johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Naibu waziri wa Afya Dr Mollel amesema Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote itaanza kutumikia mwezi huu wa April 2024 katika tarehe itakayopangwa
=====
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote itatangazwa kuanza kutumika kabla ya Mwisho wa Mwezi wa Nne Mwaka 2024 kwa tarehe itakayotajwa.
Dkt. Mollel amebainisha hayo leo kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15 na kikao cha kikao cha pili wakati akijibu swali Namba 27 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maakum Mhe. Furaha Ntengo Matondo aliyeuliza Je, lini Bima ya Afya kwa Watu Wote itaanza kutumika.
Dkt. Mollel amesema Serikali imeanza maandalizi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambapo kwa Mujibu wa Kifungu cha 1 cha Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Waziri anaweza kuteua Baadhi ya Vifungu vya kuanza kutumika.
“Baadhi ya Vifungu ambavyo vinaweka Mifumo imara ya kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote vimeshaainishwa na kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sheria itatangazwa kuanza kutumika kabla ya Mwisho wa Mwezi wa Nne Mwaka 2024 kwa tarehe itakayotajwa”, ameeleza Dkt. Mollel.
Dkt. Mollel amesema kuwa serikali imeshaainisha vyanzo vitakavyo hudumia watu wasio kuwa wa uwezo wakiwemo wajane na watoto wa mitaani.
Source: Clouds TV