Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.
Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.
Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.
Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.
Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.