Mchimwachimego
JF-Expert Member
- Jun 15, 2020
- 358
- 271
Kwanza nakupa pongezi kwa kazi kubwa uliyoifanya kwa miaka mitano ya kutujengea miundombinu ambayo itakapokamilika itakuwa nyenzo nzuri ya maisha kwa wananchi wa kawaida ambayo kwa sasa wengi wao wanajifanya hawaioni, mladi kama bwawa la mwalimu nyerere utakaopunguza gharama za umeme na kupunguza matumizi ya mkaa na gharama za uzalishaji viwandani na sehemu nyingi ambazo umeme ndio kila kitu.
Nimekuwa nikikufuatilia kwenye kampeni zako mara nyingi uwa unataja yaliyofanyika ambayo kwa sisi waelewa wa masuala ya uchumi tunakuelewa ila wale waganga njaa waliokuwa wamezoea kula kirahisi hawawezi kukuelewa.
Mh rais kwa namna yoyote ile mwanadamu unapaswa kubadilika kutokana mazingira huyu msaliti na kibaraka wa mabeberu ni mjuaji na anajifanya ni muongeaji sana kupitia hilo watu wasiojua kuchambua pumba na mchele wanamshabikia sasa ili kumvunja nguvu na sisi lazima tuangalie yale anayoyazungumza sisi tunayageuza kwa kuongeza ubora au kuyafanya kitofauti.
Mfano mzuri 2015 wao walikuja na M4C wewe ulikuja na magufuli 4
changes, hivyo inawezekana kabisa kuwafanya wapinzani hoja zao zikawa hazina uzito kwa wewe kuamua kuzinyambua kitofauti.
(1) hoja yao ya machinga ni rahisi mno ukiwaeleza machinga kwamba pesa wanazotoa si kodi bali ni gharama za kukitengeneza lakini pia kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwapa thamani watambulike rasmi na huo ni mwanzo baadaye utaviboresha kwa kuwawekea picha na kuboresha utaratibu wao wa biashara kwa kuwapa maeneo ambayo yanaweza kuwa ya wazi na ukawawekea miundombinu wezeshi.
(2) hoja pesa kwamba hazipatikani hapa jibu lake rahisi tu kwamba miaka mitano iliyopita tulikuwa tunaboresha miundombinu ambayo ndiyo nyenzo ya uchumi ila sasa mkituchagua tena tunaenda sasa kuboresha maisha ya watu kwa kutoa tenda na miladi kwa makandarasi wazawa na kampuni binafsi pia nimepanga kuongeza mshahara 50%, ajila mpya 8000 na kuwasamehe waliotumikia kazi zaidi ya miaka 10 na kuendelea kwamba licha ya kwamba walitumia vyeti feki niwape kifuta jasho na kwa sababu makosa hayo yalifanya kwa sababu ujanja ujanja.
(3)hoja ya katiba hii nayo inapangulika waeleze wananchi katiba mpya iko palepale na mkinichagua kabla sijamaliza muda wangu itapigiwa kura ila nashauri kuna baadhi ya mambo yalejelewe upya na itapitishwa.
(4) hoja ya kilimo ,ufugaji na uvuvi hizi ni hoja ambazo unatakiwa uzielezee kwa ukubwa kwamba unampango wa kuchimba mabwawa ya kuvuna maji ya mvua na ya mito midogo midogo mabwawa ambayo yatafuga samaki yatafanya kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya watu majumbani na kunyweshea mifugo, pia uwaeleze wananchi kuwa unampango wa kuwakopesha
Pembejeo wakulima au kuwapa bule wale wasiojiweza au wakulima wadogo wadogo na pia unampango wa kufanya ubia na sekta binafsi kujenga viwanda vya mkakati kwa kila mkoa vitakavyoajili watu na baadaye vitaendeshwa na wananchi wenyewe serikali itakuwa waangalizi.
(5) hoja ya elimu unaweza kuwaeleza namna ambavyo mumeanza kutoa elimu bila malipo na mpango wenu ni kuakikisha itakapofika 2025 elimu ya juu itapunguzwa gharama kutoka ilipo na utaongeza muda wa kulipa mkopo na utajenga vyuo vingine kanda ya magharibi na kusini na utajenga shule za sekondary bweni kila kata
na Advance kila tarafa shule tatu.
(6) hoja ya uwekezaji kwamba sisi tunaruhusu uwekezaji na yeyote tunampokea ila lazima mwekezaji ajue tunataka win win na tutawawezesha wawekezaji wazawa ili tuweze kuwa na matrilionea watanzania, mh rais yapo mengi lakini kwa leo naishia hapa nawaomba na wengine wenye mapenzi mema na rais atililike ambayo anaweza kuyaongelea kwenye kampeni na ninaombi kwa wahusika msiufute wala kuunganisha na uzi mwingine nataka ujumbe umfikie muhusika.
Asanteni.