Uchaguzi 2020 DKT. Magufuli: Sasa ni wakati wa kujali maslahi ya Wafanyakazi

Uchaguzi 2020 DKT. Magufuli: Sasa ni wakati wa kujali maslahi ya Wafanyakazi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amesema sasa ni wakati wa kujali maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania.

3C014760-D187-466A-8A95-7986FC587056.jpeg

Amesema kwa miaka mitano aliyoongoza ameweza kufanya nchi ifike uchumi wa kati wa chini na hivyo kwa miaka mitano inayofuata ataanza kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Amesema hauwezi kuongeza mishahara wakati hauna hela ya kuongeza mishahara. Aidha amesema hao wanasema kuhusu kuongeza mishahara hawajawahi kutawala.

Amesema wengine vyama vyao wameshindwa hata kujenga ofisi za vyama vyao. Amesema kuzungumza ni rahisi kuliko vitendo.
 
Dunia nzima hakuna vyama vyenye ofisi, ni Tanzania tu. Wapi ipo office ya Republican au Democratic? Tusidanganyane hapa, CCM imetuchangisha michango wakati wa mfumo wa chama kimoja kujenga maofisi ambayo leo hii ingekuwa mali ya serikali. Ofisi za vyama zinakuwa active wakati wa chaguzi tu. Hapo ndipo wanapokodi nyumba ya ofisi na si vinginevyo.

Uchumi wa chini kati tulishafikia tangu wakati wa Kikwete ila hakutaka ku-declare kwa sababu misaada ingepungua. Sasa huyu ili kutaka sifa akaona hilo litam-boost. By the way Tanzania bado ni nchi maskini sana, kati ya idadi yake ya watu Mil 58, Milioni 29 wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa. Msijifariji. SAFARI BADO NI NDEFU.
 
Hakuna mfanyakazi atakaa achague huyu dhalimu. Anajidanganya tu.

Si alijifanya kuwafokea! Leo maji yamemfika shingoni ndo anaanza kutapatapa. Ameshachelewa yaani.

Na ndio mnachokifanya hiki kupiga propoganda zilizojaa uzushi ili kuyumbisha msimamo wa Rais. Na akiyumba mnapata nafasi ya kumboa zaidi.

Huwezi kuficha ukweli kwamba moja ya vitu ambavyo JPM na serikali yacawamu ya 5bwamefanikiwa ni kudhibiti mfumuko wa bei. Isingesaidia saba kuongeza mishahara tena wakati mwengie kwa 20,000/- mpaka50,000/-.

Na matokeo ya kuongeza mshahara ya lete mfumuko wa bei unaokula ongezeko la matumizi ya mshahara jati ya 60,000/- mpaka 120,000/- Huu utakuwa ulaghai kwa wafanyakazi.
 
Watumishi wengi wamejaa madeni na hofu isiyokuwa na maana, weka pembeni huyu mwenyekiburi chagua Lissu
Hiyo kitu haiko kwenye Ilani ya chama kama zile million 50 za Kila kijiji na laptop kwa Kila mwalimu. Pesa iliyopo iko commited kwenye miradi mikubwa. Hivyo wa kubanwa ni wafanyakazi. Akiongeza mishahara tunakwama SGR.
 
Na ndio mnachokifanya hiki kupiga propoganda zilizojaa uzushi ili kuyumbisha msimamo wa Rais. Na akiyumba mnapata nafasi ya kumboa zaidi.

Huwezi kuficha ukweli kwamba moja ya vitu ambavyo JPM na serikali yacawamu ya 5bwamefanikiwa ni kudhibiti mfumuko wa bei. Isingesaidia saba kuongeza mishahara tena wakati mwengie kwa 20,000/- mpaka50,000/-.

Na matokeo ya kuongeza mshahara ya lete mfumuko wa bei unaokula ongezeko la matumizi ya mshahara jati ya 60,000/- mpaka 120,000/- Huu utakuwa ulaghai kwa wafanyakazi.
Sawa wamedhibiti mfumuko wa bei ya sukari kutoka 1,800/= mwaka 2015 mpaka 3,000/= mwaka 2020!

Marais wote waliomtangulia waliongeza mishahara walau kidogo na hii iliwasaidia sana waliokuwa wanastaafu.
 
Hiyo kitu hsiko kwenye Irani kama zile million 50 za Kila kijiji na laptop kwa Kila mwalimu. Pesa ikiyopo iko commited kwenye miradi mikubwa.... Hivyo wa kubanwa ni wafanyakazi. Akiongeza mishahara tunakwama SGR.
Sijakuelewa
 
Amesema hauwezi kuongeza mishahara wakati hauna hela ya kuongeza mishahara. Aidha amesema hao wanasema kuhusu kuongeza mishahara hawajawahi kutawala.
Siwezi kuongeza mshahara wakati sijamaliza miradi yangu mikubwa ya miundombinu. Kwa hiyo sasa hivi watumishi wasahau nyongeza ya mishahara sasa hivi!
 
Sawa wamedhibiti mfumuko wa bei ya sukari kutoka 1,800/= mwaka 2015 mpaka 3,000/= mwaka 2020!

Marais wote waliomtangulia waliongeza mishahara walau kidogo na hii iliwasaidia sana waliokuwa wanastaafu.
Wewe unatolea mfano sukari ambayo biashara yake inaendeshwa na genge la mafisadi waliojichimbia mizizi ya mbuyu ndani ya mifumo ya uendeshaji wa serikali. Toa mfano wa unga wa sembe tuone.
 
Back
Top Bottom