Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli unamtenga Jakaya Kikwete kwenye Kampeni zako, kumbuka ndiye aliyekupa Urais 2015. Muangukie akusaidie

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli unamtenga Jakaya Kikwete kwenye Kampeni zako, kumbuka ndiye aliyekupa Urais 2015. Muangukie akusaidie

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Salaam,

Wakuu, Huu mwenendo wa hiii CCM na Mgombea wake kutaka kumuangushia jumba bovu Kikwete, haikubariki. Na kwenye Kampeni za 2020, Msipomshirikisha, CCM itapata kura za aibu. Mtaishia kuiba kura ili kuficha aibu. Sasa mnamchafua Kikwete kwamba kaharibu kwamba hajafanya lolote, basi hata ungemshukuru kwa kukuweka Ikulu na kukufanya ukubalike Geita.

Kwa miaka mitano wamekuwa wakisema hajafanya kitu. Kila siku wanasema vitu vyote kafanya Magufuli. Eti barabara kajenga Magufuli, Madaraja, Hospital, Shule na Maji nk kwamba Magufuli ndo kajenga. Hawana hata aibu.

Ni Kweli Rais Mstaafu Kikwete ana Mapungufu yake lakini aliacha Tanzania ikiwa Moja na amani. Hapakuwa na chuki za Kikabila, Kidini wala Kichama. Sasa hivi CCM na CHADEMA hawazikani. CCM inavibagua vyama vingine na kuviita vya Mabeberu, Wasaliti, Wachochezi na Kila jina baya. Kumbukeni vyama vyote vinaongozwa na Watanzania na Wanachama ni Watanzania.

Kipindi cha Kikwete alikuwa anakusanya Kodi kidogo Wastani wa Bil 800 hadi 900, lakini alikuwa anafanya Vitu vinaonekana. Mishahara ilikuwa ikiongezwa, Watu wanaajiliwa, Watu hawabambikiwi kesi za Uhujumu Uchumi, Watu walikuwa hawalipishwa Kodi ya kukomoa na mengine mengi tu.

Lakini Awamu ya Tano wanadai Wanakusanya Kodi Trilioni 1.2 hadi 1.8, Lakini Walichokifanya hakionekani. Tunasoma kwenye karatasi tu kwamba Viwanda 8,000 Shule zimejengwa na Barabara. Mwisho wa Siku unaona barabara ni zilezile za Kikwete alizojenga nyingine akatoka hazijaisha.

Kwa Miaka Mitano Magufuli hana kitu chake alichokuja nacho Mkoni au wazo lake la kututoa Watanzania Kwenye Umasikini. Kila anachojivunia ni Mawazo na Fikra za Watangulizi wake. Mfano;

1. Kuhamia Dodoma ni Idea ya Mwalimu Nyerere
2. Stiegler's Gorge ni Idea ya Nyerere
3. Flyover zote ni Idea za Jakaya Kikwete
4. TASAF ni Idea ya Mkapa
5. Umeme Vijijini REA ni Idea ya Kikwete nk.

Ila ambacho naona Kajitahidi Magufuli ni
1. Kuminya Uhuru wa Kutoa na Kupata habari
2. Vyama vinavyoshindana na CCM kuitwa vyama vya kiharifu na kwamba ni Wasaliti
3. Watu kutekwa na kupotea
4. Chuki miongoni mwa Watanzania(Hamna Umoja wa Kitaifa hata kwenye mambo ya Kitaifa(Mazishi ya Mkapa ni Mfano)
5. Bunge, Mahakama na Wanaamuliwa cha kufanya.

Dr. Magufuli bado anayo nafasi ya Kumuangukia Jakaya Kikwete ili ampe Ushauri na Support kwenye Uchaguzi huu. Vinginevyo Magufuli ataendelea Kufanya Ziara na Bonanza akidhani ndo Kampeni.
 
Sio kamtenga wao ndio wamemtenga si unaona kampeni anajinadi mwenyewe?

Iko wapi ile ccm ya jk 2015 ike timu hivi unaikumbuka?kwa sasa hata ile amshaamsha haipo.tushazoea barabara zote kipindi kama hivi mabango mwanzo mwisho na bendeza kila mahali.

Kwa sasa kampeni inafanywa kama vile bendeza ziko nusu mlingoti
 
Kwa Miaka Mitano Magufuli hana kitu chake alichokuja nacho Mkoni au wazo lake la kututoa Watanzania Kwenye Umasikini. Kila anachojivunia ni Mawazo na Fikra za Watangulizi wake. Mfano;

1. Kuhamia Dodoma ni Idea ya Mwalimu Nyerere...

Ila nasikia kwa utaratibu wa CCM, kila Rais anatekeleza sehemu ya pili ya mpango mkakati wa mtangulizi wake. Kwa hiyo kama akishinda atatekeleza wa kwake kuanzia 2020-2025.
 
Nadhani JK, Kanali Kinana Abdulrahman, Mzee Makamba Yusuph na wengine kibao wamewekwa kama jeshi la akiba. Nahisi ndani ya masiku haya hamsini na ushei yaliyobaki ajili ya kampeni wataambiwa wavae jezi waingie kubadilisha hali ya mchezo.

