Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Siwezi kudanganya watumishi wa umma kuwa nitawapandishia mishahara!

Kuongeza salary sio swala la kuamua mtu ni swala ambalo lipo kisheria.

Kama hataki kiongeza basi awaambie wabunge wa ccm wafute hiyo sheria.

NB: Jitahidi kuficha ujinga wako.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Projects zinazofanyika sasa zikikamilika zitakuwa na faida kubwa kwa vizazi vya sasa na baadae.
 
Duh..miaka 5 tena..wakati vitu vinapand bei vifaa vya ujenzi, mafuta, vyakula..[emoji24][emoji24] bora asingeongelea hil swala
Mwenye masikio na asikie, 5 mingine bila nyongeza
 

Hajielewi huyu. Huduma zote hizo watumishi wa umma wanazipata bure? Bila fedha watapanda hizo ndege? Bila fedha wataendesha magari kwenye hizo barabara? Bila fedha watanunua uniform za watoto? Na je thamani ya fedha imebaki ile ile miaka yote 5? Watoto kwenye familia zao hawajazaliwa kwa miaka 5? Mavazi hayajachakaa kwa miaka yote 5? Nyumba hazihitaji ukarabati kwa miaka yote 5? nk. Hivi huyu Rais tulimuokota wapi? Anafikiri watumishi wa umma wanalishwa bure kama yeye Ikulu? Hajui mshahara na daraja unalostaafu nalo ndicho kigezo cha stahiki zako za uzeeni? Sasa kwa miaka 5 wangapi wamepungukiwa stahiki hizo? Kwa akili hizi kweli huyu jamaa anastahili kupewa miaka mingine 5 ya URAIS? Yeye akimaliza muda wake wa URAIS ataendelea kutunzwa bure na Taifa maisha yake yote. Sasa watumishi wa umma wakistaafu watatunzwa na nani kwa mafao yapi? Kama huna uwezo wa kuongoza nchi tafadhali wapishe wengine usisubiri sanduku la kura.
 
Kuna watu walikua wanamtetea kwamba anaongeza mishahara. Kiko wapi sasa kasema mwenyewe hatoongeza. Kazi kwenu wafanyakazi, maisha yanapanda kila Siku lakini mshahara upo palepale.
Mzee Rungwe aliwahi kusema huyu mtu anakula bure, anavaa bure hajui shida zetu.
 
Kwa lugha yako Watumishi ni wawekezaji wa ndani
 
Kama hawezi kufanya mazuri kwa wafanyakazi maana yake ata kwa wakulima,wafanyabiashara na sekta zingine zote hawezi kuwafanyia mema.huo ndio ukweli.
Wakati sahihi ukifika tumwombee kazi ya kusimamia miundombinu,kwa anayekuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…