Dkt. Mwigulu: Mpina afute kauli yake kwa kulipotosha Bunge

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kufuta kile alichotanabaisha kuwa kauli ya uongo kuhusu DP World kuanza kukusanya kodi katika Bandari ya Dar es Salaam na kwamba kauli hiyo imelenga kulipotosha Bunge na Watanzania.

Baada ya Waziri Mwigulu kuomba kuhusu utaratibu Mbunge Mpina amekubali kuyafuta maneno hayo kwani lengo lake ilikuwa ni kumaanisha tozo ambazo zinakusanywa na siyo kodi.
Your browser is not able to display this video.
 
uongo ni tabia mbaya na ya fedhaha sana kama ilivyo kwa ombaomba wa kitaifa na kimataifa 🐒
 
Kwa nini Huwa anapenda Ligi za kijinga mda wote hiyo mpina wenu?

View: https://www.instagram.com/reel/DCEb7fLqjPv/?igsh=azJ4cnFmN2tocDVm
 
KI uhalisia kodi na tozo si ni kitu kile kile ndugu zangu.. yaani ni kama Rushwa na Takrima.
 
Kwa akili yangu mbovu kodi na tozo ni kitu kile kile ila siyo malipo. Wajuzi waje wanielimishe
 
Mwamba karejea kuchangamsha bunge.
Hatimae "kumechangamka"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…