Dkt. Mfisi: Bangi inatumika zaidi Tanzania

Dkt. Mfisi: Bangi inatumika zaidi Tanzania

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema dawa ya kulevya inayoongoza kwa kutumiwa zaidi hapa Nchini ni bangi ikifuatiwa Heroin.

Amesema sehemu ya Heroin inayoingizwa Nchini Tanzania husafirishwa na kupelekwa kwenye masoko mengine Duniani ikiwemo China na Marekani.

Dkt. Mfisi anasema "Bangi inastawi mikoa mingi hapa Nchini hata katika udongo wa ajabuajabu, sijui kwanini lakini nafikiri ndiyo maana imekuwa ikipatikana maeneo mengi."

Source: EATV
 
Hivi, mbona watu wa mataifa mengine wanapiga huu moshi na hawana shida? Huenda madhara yake si makubwa kama inavyosemwa na wataalamu au mamlaka za serikali. Hata Waadzabe wanakula bangi kama maji lakini hatusikii wakibakana wala kukatana mapanga. Ninadhani uhalifu ni tabia zaidi na ukichaa ni matatizo mengine ya kimazingira ama jenetiki zaidi , bangi inasingiziwa tu.
 
Ila nilivokuaga dogo mtu akisema Bangi nikawa nachukulia kitu cha ajabu hafu watumiaji nawaona kama waharifu kinoma..
 
Nilivuta bangi for at least six years now nashukuru nimeishaicha..na pombe leo Niko siku ya pili napumzika.hope I willl quit be..pray for me guys kuacha mazoea mabovu inawezekana..jali afya yako kuwana msimamo...[emoji123][emoji123]
 
Mimi mwenyewe natumia..

Navyoiback up na facts huku kwenye jamii Wakuu wangu naona wameanza kunishtukia.

Juzi Mmoja akanambia nkamchukulie kitu .. kwanza alifanya ssssss ile kama anabana moshi KWA jula hivi Nkacheka akasema kamanda Kanifanyie mchongo ..

Bila hiyana nikatia timu KWA mjubawise .. Kufika akanambia haujaja na inzi nkamwambia Hapana Nipo Msafi usiwaze .. akanivuta Fasi ya dwasi ... Akasororoa mgozi.

Kufika KWA mkaliwade(Mkuu ) Tom(phantom) likanyongwa pembeni Ceres , Fruit salad Ni mwendo wa Nipasie nkupasie ... We ended up making superb plans za Biashara na mikakati mingine .. alichonambia Till next time Mkali ..

Bangi na iheshimiwe
 
Kuna mbegu mpya za Bangi zimefanyiwa modification hiyo mbegu ni dawa, na hizingui na haina THC

THC ndio huwa imazingua na kuleta Uchizi
 
Ni wakati sasa umefika kuishusha Daraja au kuihalalisha na ilipiwe Tozo au Kodi stahiki.
Ninaweza kuwa tofauti kimtazamo na wewe mkuu, kwa upande wangu
1. Kuna watu imeharibu maisha yao, mtu akishavuta bangi anasinzia kwenye couch, hata haendi kufanya mitikasi mingine ya kimaisha.
2. Wengine wenye vichwa panzi wamewehuka kabisa.
3. Pia kisaikolojia ina uraibu mkali sana, kuna wale wameteseka miaka na miaka wameshindwa kuacha baada ya kuwa wavutaji wa kila siku.
Bora waihalalishe kama zao la kibiashara kwenda nchi za nje, lakini siyo kutumika kama kiburudisho.
 
0c2ffa3bcd899b9bc7c172cbf49d9066.jpg
 
Kwenye Bangi kemikali inayoleta Uchizi ni THC ni kuagiza mbegu ambayi imefanyiwa Modification na kutolewa hiyo THC.
 
Kwenye Bangi kemikali inayoleta Uchizi ni THC ni kuagiza mbegu ambayi imefanyiwa Modification na kutolewa hiyo THC.
Mbona huku Tunavuta asili na tupo fresh Tuu ila ni KWA kiwango.

Fid q " Tunamoka Ili kusafiri kihisia"

Sumu
 
Back
Top Bottom