Mbona unarudia rudia Ulichosema Mwanzo Sawa JPM hataweza kuajiri
Tupe ways basi Za kutoa Ajira kwa vijana
Kwanza kabisa serikali inatakiwa kuondoa ukiritimba katika biashara.
Kuondoa milolongo ya kodi na vibali.
Pili serikali inatakiwa kujitoa kwenye biashara za white elephant projects kama kununua midege mikubwa ambayo kuiendesha gaharama yake ni kubwa sana na sekta binafsi ilishaanza kujiweka vizuri kuendesha biashara ya ndege.
Serikali inatakiwa kutumia nafasi yake kuwezesha vijana kufanya biashara ndogondogo na za kati zitakazoongeza mzunguko wa fedha na kuzalisha zaidi, siyo kufungia pesa nyingi katika white elephant projects ambazo hazifanyiwi hata audits wala kufuata tender process. Hili ni chaka la ufisadi mamboleo tu.
Tatu serikali inatakiwa kuwa na muelekeo. Sio mara inajitoa katika biashara na kuuza nyumba za umma. Mara inajirudisha katika biashara na kununua ndege na kuingilia biashara ya korosho.
Serikali ya Magufuli imeangusha mapato ya kilimo kutoka nje kwa silimia 55 mwaka ulioishia September 2019. Kwa kiasi kikubwa jwa sababu ya kuingikia biashara ya korosho. Ripoti ya Bank of Tanzania ndiyo imesema hilo.
Nne, serikali iache kuingilia mzunguko wa fedhs kwa makusudi na kulazimisha taasisi zake zifanye banking wapi kwa nia ya kuhodhi fedha za umma. Taasisi za umma zipewe uhuru wa kufanya biashara popote penye tija na ufanisi.
Tano, ajira zitolewe kwa watu wenye uwezo. Sio watu wenye connection.
Tano, rais aache kusema maneno ovyo ovyo. Ana undermine uchumi wa nchi. Watu wengine wakiona nchi ina rais msema ovyo hawawekezi kwenye nchi hiyo. Mambo mengine tukijipanga kidogo tu kwenye Public Relations and Messaging, mengine yatatengemaa.
Sita, rais aache kujifungia ndani kama mwali na kukataza watu kusafiri. Rais ana kazi ya kuwakilisha nchi ndani na nje ya nchi. Kujifungia ndani anatukosesha fursa nyingi za biashara na kujumuika kimataifa.
Saba, serikali inabidi ijikite katika research and develooment kuqnzia mambi ya uchumi mpaka sayansi. Kwa sasa mambo yanaenda kisiasa zaidi bila kujali uchumi wala sayansi.
Nane, serikali inabidi ijikite kutumia vizuri zaidi rasilimqli zetu za ndani. Fiscal policy itumike kuchochea maendeleo. Mifuko ya oensheni itumike kwenye shughuli zenye maendeleo ya kiuchuni na si kisiasa kama sasa. VAT itumike vizuri kwenye diatribution impact. Incentives na sera ziwekwe kuwndeleza na kupata kodi sahihi kutoka sekatq isiyo rasmi.
Tisa, sera ya taifa kuhusu extractives ijikite kuwa rafiki kwa mazingira na endelevu zaidi ili kuchangia uwezo wa kujiondoa katika a "rent seeking economy". Kuna migodi kama Buzwagi huko madini yashaisha yamebaki mashimo tu. Pia inqbidi tuwe business friendly zaidi, serikali isione wawekezaji maadui, ika walipe kodi na kudhibitiwa wasituibie. Kwa sasa wawekezaji ni kama maadui.
Kumi, land reform. Ni wakati sasa tuondokqne na habari za Ujamaa za serikali kumiliki ardhi na kukodisha watu. Hii ni moja ya sababu wawekezaji serious hawataki kuwekeza Tanzania. Utawekezaje kilimo cha mashambq makubwa na kutia ajira kwa watu kama simu yoyote serikali inaweza kutaifisha ardhi yako kwa kisingizio chochote bila hata malipo?
Bonus point.
Miradi ya kijilingajinga ya kisiasa kama kuhamisha mji mkuu kwenda Dodoma, ambayo sio tu haina ufanisi wa kiuchumi, bali pia ina gharama kubwa, itupiliwe mbali.
Naweza kuandika point mia kama hizi. Na hizi sijaandika kwa order ya umuhimu.
Ila kwa keo niishie hapa.