Dkt Mvungi: Muungano Ulishavunjika!


Hapa muafaka labda kuwe na Mahakama ya Katiba itakayoshughulikia migongano kati ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977!
 

Wenye matatizo ni wazanzibar ambao wanataka 'sovereinity, hivyo kuanzisha chokochoko, pia Zanzibar ndiyo inafaidika sana kiuchumi, maana wao cha kwao ni chao na cha kwetu bara ni cha wote. Ningekuwa rais ningevunja huo muungano kabisa maana wanatujazia nafasi zetu za kazi, wanatumia hela zetu halafu wanaleta jeuri, nasisi tunawabembeleza
 

Hii mada inajirudia sana katika hali tofauti,namimi nimekuwa na maswali ambayo wanzanvibar hawataki kuyajibu. Lakini nianze na kujibau hoja nyepesi zenye wino mwekundu. Yale ya kisheria nawaachia akina Mvungi maana wao ni wataalamu.
1. Ni kweli znz ina ardhi na mipaka, kwahiyo unachosema hapa ni kuwa Wazanzibar wanaosihi bara wakitumia ardhi ya bara kama watanganyika bila bughudha wanavunja sheria kwa sababu wao ni raia kama wale wa kenya, uganda na burundi. Hapa ndipo tunasema ondokeni muende katika nchi yenu yenye ardhi na mipaka, na mkija tanaganyika mje kama wageni.
2. Hakuna anayetakataa waznz kuwa na nchi yao, je wanaitambua katiba ya muungano? kama jibu ni ndio, je uhalali wa nchi yao kwa mujibu wa katiba ya muungano unatoka wapi.
3. Kama hutambui katiba ya muungano unawezje sema unataka muungano. Kwanini waznz wasiwe na kura ya maoni kuhusu muungano kama wanautaka au la. Wabara hawahitaji maana hawana cha kupoteza na kama kipo nifahamishe tafadhali.
4. Waznz wamedai wimbo wa taifa,wanao. Wakadai bendera yao, wanayo. Wakadai nembo yao, wanayo. Sasa kitu gani wanadi tena ambacho hawajapewa?

Kumbuka kuwa znz ina bunge na serikali yake, inasikitisha kuona kuwa waznz wanashirki kumchagua rais wa tanganyika. Wana wabunge amabo wanalipwa kwa fedha za Tanganyika, ni wabunge hao hao wanatoa maamuzi yanayowahusu watanatanganyika na si waznz. Nani hapa anayepata hasara?
Kama suala ni serikali tatu, nani atagharamia serika ya muungano tukizingatia kuwa uchumi na bajeti ya znz ni ndogo kuliko uchumi wa soko la kariakoo kwa mwaka.

Mwisho, wanznz wadai kura ya maoni ya kujitenga na muungano, wakitaka kuondoka katika muungano ruksaa, lakini kila haki ina wajibu. Wajibu wa kwanza ni wao kuondoka bara na kama wakija waje kama wakenya au warundi. Wasiruhusiwe kumiliki ardhi maana wao ni rai wa kigeni na kama ikiwa ni lazima basi wawe wanahudumiwa kama waingereza au wamarekani.
Njia rahisi si wanznz kulalama, waondoke Tanganyika warudi wakaijenge nchi yao. Kama Watafuatwa huko ndio walalamike. Waondoke kutoka katika ajira za bara kama walivyojazana wizara ya fedha, afya n.k maana wana wizara zao na hakuna sababu ya msingi ya kuwazibia nafasi watanganyika maana wao si sehemu ya muungano.
Waje kusoma katika vyuo kwa gharama za nchi yao na si za walipa kodi wa Tanganyika,maana wanvyuo vyao na wao si sehemu ya muungano.
Lakini kama wapo wanznz wanafanya kazi bara,biashara na wanamiliki ardhi, wanasoma kwa kodi za wabara, basi wakae kimya maana ipo siku watachafua hali ya hewa zaidi na wasije shangaa wakitimuliwa kama wezi.
Short, waznz ondokeni mkadai nchi yenu mkiwa kwenu kwanza.
 
Naunga mkono hoja-ni bora huu muungano ufe-kila m2 akae nchini mwake ajenge nchi yake kwa resources zao-na si kuibiana kama tunavofanya sasa-kama ikitokea nchi moja ikataka muungano na nyingine-itabidi tuweke terms mpya za muungano zinazoendana na hali ya sasa.
 
Ni kweli hata ukisoma Katiba yetu:

1.​
Tanzania is one State and is a sovereign United Republic.

2.​
- (1) The territory of the United Republic consists of the
whole of the area of Mainland Tanzania and the whole of the area

of Tanzania Zanzibar, and includes the territorial waters.

Sasa hivi Zanzibar ni nchi na yenye mipaka yake. Pia ni "state" (dola) inayojitegemea.
Kwanini CCM wako kimya, au wanataka mjadala wa Bunge uanze na hili?
 