Wenyewe CCM wanatamba kuwa wanazo mbinu 105 za kushinda chaguzi na hadi sasa inatumika mbinu moja tu kati ya hizo. Tusuburi tuone ila mpambano ni mkali sana
 
Mlisema kinana ndiye mastermind wa ushindi [emoji3][emoji3][emoji3]
Mmeanza kuweweseka
 
Salaam,

Wakuu, Huu mwenendo wa hiii CCM na Mgombea wake kutaka kumuangushia jumba bovu Kikwete, haikubariki.

Na kwenye Kampeni za 2020, Msipomshirikisha, CCM itapata kura za aibu. Mtaishia kuiba kura ili kuficha aibu...
Ni bora ajitenge kila mtu abaki na mapungufu yake.
 
Sio kamtenga wao ndio wamemtenga si unaona kampeni anajinadi mwenyewe?
Iko wapi ile ccm ya jk 2015 ike timu hivi unaikumbuka?kwa sasa hata ile amshaamsha haipo.tushazoea barabara zote kipindi kama hivi mabango mwanzo mwisho na bendeza kila mahali.
Kwa sasa kampeni inafanywa kama vile bendeza ziko nusu mlingoti
Jamaa Tanzania bara anajiamin atashinda kwasababu ya TISS, NEC na wakurugenzi
 
Ni ngumu sana kujua Magufuli ni Mtu Wa namna gani...anaweza akaamka akawaambia kuwa "maendereo hayana chama" au "Mimi ni raisi Wa Watanzania wote na ninawapenda sana ndugu zangu au nasema uongo jamaniii!!"

sasa siku akiamka na maruhani kichwani utachoka mwenyewe kumsikiliza kwa pumba atakazotoa, yaani hapo CCM ndio chama cha maana vingine takataka, hapo Maendeleo yanakuwa na chama (yanawahusu wavaa nguo za kijani tu) vyama vingine vinakuwa mashetani...hebu angalia hiki kituko, Wazungu wakitupa misaada ya kifedha anawaita "Wahisani wetu wa maendereo hawa!"

At the same time haohao waliompa pesa wakimshauri au wakitoa takwimu zinazogusa maslahi yake anawaita "Mabhebheru hawa". Dah! Ni ngumu sana kujua huyu mtu kichwa chake kipoje.
 
Nadhani JK, Kanali Kinana Abdulrahman, Mzee Makamba Yusuph na wengine kibao wamewekwa kama jeshi la akiba. Nahisi ndani ya masiku haya hamsini na ushei yaliyobaki ajili ya kampeni wataambiwa wavae jezi waingie kubadilisha hali ya mchezo. Wenyewe CCM wanatamba kuwa wanazo mbinu 105 za kushinda chaguzi na hadi sasa inatumika mbinu moja tu kati ya hizo. Tusuburi tuone ila mpambano ni mkali sana
Mbinu yao ya mwisho na uhakika kwa CCM ni kukimbia na mabox ya kura.
 
Sawa, lakini hujiulizi kwanini idea ya Mwalimu Nyerere haukutekelezwa na Marais mwinyi, Mkapa, kikwete? Magufuli katekeleza anastahili pongezi.
 
Kwa nini kila kitu mnakiwaza kwa ubaya!? Je. Hamuoni kuwa Mgombea wa CCM kaamua kutokuwasumbua wazee hawa ambao wamelitumikia taifa kwa muda mrefu? Kamati ya Kampeini labda imeona wazee hawa waachwe wapumzike wafurahie maisha yao ya kustaafu na wafaidi pia misingi imara waliyoiweka ya CCM. Kama wakiamua kusaidia kampeini itakuwa kwa ajili ya kujiburudisha. Tuwaze positively!
 
Sio kamtenga wao ndio wamemtenga si unaona kampeni anajinadi mwenyewe?
Iko wapi ile ccm ya jk 2015 ike timu hivi unaikumbuka?kwa sasa hata ile amshaamsha haipo.tushazoea barabara zote kipindi kama hivi mabango mwanzo mwisho na bendeza kila mahali.
Kwa sasa kampeni inafanywa kama vile bendeza ziko nusu mlingoti
Kampeni za namna unayosema wewe, hua zinafanyika kipindi ambapo mtu mpya ndani ya CCM ameteuliwa kugombea Uraisi, hapo lazima atapewa support na amshaamsha ya kutosha,Sasa mkuu mtu tayari Ni rais, Dola inamtii yeye, afu mtumie nguvu ili iweje🤔? Jaribu kulinganisha hata kampeni za kikwete 2005, na zile za 2010 alipokuwa Ni rais tayari, utagundua kitu.Au za mkapa wakati anaingia 1995 na zile za 2000.
 
Sawa, lakini hujiulizi kwanini idea ya Mwalimu Nyerere haukutekelezwa na Marais mwinyi, Mkapa, kikwete? Magufuli katekeleza anastahili pongezi.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Walibanwa na Katiba. Ingekua Awamu ya Urais ni miaka 15 au 20. Miradi yote ingekamilika. Hata Magufuli hatamaliza atakuja mwingine atafanya. Haiondoi kwamba Magufuli alifanya kitu. Au sio?
 
Mlisema kinana ndiye mastermind wa ushindi [emoji3][emoji3][emoji3]
Mmeanza kuweweseka
Kwanini Rais Magufuli haongezi Mishahara wala kulipa mafao wakati Kodi imeongezeka mara dufu zaidi ya Kikwete. Kwanini anashindwa Kuwahudumia Wananchi kama Kikwete alivyokuwa anahudumia?
 
Back
Top Bottom