Dkt Mwigulu: Kuna viashiria vya uhalifu, watoto kutekwa, watu kupigwa risasi

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kusimama imara kuzuia vitendo vya uhalifu vikiwemo vya wa watoto kutekwa na kuuwawa, mtu mmoja mmoja kupigwa risasi kwenye makazi yake, hadi sasa kuna viashiria vya uhalifu huo.

Ameyasema hayop alipokuwa akiwasilisha makadio ya mapato na matumizi ya kwa mwaka 2025/26 bungeni jijini Dodoma, akiwataka wananchi waviachie vyombo hivyo vifanye kazi yake.

“Hata sasa vimejitokeza viashiria vya uhalifu kama huo ambavyo havipiganwi kwa kupeleka vikosi na kampeni au kusema tunapigana vipi? Tukiendelea kunyoosheana vidole na kunyooshea vidole vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tutaacha adui aendelee na uhalifu.

“Vita vya aina hii vinapiganwa kwaintelijensia, hivyo niwasihi watanzania wenzangu tuviache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake na tuendelee kufanya kazi kwa maendeleo ya Taifa letu,” amesema.
 
View attachment 3365871

Kumbe wanajua, nini kinawafanya wawe wakali yakiongelewa haya?
 
Ni vita vinapiganwa kiitelejensia,mmeelewa waropokaji?
 
Eti viashiria.

Yaani watu wanapotea kisha kupatikana wamekufa wewe unasema viashiria?

Aende huo ujinga awaambie familia ya mzee Kibao halafu aone kama atarudi Singida.
 
Back
Top Bottom