitafutie kama walivyozoea.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha mzigo mwepesi, atatamika sana. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa (birth right)! Ukimbebesha punda mzigo mwepesi ukikatiza karibu yake, lazima akupige mateke kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Ataona unamkwamisha katika harakati zake za ubebaji mizigo.

Nadharia hizi mbili zinafafanua maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu. Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wanakukiunga mkono kiendelee kubaki madarakani milele! Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kuendelea kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2020. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hivyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kupiga vita UFISADI kwa kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura, hapo 2019 (katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa) na 2020 (katika Uchaguzi Mkuu). Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (mafisadi wa CCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo aliyoyaleta mkoloni (pamoja na kwamba tulimuona mkoloni kuwa dhalimu na katili).

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa kuleta “maisha bora kwa kila mtanzania”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 9 alizoziacha Mkapa hadi 22! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi “maisha bora kwa kila mtanzania”, tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukaipigie kura CHADEMA ili ituondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hiyo ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi ( Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu, 2020!
 
Back
Top Bottom