Dah! Ila Yanga kuna utani sana. Kuanzia kwa kocha mwenyewe, wachezaji, mpaka kwa viongozi. Yaani dirisha la usajili walitambua fika striking force ni mbovu! Wakamsajili Saido Ntibazonkiza, haonekani uwanjani! 😇
Wakamleta Fiston! Nae anaonekana kukosa kabisa match fitness!! Sijui alikuwa hana timu kabla ya kuja Jangwani!! Kiasi anaonekana kupuyanga tu uwanjani kama Mbwana Samatta kule Fernabace! Yaani anapitwa mbali na Striker Mburundi mwenzake Didier na anayechezea Mbeya City!
Kazi kweli kweli! Ditram Nchimbi naye ni mchezaji nyota wa timu ndogo! Na siyo timu kubwa! Wakati alipokuwa Mwadui na Polisi Tanzania, amecheza kwa kiwngo cha juu sana kuliko alipokuwa Azam na sasa Young Africans!! Jana alikosa goli la wazi kabisa!! Dah! Inauma sana. Maana timu isipo badilika, Ubingwa utarudi tena Msimbazi.