Dkt. Mashinji: Huwezi ukawatofautisha Serikali, Mahakama na Bunge. Hata Mbinguni kuna Baba, Mwana na roho lakini maamuzi ni yaleyale

Haya. Twende. Taifa huru miaka 60 bado tu changa? Basi limedumaa. Na wakulaumiwa kwa udumavu huu ni CCM. Ndugu yangu Mashinji naona unatafuta ka-uteuzi. Kazana kutupa madongo kule ulikotoka. Njaa uliyonayo itayeyuka.
 
Sasa miaka50 ya uhuru unataka tulingane na wale wa miaka 250 ya uhuru...? Tena wale waliotuibia na wanalazimisha kuendelea kutuibia?
Tutafika walipo safari ni hatua
kitendo tu cha hata kushindwa kuchaguana karne hii ya 21, yaani kifupi hustahili hata kuitwa mwanadamu kwa kweli.
 
Umekuja kujipigia debe Dokta Mashinji. Subiri utapewa ukuu wa wilaya.
 
Ujinga tena huu, labda hivyo vitu havitenganishwi kwa Afrika tu. Alafu ni ujinga kulinganifa hivyo vitu na utatu mtakatifu
 
Hebu fafanua haya maneno ulioandika
Executive
Serekali
Bunge
Mahakama
Dola
Naona kama umetuchanganyia hujaeleweka kisha utuambie mihili mitatu ni ipi kati ya hiyo au kuna mihimili mi5?
 
Yuko meza kuu hivyo lazima aimbe nyimbo anazopenda kuzisikia mkuu wa meza.
 
Tanzania sio changa, bali ina viongozi ambao wanafanana, wana akili hazikomai.

Nchi ambayo ni zaidi ya miaka 50 tangu ipate uhuru kuiita changa ni matusi.

CCM imeshindwa kusimamia dira ya kuivusha nchi kwenda kwenye maendeleo.

Inacho fanya kwa sasa ni kutengeneza na kukomaza uasi miongoni mwa watanzania, na hasa kizazi cha wasomi.

Mbali ya kujitahidi kufubaza elimu, haitachukua mwongo mmoja kabla ya maasi ya umma kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…