Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake

Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake

USIPOJIFUNZA KWA KUSIKIA,
UTAJIFUNZA KWA KUONA (MATOKEO).

Walianza na KUKU, sasa NGURUWE, unakuja mradi wa MBUZI
Bila kuwasahau wale JATU, eti ww unawapa hela wao wanakulimia na kukupa faida. Yaani ww ulale tu nyumbani mtu mwingine akufanyie kazi😂😂😂😂
 
Last week wakati naona video ya Dotto magari akiwa kijiji cha nguruwe nilikomenti kuwa biashara ile ni ya kitapeli.
Watanzania tutumie akili vizuri hata kama IQ zetu ni tia maji tia maji
Kwa hiyo dotto magari,akiwahamasisha watu na watu wanajaa kweli 😄

Ova
 
Haya sasa sema kimeumana Dr. Manguruwe akaliwa kooni adaiwa katapeli watu. Bwebwe nyingi huko mtandaoni kumbe nyuma ya camera anayake mambo
===================
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotarajiwa kampuni ya Pig Investment International (Kijiji cha Nguruwe) inayomilikiwa na Simon Mkondya (Dr. Manguruwe) imenyooshewa kidole ikidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia wito wake wa kuwekeza kwenye kampuni hiyo

Taarifa za kuaminika ilizonazo Jambo TV zinadai kuwa kampuni hiyo inadaiwa mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi wa maeneo tofauti nchini ambao kwa kiasi kikubwa wengi walishawishika kujiunga na kuwekeza kwenye 'Kijiji cha Nguruwe' kufuatia taarifa na matangazo yaliyokuwa yanatolewa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo kituo cha radio cha Wapo, ambapo uwepo wa matangazo hayo umetengeneza ushawishi mkubwa kwa jamii wa kuamini kuwa fedha zao zingekuwa salama pindi wakiwekeza kwenye kampuni hiyo jambo ambalo kiuhalisia wengi wao kwa sasa wanajuta

Soma Pia: Walimu wanne wakamatwa wakituhumiwa kufanya utapeli kwa safaru ya kimtandao Mwanza

Jeremiah Magesa, mkazi wa Mbagala, Temeke, jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa waathirika wa utapeli huo ambapo katika mazungumzo yake na Jambo TV amedai kuwa awali alipata taarifa ya uwepo wa kampuni hiyo kupitia matangazo yaliyokuwa yakisikika kwenye kituo cha radio cha Wapo, kituo kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo hamasa ya tangazo lililokuwa linaendelea lilimshawishi naye kuitafuta kampuni hiyo kwa ajili ya kuanza uwekezaji

Amesema alianza uwekezaji wake mnamo Mei 21.2024 ambapo aliwekeza shilingi milioni 1.4 na kwamba walikubaliana kuwa yeye atakuwa akipokea shilingi laki 1 na elfu 40 kila wiki kwa muda wa miezi sita, lakini katika simulizi yake anadai kuwa makubaliano hayo yalieanda sawa ndani ya muda wa wiki tatu tu za mwanzo ambapo kwa ujumla wake alipatiwa shilingi laki 4 na elfu 20, tangu hapo hajapokea kiasi chochote cha pesa hadi sasa

Sambamba na huyo, yuko mtu mwingine aliyejitambulisha jina la Modest Emmanuel Kanan, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo yeye anadai kuwa aliwekeza mtaji wa shilingi milioni 1.
Hivi watu hawajifunzi kwa tapeli Mr Manguruwe? Kwani ni mara ya kwanza kufanya utapeli? Huu mradi wa nguruwe ni kama utapeli wake watatu ,anafanya anapiga watu MPUNGA anasepa anaenda kuanzisha mradi mwingine mazombie yanajaa tena anapiga MSHINDO anasepa ,anaanzisha mradi mwingine anawaingiza 18 anasepa na Kijiji tena lakini watu hawastuki sijui binaadamu tuna ubongo wa kuku?
 
Back
Top Bottom