Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake

Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake

Bila kuwasahau wale JATU, eti ww unawapa hela wao wanakulimia na kukupa faida. Yaani ww ulale tu nyumbani mtu mwingine akufanyie kazi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Hata Bakhresa au Mo hawalali wanachakalika ila mwenzangu na mie anataka alale mr kuku au Mr manguruwe amfugie yeye awe anamumtumia tu kwenye simu huku yeye amelala ๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜€
 
Aise,na wabongo wakisikia hivyo
Wanajaaa ๐Ÿ˜„

Ova
Sio wabongo tu nadhani Afrika kwa ujumla hasa kusini mwa jangwa la sahara. Zambia kuna jamaa alisifiwa hadi na Rais kwenye mambo ya ujasiriamali kumbe ni tapeli FIRST CLASS.. sasa hivi anaishi kama digidigi baada ya kuwapiga watu.
 
Doto alisema nguruwe anakula laki 3 kwa siku ....Vyombo vya habari na celebrities wataendelea kutangaza utapeli milele, kama hutotumia akili yako basi utapigwa kila siku .
 
Dogo alisema nguruwe anakula laki 3 kwa siku ....Vyombo vya habari na celebrities wataendelea kutangaza utapeli milele, kama hutotumia akili yako basi utapigwa kila siku .
Tena hao ndiyo wanawatumia

Ova
 
Jamaa ana akili sana,
wawekezaji wake kina Ismael, Rajabu, Omary, abdallah.
Hawa kujitokeza hadharani kulalamika ni ngumu.
 
Hata Bakhresa au Mo hawalali wanachakalika ila mwenzangu na mie anataka alale mr kuku au Mr manguruwe amfugie yeye awe anamumtumia tu kwenye simu huku yeye amelala ๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜€
Imagine ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Haya sasa sema kimeumana Dr. Manguruwe akaliwa kooni adaiwa katapeli watu. Bwebwe nyingi huko mtandaoni kumbe nyuma ya camera anayake mambo
===================
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotarajiwa kampuni ya Pig Investment International (Kijiji cha Nguruwe) inayomilikiwa na Simon Mkondya (Dr. Manguruwe) imenyooshewa kidole ikidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia wito wake wa kuwekeza kwenye kampuni hiyo

Taarifa za kuaminika ilizonazo Jambo TV zinadai kuwa kampuni hiyo inadaiwa mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi wa maeneo tofauti nchini ambao kwa kiasi kikubwa wengi walishawishika kujiunga na kuwekeza kwenye 'Kijiji cha Nguruwe' kufuatia taarifa na matangazo yaliyokuwa yanatolewa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo kituo cha radio cha Wapo, ambapo uwepo wa matangazo hayo umetengeneza ushawishi mkubwa kwa jamii wa kuamini kuwa fedha zao zingekuwa salama pindi wakiwekeza kwenye kampuni hiyo jambo ambalo kiuhalisia wengi wao kwa sasa wanajuta

Soma Pia: Walimu wanne wakamatwa wakituhumiwa kufanya utapeli kwa safaru ya kimtandao Mwanza

Jeremiah Magesa, mkazi wa Mbagala, Temeke, jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa waathirika wa utapeli huo ambapo katika mazungumzo yake na Jambo TV amedai kuwa awali alipata taarifa ya uwepo wa kampuni hiyo kupitia matangazo yaliyokuwa yakisikika kwenye kituo cha radio cha Wapo, kituo kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo hamasa ya tangazo lililokuwa linaendelea lilimshawishi naye kuitafuta kampuni hiyo kwa ajili ya kuanza uwekezaji

Amesema alianza uwekezaji wake mnamo Mei 21.2024 ambapo aliwekeza shilingi milioni 1.4 na kwamba walikubaliana kuwa yeye atakuwa akipokea shilingi laki 1 na elfu 40 kila wiki kwa muda wa miezi sita, lakini katika simulizi yake anadai kuwa makubaliano hayo yalieanda sawa ndani ya muda wa wiki tatu tu za mwanzo ambapo kwa ujumla wake alipatiwa shilingi laki 4 na elfu 20, tangu hapo hajapokea kiasi chochote cha pesa hadi sasa

Sambamba na huyo, yuko mtu mwingine aliyejitambulisha jina la Modest Emmanuel Kanan, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo yeye anadai kuwa aliwekeza mtaji wa shilingi milioni 1.
Wabongo wanapenda kutapeliwa maana mambo mengine hayahitaji kuwa na PhD kujua kuwa ni wizi na utapeli. Kwanza inadaiwa jamaa aliwatapeli wakulima huko kabla ya kuja na hii eti manguruwe.
Hii yani ni wazi kuwa ni pyramid scheme. Matapeli wa hivi hawaishi kwa sababu huwa hawafungwi huenda wanakula na vyombo vya usalama na pia watanzania nao wanapenda kutapeliwa.
 
Dogo alisema nguruwe anakula laki 3 kwa siku ....Vyombo vya habari na celebrities wataendelea kutangaza utapeli milele, kama hutotumia akili yako basi utapigwa kila siku .
Na hizi media,wasanii sjui influencer wanawatumia kuwaingiza King mafala

Ova
 
Back
Top Bottom