Dkt. Mpango: Vijana achaneni na kupenda mashangazi

Dkt. Mpango: Vijana achaneni na kupenda mashangazi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu mmesikia huko alichokisema Dkt. Mpango kuhusu Mashangazi?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philiph Mpango, amesema zinahitajika tafiti za kina pamoja na mikakati katika kufanya mapinduzi ya kitamaduni kubadili tabia na mazoea yasiyofaa yanayojitokeza katika Jamii hivi sasa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo.

Dkt Mpango amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kusherehekea miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) uliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo ametaja baadhi ya mazoea na tabia hizo ni pamoja na kutojali muda, kutokuwa na uaminifu mahali pa kazi pamoja na kutumia njia zisizofaa katika kupata kipato.

Makamu wa Rais ameitaka ESRF pamoja na Watalaam wa Fikra Tunduizi (Think Tank) kuangazia pia tabia za hivi karibuni za Vijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanawake waliyowazidi umri (Mashangazi) kama njia rahisi ya kujikimu, kutumia muda mwingi bila kufanya kazi kwa kushinda Vijiweni, uchezaji kamari, utupaji taka ovyo, uchomaji moto ovyo wa nyasi na misitu pamoja na ubinafsi.

Pia Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuangazia tabia nyingine kama vile matumizi makubwa ya fedha katika anasa kuliko kuweka akiba ikiwemo uchangiaji zaidi katika matukio ya sherehe na tafrija kuliko kusaidia gharama za elimu na matibabu kwa familia za kipato cha chini.
Soma: Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania
 
Back
Top Bottom