Dkt. Mashinji: Huwezi ukawatofautisha Serikali, Mahakama na Bunge. Hata Mbinguni kuna Baba, Mwana na roho lakini maamuzi ni yaleyale

Mbona tuliambiwa tunataka kufanyiwa Tanzania iwe kama ulaya? Au ulaya hamuitaki tena. Au mnadhani ulaya ni maghorofa tu.
Tanzania ni nchi changa bado tukiwa wakubwa tutakua kama Amerika
Kwa sasa watuache tujijenge taratibu tutafika tuu

Wasitulazimishe kufanya vitu wanavyofanya wakubwa vikatutesa
 
Anasubiria uteuzi
 
Akili za huyu brother ni za zamani sana. Kabla hata ya wazee wetu kutaka kujikomboa toka utumwani. Kashashiba sasa hivi ndio anacheua huo uvundo.
 

Ni "manywele" huyu huyu asiyekuwa kingunge CDM?

Huyu kama katawi alikuwa afisa kipenyo. Atakuwa amerudi nyumbani kweli kweli.
 
Tofauti ya msomi na ambaye hajasoma nchi hii ni ndogo sana. Wamepishana tu muda wakukaa darasani ila kwenye mind set, weledi, ufanisi, utendaji, matumizi ya elimu, taaluma, muda na maarifa hatuna tofauti.

Yaani weka yote unayoyajua duniani ila jua hatuna tofauti kati ya walioshinda shuleni na wale walioshinda nyumbani na tatizo letu kubwa la kwanza ni Kutokujiamini.
Hao ndo wasomi wetu wabobevu - bora umufuate Slaa utupunguzie jam
 
Mbona tuliambiwa tunataka kufanyiwa tanzania iwe kama ulaya?.Au ulaya hamuitaki tena.Au mnadhani ulaya ni maghorofa tu.
Ndio hatua zimeanza hata ulaya ilikua kama sisi zamani

Rome wasn't built in a day - wahenga wa ulaya
 
Huyu nae ni bora akae kimya tu. Katika watu waliofeli mapema ni huyu blaza.

Sijui udokta wake ni wa nini huyu jamaa?

Anaibuka sasa kipindi cha uteuzi anawaza anaweza bahatisha hata mkaguzi wa waganga wa kienyeji wilaya.
Alikuwa general Secretary wa chama kikuu Cha upinzani chadema. Aliteuliwa na Mbowe baadae akawaona saccos makanjanja akasepa.
Leo eti kafeli, mlikuwa na gs ambaye kafeli? Hapa iliyofeli ni chadema na Mbowe.
 
Mbona anachoongea hakuna uhalisia na mifano yake ni ya kiwango cha chini sana sana, pia mahojiano ni ya kiwango cha uswazi siyo cha dokta.
Malalamiko ya Zambia yanahusu wachina kujazana kwenye biashara ndogondogo kama walivyo hapa. Zambia na Malawi zilipata uhuru baada ya Tanzania na zimekuwa zikijitahidi kwenye chaguzi zake za vyama vingi. Kiwango cha Mashinji kwenye siasa ni kidogo sana kwani hata huko Chadema na kufanya lolote la maana na ndivyo alivyo CCM.
 
Alikuwa general Secretary wa chama kikuu Cha upinzani chadema. Aliteuliwa na Mbowe baadae akawaona saccos makanjanja akasepa.
Leo eti kafeli, mlikuwa na gs ambaye kafeli? Hapa iliyofeli ni chadema na Mbowe.
Alifeli kwa sababu wakati wa uhai wake akiwa chadema chama kilidorora sana. Yeye kama katibu mkuu hakuna na jipya kukipa uhai chama chake.
 
Charles Bowkosk alisema - "The problem with world is that intelligent people are full of doughts while the stupid one's are full of confidence"

Mwanzo sikumwelwqwa lkn siku zinavyosonga mbele nagundua shida waliyonayo wasomi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…