Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Siwezi kudanganya watumishi wa umma kuwa nitawapandishia mishahara!

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Siwezi kudanganya watumishi wa umma kuwa nitawapandishia mishahara!

Msema ukweli ni mpenzi wa Aliye juu ya yote.

Haiwezekani hata kama ni mimi ndiye kiongozi kusema uongo, watumishi wa umma nchi hii ndio wenye nafuu ya kila kitu kuanzia mikopo, ajira ya kudumu n.k.

Hivyo kuwaongezea mishahara na kila kitu huku sekta binafsi ikiangaika si sawa, kwanza wao ndio waliotamalaki kila mahala kwenye uwekezaji wa ndani huku wasiokopesheka wakifunga biashara zao.

Watumishi watosheke, waache Mh.Rais afanyie kazi sekta binafsi, kuimalisha miundombinu na kujenga uchumi imara kwa manufaa ya wote.
Kuongeza salary sio swala la kuamua mtu ni swala ambalo lipo kisheria.

Kama hataki kiongeza basi awaambie wabunge wa ccm wafute hiyo sheria.

NB: Jitahidi kuficha ujinga wako.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Projects zinazofanyika sasa zikikamilika zitakuwa na faida kubwa kwa vizazi vya sasa na baadae.
 
Duh..miaka 5 tena..wakati vitu vinapand bei vifaa vya ujenzi, mafuta, vyakula..[emoji24][emoji24] bora asingeongelea hil swala
Mwenye masikio na asikie, 5 mingine bila nyongeza
 
Hakikaa
IMG_20200905_183324.jpeg
 
Hayo ameyasema Leo akiwa mkoani Mara kwenye kampeni za kuomba kuchaguliwa kwa miaka mitano ijayo.

Ahadi hii imeniacha na maswali mawili Kama ifuatavyo: 1 Je huyu mgombea anawachukuliaje watumishi wa umma? Huwaona Kama wanaokula bure?, au makondoo tu wasio na lolote.! 2 Nini mtazamo wa watumishi juu ya ahadi hii?
========

DKT. MAGUFULI: Ukaacha kujenga reli ambayo italeta uchumi mkubwa, ukasema naipeleka hii kupandisha mishahara. Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, tumejenga katika nchi nzima vituo vya afya 487. Wanaotibiwa sio wakulima na wafanyabiashara, hata wafanyakazi wanatibiwa pale.

Kwa hiyo tuliamua hiyo fedha iende kwa kujenga vituo vya afya na dispensary zaidi ya elfu moja na kitu, hospitali za wilaya 99 na hospitali za rufaa zaidi ya tatu. Hizi hospitali zinawatibu pia wafanyakazi, zinawatibu pia watoto wa wafanyakazi.

Tumeamua kutoa elimu bure kwa watoto wetu kuanzia darasa la kwanza mpaka sekondari na mikopo ya chuo kikuu tukaiongeza mpaka bilioni 450 ili mtoto wa masikini nae aweze kupata mkopo atakapokuwa chuo kikuu.

Tumitumia trilioni 1.06, hizi fedha tungeweza tukawadanganya wafanyakazi tukasema tumewaongeza mishahara, kupanga ni kuchagua, tuliamua watoto wasome bure kwanza.

Sisi wafanyakazi tunawapenda na ndio maana tunatoa hizi huduma, ndio maana katika ilani ya uchaguzi inazungumzia juu ya maslahi ya wafanyakazi.



Hajielewi huyu. Huduma zote hizo watumishi wa umma wanazipata bure? Bila fedha watapanda hizo ndege? Bila fedha wataendesha magari kwenye hizo barabara? Bila fedha watanunua uniform za watoto? Na je thamani ya fedha imebaki ile ile miaka yote 5? Watoto kwenye familia zao hawajazaliwa kwa miaka 5? Mavazi hayajachakaa kwa miaka yote 5? Nyumba hazihitaji ukarabati kwa miaka yote 5? nk. Hivi huyu Rais tulimuokota wapi? Anafikiri watumishi wa umma wanalishwa bure kama yeye Ikulu? Hajui mshahara na daraja unalostaafu nalo ndicho kigezo cha stahiki zako za uzeeni? Sasa kwa miaka 5 wangapi wamepungukiwa stahiki hizo? Kwa akili hizi kweli huyu jamaa anastahili kupewa miaka mingine 5 ya URAIS? Yeye akimaliza muda wake wa URAIS ataendelea kutunzwa bure na Taifa maisha yake yote. Sasa watumishi wa umma wakistaafu watatunzwa na nani kwa mafao yapi? Kama huna uwezo wa kuongoza nchi tafadhali wapishe wengine usisubiri sanduku la kura.
 
Kuna watu walikua wanamtetea kwamba anaongeza mishahara. Kiko wapi sasa kasema mwenyewe hatoongeza. Kazi kwenu wafanyakazi, maisha yanapanda kila Siku lakini mshahara upo palepale.
Mzee Rungwe aliwahi kusema huyu mtu anakula bure, anavaa bure hajui shida zetu.
 
Msema ukweli ni mpenzi wa Aliye juu ya yote.

Haiwezekani hata kama ni mimi ndiye kiongozi kusema uongo, watumishi wa umma nchi hii ndio wenye nafuu ya kila kitu kuanzia mikopo, ajira ya kudumu n.k.

Hivyo kuwaongezea mishahara na kila kitu huku sekta binafsi ikiangaika si sawa, kwanza wao ndio waliotamalaki kila mahala kwenye uwekezaji wa ndani huku wasiokopesheka wakifunga biashara zao.

Watumishi watosheke, waache Mh.Rais afanyie kazi sekta binafsi, kuimalisha miundombinu na kujenga uchumi imara kwa manufaa ya wote.
Kwa lugha yako Watumishi ni wawekezaji wa ndani
 
Kama hawezi kufanya mazuri kwa wafanyakazi maana yake ata kwa wakulima,wafanyabiashara na sekta zingine zote hawezi kuwafanyia mema.huo ndio ukweli.
Wakati sahihi ukifika tumwombee kazi ya kusimamia miundombinu,kwa anayekuja.
 
Back
Top Bottom