Wazanzibari hawahitaji muungano. ndio maana kila kitu nationalism. Wimbo wa taifa, bedera ya taifa, majeshi ya zmz, mafuta, gesi,mipaka mpaka sovereignity. What remains is just a declaration out of the Union. Chovya chovya humaliza buyu la asali. Wataula Muungano mpaka udondoke.
 

Ukiangalia vizuri namna katiba yetu ilivyofumwa utaona kwamba kuna mamlaka tatu za kiserikali japo kuna serikali mbili. Serikali ya Zanzibar ina mamlaka kwa upande wa Zanzibar. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina mamlaka mbili. Kwanza ina mamlaka ya muungano katika masuala yote ya Muungano kwa minajili ya katiba. Pili, ina mamlaka yote ya serikali ya iliyokuwa Tanganyika katika masuala yote yasiyo ya Muungano. Kwa mfano, japo elimu ya msingi sio suala la Muungano, ipo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni hivyo hivyo katika masuala kama utamaduni, kilimo, mifugo, serikali za mitaa, afya na jamii. Utaona kwamba Bunge linalojadili masuala ya elimu ya msingi, afya na kadhalika ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania japo mambo hayo ki msingi ni ya Tanzania Bara. Masuala ya afya na maji kwa upande wa Zanzibar yanajadiliwa na Baraza la Wawakilishi. Pia nafasi nyingine kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu zinazua utatata kama ni ofisi za Muungano au za Tanganyika ndani ya Serikali ya Muungano.
 
Hapa muafaka labda kuwe na Mahakama ya Katiba itakayoshughulikia migongano kati ya Katiba ya Zanzibar, 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977!

Ki msingi mahakama hiyo inatamkwa katika Katiba japokuwa haijawahi kuundwa. Na Mahakama hii ian nguvu zote kwa mujibu wa katiba ya jamhuri kushughulikia mgogogo unaohusu pande mbili za muungano. Huu ulikuwa ni wakati muufaka wa mahakama hiyo kukaa japo kutokana na mchakato wa mabadiliko ya katiba uliyoanza kuelea kwa sasa haina maana tena. Tutarajie suluhisho lake katika katiba mpya. Ni bora hili likanukuliwa kama moja ya mapungufu makubwa katika mfumo wetu wa katiba ambayo yanapaswa kutizamwa kwa macho ya upevu.
 
Sina hakika kama waliokua wakiruhusu mambo hayo kufanyika walimaanisha kuwanyamazisha wazanzibar. Hata ivyo tulipofikia sasa ni matokeo ya kutofanya yaliyo sahihi juu ya muungano wetu kwa kipindi chote kilichopika.. Nina imani sisi kwa pamoja WATANZANIA(sipendi kutumia watanganyika na wazanzibar kwa sababu natamani maneno haya yafe) tunaupenda na tunauhitaji sana muungano wetu na hatuko tayari kuupoteza..wanaofanya mzaha juu ya jambo hili ndio wanaosababisha tuone kama tunatofautiana ikiwa ukweli ni sivyo.. Muungano unajadilika,unazungumzika, unatengenezeka upya kisheria unakuwa imara zaidi.. Tujadili tusiogope na TUAMINIANE...
 
Waziri wa afya Dr. Hussein Mwinyi unamuweka wapi? kwa kuwa anaongoza wizara ya afya ambayo si ya muungano ni mtanganyika?
 
Waziri wa afya Dr. Hussein Mwinyi unamuweka wapi? kwa kuwa anaongoza wizara ya afya ambayo si ya muungano ni mtanganyika?


Tukienda hivyo orodha haitaisha. Mtu atauliza Wizara ya Elimu si ya Muungano, Wizara ya Afya si ya Mungano, Wizara ya Kilimo si ya Muungano lakini Bunge linalojadili bajeti yake ni Bunge la Muungano. Sheria zinazotumika Tanzania bara peke yake zinatungwa na Bunge la Muungano wakati sheria za Zanzibar Bunge la Muungano halihusiki. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni Waziri Mkuu ambaye sio ofisi ya Muungano wakati serikali Bungeni anayoiwakilisha ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hizo ni baadhi ya changamoto katika muungano wetu amabazo tunapaswa kuzitafakari na kuzitafutia masuluhisho kwa mujibu wa wakati tulionao. Sio wakati wa kulaumu wabara wanawakandamiza wazanzibar au kinyume. Yawezekana kuna baadhi ya masuala yalikuwa mhimu wakati muungano ukiasisiwa na kwa sasa mambo yamebadilika. Yawezekana pia kwamba yakawa bado mhimu. Ni mhimu wananchi tukajadili kwa kwenda mbele badala ya kujadili kwa kurudi nyuma.Inapobidi kurudi nyumba iwe ni kwa ajili ya kujenga hoja na kutafakari kwa kuzingatia usemi kwamba "Kuelewa leo ni kuelewa jana na kuelewa na kuelewa leo ni kuelewa tunakoelekea"
 
Ni kweli Muungano upo kimaneno zaidi kuliko uhalisi wenyewe wa muungano,
 
Pumzika kwa Amani Dr. Edmund Sengondo Mvungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…