Dkt. Mpango aendeleza marufuku ya lumbesa. Je, Viongozi wanakwama wapi kumaliza hili tatizo?

Dkt. Mpango aendeleza marufuku ya lumbesa. Je, Viongozi wanakwama wapi kumaliza hili tatizo?

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amepiga marufuku ununuzi wa mazao ya wakulima kwa kutumia vipimo visivyokuwa rasmi ikiwemo ujazo ulizidi yaani lumbesa

Alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizindua Maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini hapo.

Dk. Mpango alisema, kuanzia sasa mazao yote yanatakiwa kuuzwa kwa kupimwa kwenye mizani huku akiwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kusimamia matumizi ya vipimo hivyo.

Alisema hata mifugo inatakiwa kuuzwa kwa kutumia mizani na kuagiza ielekezwe kwenye minada yote ya mazao ili itumike kupima mazao ya wakulima.

“Kuanzia sasa lumbesa nchini ‘no’ (hapana), kwa hiyo mazao yote yatanunuliwa kwa kutumia mizani, nawaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya msimamie hili, hatutaki kusikia mahali popote biashara hii ikiendelea,” alisema Dk. Mpango.

Alisema faini za lumbesa hazitatakiwa kuwa chanzo cha kuendelea kutumika kwa vipimo hivyo visivyostahili kwenye ununuzi wa mazao ya wakulima.

Pia soma: PM Majaliwa apiga marufuku kufunga rumbesa
 
Alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizindua Maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini hapo.

Dk. Mpango alisema, kuanzia sasa mazao yote yanatakiwa kuuzwa kwa kupimwa kwenye mizani huku akiwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kusimamia matumizi ya vipimo hivyo.
Kila mwaka awe anatumbuliwa kiongozi aliyeshindwa kutimiza wajibu
 
Maonesho ya 88 Yanafanyika kitaifa jijini hapo ( WAP)dar,mwanza,arush au!?
 
Back
Top Bottom