nani kasema zanzibar si nchi? hebu tafuteni vizuri hizo kumbukumbu zenu ili mujue kuwa ni nchi au siyo. Hivi kama huyo Sengodo Mvungi anayewatia ujinga watanzania kwa kusema Zanzibar si nchi anajua vizuri Historia ya Zanzibar na Tanganyika na jinsi huo muungano ulivoanzishwa au anpiga kelele tu kwa vile kazizowea? Aliulizwa dola inatakiwa iwe na nini akasema mambo manne; 1:watu, 2:Uongozi wenye maamuzi, 3:Ardhi yenye mipaka, 4:kutambulika kimataifa. Swali linakuja hapa, je Zanzibar haina vitu vyote hivo? Kuna watu, viongozi, ardhi ambayo mipaka yake si ya kuwekwa na mtu(mzungu) bali ni mipaka iliyowekwa na mungu (bahari)na hilo la mwisho kama hajui historia ya zanzibar arudi asome tena, Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa, kabla hata ya Tanganyika kufikiria suala hilo. Sasa kama wanzanzibari wanadai nchi yao kisha wanaambiwa si nchi kwa misingi ambayo haipo kabisa, ni jambo la kushangaza sana. Sisemi kama muungano usiwepo, la ila wapeni wazanzibari kile wanachokidai bila kupiga makelele. Naamini watu wenye akili na wasomi kama hao kina Sengodo Mvungi wakikaa pamoja na kujadili na kukubaliana juu ya matakwa ya wazanzibari bac hayo ni mambo madogo na rahisi sana kutekelezeka, kama vile ilivokuwa rahic kwa baba yenu wa taifa kuunda muungano........!!!!
Hii mada inajirudia sana katika hali tofauti,namimi nimekuwa na maswali ambayo wanzanvibar hawataki kuyajibu. Lakini nianze na kujibau hoja nyepesi zenye wino mwekundu. Yale ya kisheria nawaachia akina Mvungi maana wao ni wataalamu.
1. Ni kweli znz ina ardhi na mipaka, kwahiyo unachosema hapa ni kuwa Wazanzibar wanaosihi bara wakitumia ardhi ya bara kama watanganyika bila bughudha wanavunja sheria kwa sababu wao ni raia kama wale wa kenya, uganda na burundi. Hapa ndipo tunasema ondokeni muende katika nchi yenu yenye ardhi na mipaka, na mkija tanaganyika mje kama wageni.
2. Hakuna anayetakataa waznz kuwa na nchi yao, je wanaitambua katiba ya muungano? kama jibu ni ndio, je uhalali wa nchi yao kwa mujibu wa katiba ya muungano unatoka wapi.
3. Kama hutambui katiba ya muungano unawezje sema unataka muungano. Kwanini waznz wasiwe na kura ya maoni kuhusu muungano kama wanautaka au la. Wabara hawahitaji maana hawana cha kupoteza na kama kipo nifahamishe tafadhali.
4. Waznz wamedai wimbo wa taifa,wanao. Wakadai bendera yao, wanayo. Wakadai nembo yao, wanayo. Sasa kitu gani wanadi tena ambacho hawajapewa?
Kumbuka kuwa znz ina bunge na serikali yake, inasikitisha kuona kuwa waznz wanashirki kumchagua rais wa tanganyika. Wana wabunge amabo wanalipwa kwa fedha za Tanganyika, ni wabunge hao hao wanatoa maamuzi yanayowahusu watanatanganyika na si waznz. Nani hapa anayepata hasara?
Kama suala ni serikali tatu, nani atagharamia serika ya muungano tukizingatia kuwa uchumi na bajeti ya znz ni ndogo kuliko uchumi wa soko la kariakoo kwa mwaka.
Mwisho, wanznz wadai kura ya maoni ya kujitenga na muungano, wakitaka kuondoka katika muungano ruksaa, lakini kila haki ina wajibu. Wajibu wa kwanza ni wao kuondoka bara na kama wakija waje kama wakenya au warundi. Wasiruhusiwe kumiliki ardhi maana wao ni rai wa kigeni na kama ikiwa ni lazima basi wawe wanahudumiwa kama waingereza au wamarekani.
Njia rahisi si wanznz kulalama, waondoke Tanganyika warudi wakaijenge nchi yao. Kama Watafuatwa huko ndio walalamike. Waondoke kutoka katika ajira za bara kama walivyojazana wizara ya fedha, afya n.k maana wana wizara zao na hakuna sababu ya msingi ya kuwazibia nafasi watanganyika maana wao si sehemu ya muungano.
Waje kusoma katika vyuo kwa gharama za nchi yao na si za walipa kodi wa Tanganyika,maana wanvyuo vyao na wao si sehemu ya muungano.
Lakini kama wapo wanznz wanafanya kazi bara,biashara na wanamiliki ardhi, wanasoma kwa kodi za wabara, basi wakae kimya maana ipo siku watachafua hali ya hewa zaidi na wasije shangaa wakitimuliwa kama wezi.
Short, waznz ondokeni mkadai nchi yenu mkiwa kwenu kwanza.