OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wakati mashabiki wa Yanga wakichukizwa na matokeo ya sare ya mabao 3-3 hasira zao zilielelekezwa kwa Mwenyekiti wa klabu Dk Mshindo Msolla.
Tukio hilo lilijiri dakika chache mara baada ya firimbi ya mwisho ya mchezo wakati bosi wao huyo akielekea katika gari yake.
Wakati Msolla akitoka makundi ya mashabiki wakionekana kumzunguka kiongozi wao huyo huku wakimshambulia na maneno makali ya lawama.
Hata hivyo Msola alikuwa salama kutokana na kuzungukwa na idadi kubwa ya askari wa jeshi la polisi waliokuwa na silaha wakimsindikiza kiongozi huyo wa juu wa klabu hiyo.
Mashabiki hao walionekana kumlaumu kiongozi wao huyo wakimtaka pia kuachia ngazi kutokana na matokeo hayo ambayo Yanga ilipata sare ya tatu mfululizo.
Hata hivyo Msola alibahatika kutoka salama uwanjani huku dakika moja kabla ya kuondoka alitanguliwa na basi la timu hiyo lililoondoka kwa kasi uwanjani hapo kwa msafara wa pikipiki moja ya polisi.