Dkt. Msola atolewa na uwanjani polisi kumnusuru dhidi ya Yanga

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakati mashabiki wa Yanga wakichukizwa na matokeo ya sare ya mabao 3-3 hasira zao zilielelekezwa kwa Mwenyekiti wa klabu Dk Mshindo Msolla.

Tukio hilo lilijiri dakika chache mara baada ya firimbi ya mwisho ya mchezo wakati bosi wao huyo akielekea katika gari yake.

Wakati Msolla akitoka makundi ya mashabiki wakionekana kumzunguka kiongozi wao huyo huku wakimshambulia na maneno makali ya lawama.

Hata hivyo Msola alikuwa salama kutokana na kuzungukwa na idadi kubwa ya askari wa jeshi la polisi waliokuwa na silaha wakimsindikiza kiongozi huyo wa juu wa klabu hiyo.

Mashabiki hao walionekana kumlaumu kiongozi wao huyo wakimtaka pia kuachia ngazi kutokana na matokeo hayo ambayo Yanga ilipata sare ya tatu mfululizo.

Hata hivyo Msola alibahatika kutoka salama uwanjani huku dakika moja kabla ya kuondoka alitanguliwa na basi la timu hiyo lililoondoka kwa kasi uwanjani hapo kwa msafara wa pikipiki moja ya polisi.
 
Hilo n garasa la mwisho huwa najiuliza hata kuongea tu shida sjui alimzid nn Dr Jonas tibolowa
 
Sijui nani alimchagua yule jamaa...huwa nikimwangalia tu naona hayupo sawa
 
Wakati mashabiki wa Yanga wakichukizwa na matokeo ya sare ya mabao 3-3 hasira zao zilielelekezwa kwa Mwenyekiti wa klabu Dk Mshindo Msolla...
Ila mashabiki no wana fiki sana aliye wasajikia wachezaji wana mjua ila wana muogopa kumgusa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ lwan msola ndio walikuwa wana enda kumpokea airport na wachezaji ?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mashabiki utopolo waache ubabaishaji mnaletewa striker supong mmampokea kwa mbwembwe wakaona haitoshi mkaletewa festo maneno mengi work done is equal to zero
 
Msolla amemfukuza mollinga na kumsajili sarpong.

Lazima atupe majibu kwa nini alimfukuza david molinga
 
Msola na Mwakalebela ni mizigo hapo utopolo,wapo kuzengea hela ya Gharib tu,na hawa manyani wasipowaondoa watausikia Ubingwa masikioni tu.
 
Mashabiki wa Yanga tambueni Msola yy hajawasajiliaa wachezaji na kocha, aliye wasajikia wachezaj na kocha mnamjua lkn mna muogopa kumgusa. Sasa sisi ambao tuliwaona kipimdi kile mna kwenda airport kupokea wageni wenu leo tuta wa kumbusha huyo muhusika wa kumlaumu
Si mnakumbuka kuna mtu mlimbeba juju ktk kiti pale airport sasa huyo ndio mka deal nae maana yy ndio alikuwa ana wasajikia wachezaj πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Anasakwa aliye mleta zawadi mauya jangwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…