GE2025 Dkt. Mollel: Wenzetu wanaompinga Rais Samia nafikiri wana changamoto ya Afya ya Akili

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ametoa kauli yenye uzito dhidi ya baadhi ya wanachama wenziye wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaojitokeza hadharani kumpinga Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Dkt. Mollel amesema kuwa baadhi ya wana CCM wanaoonekana kuhoji au kupinga uongozi wa Rais Samia huenda wanakabiliwa na changamoto ya afya ya akili.

"Wapo watu ambao wanapokuwa sio main character, wanajichanganya na kufikiri kuwa huo sio ukweli. Hilo ni tatizo la akili kama ilivyo matatizo mengine ya akili."

Your browser is not able to display this video.
 
Daktari Mollel ameteleza big time, mtu anayekupinga kwa hoja unatakiwa kumjibu kwa hoja yenye mshindo zaidi hadi afike kileleni na ikiwezekana apite kilele badala ya kuleta ujanja ujanja kwenye mambo serious kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Nimesikitika sana,sasa yeye mbona ndio anaonekana mgonjwa wa akili
 
Daktari Mollel ameteleza big time, mtu anayekupinga kwa hoja unatakiwa kumjibu kwa hoja yenye mshindo zaidi hadi afike kileleni na ikiwezekana apite kilele badala ya kuleta ujanja ujanja kwenye mambo serious kwa maslahi mapana ya taifa.
Ngoja akae kitaa mindset ya kichawa imuoshe kwanza
 

Kwani daktari wa meno naye ni mbobezi wa kanuni na Sheria?
 
Yeye ndiye mwenye changamoto ya Afya ya Akili. Mwanaume mzima anakubali vipi kununuliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…