Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

=========

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo

Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

View attachment 1826377
Kwani leo ni April1?
 
Hawa wamesomea elimu ya kodi au waziri analeta mzaha katika kazi.
Nawasubiri kuwapiga maswali ya kodi na sheria zake. Ila kwa kweli mizaha imezidi sana siku hizi, yaani masuala mazito ambayo ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi watu wanaleta watu wa ajabu ambao hata maana ya kodi au uchumi hawajui, mambo ya kodi na uchumi ni tofauti na kumtangaza Faru John au Mlima Kilimanjaro au kumjadili Karia na TFF yake.
 
Hivi kweli Hamisa akakueleze kuhusu elimu ya Mlipa kodi? Kweli?

Kwani elimu ya mlipa kodi inahitaji mvuto wa ngozi na makalio ili mtu aweze kuelewa vema?

Si kuja vijana wengi tu wamesoma Chuo cha Kodi, wapewe hilo chapuo.

Wakawaeleweshe watu mtaani na kuwajibu kwa ufasaha. Pengine makali ya kukosa ajira yangepunguzwa kidogo.

Upuuzi!.
Anarudia makosa ya Kingwangwala, anadhani anatangaza mbuga za wanyama
 
Kuhamasisha mtu mpaka "kupenda" kulipa kodi...,,[emoji848]
EGFlOByU8AANHGo.jpg

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mikataba yao iwekwe wazi watakua wanapokea shilingi ngapi kwa mwezi, na per diem zao zitakua ngapi iwapo watazunguka vitongoji vyote nchini.

pia tuambiwe nchi ngapi wametumia mbinu hizo na wakafanikiwa.
 
Mwigulu bwana, sasa kati ya hao nani anajua maswala ya kodi au uchumi?????? Kama hawajui watatoaje elimu gani, mpria, utangazaji, comedy au ulimbwende????
Nadhubuti kusema ni yale yale ya Kigwang`ala, wasanii na utalii kumbe tulipigwa hadi basi.
Leo asubuhi nilimwona akisoma nyaraka na kulieleza bunge mipango ya maendeleo
Hafanani kabisa na uchumi
Tulimwambia Rais kwa mwigulu kaingia chaka
 
Vipi maslahi yao? Watalipwa kiasi gani hao?
 
Nyie mnaopinga hapo juu mnajielewa? Wewe uliyesoma upo mbwinde huko na mbwana samatta au edo kumwembe nani ana fan base kubwa na anaweza kusikilizwa akihamasisha kodi?
Binafsi wangemchagua Mh Jumanne Kishimba au King Musukuma watu wangeelewa zaidi
 
Kumuudhi mlipa kodi tu.

Hii dhana sijui wameiokota wapi yaani kitu kidogo tu awareness campaigns through billboards, radio and print ads !!

PM itabidi ateue akina chumvi kuwa balozi wa kuwatunza wabunge adabu wakatwe kodi na payee ili wapewe kiinua tumbo halali...
 
PhD ya Mwigulu ndio matokeo yake haya? Hadi Hamisa Mabeto, ndio PhD zetu zinatoa maamuzi kama haya😳😡 Aiseee
 
Hivi TRA wanavyopeleka matangazo redioni na hizo mentions zao kusomwa na watangazaji hao watangazaji wanakuwa ni IFM's graduates wanaokuwa na elimu ya Kodi?

Hawa wanaweza kutumia platform zao kupost short briefs za maofisa wa kitengo cha elimu kwa mlipa kodi kinachoongozwa na Kayombo pale TRA na pia watapewa semina na nini cha kusema.
Kuongoza watu/nchi ni kazi sana mkuu
Wengine utasema common sense hazipo
Yani wanajaji vitu vingine hata havipo
Mbona hesabu ndogo tu kujua kwanini hawa wameteuliwa
Kama kiongozi una roho ndogo ukawii kuwa dikteta utajiona kama urais vile umekushinda kumbe hamna

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Uzuri siku hizi dunia ni darasa tosha. Hili tumeiga kutoka nchi gani miongoni mwa nchi zilizoendelea??
Nchi nyingi tu hutumia influencer kufikisha baadhi ya Mambo, waweza kuwa na shule lakini hamna anayekujua na sikuhizi ma socialite ndo Wana followers wengi, mfano christiano Ronaldo alivo weza affect kampuni ya coca-cola, so tusiye tuna ignore hawa ma celeb hasa kwa vichwa au vijana wa zama hzi
 
why mnawataj
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

=========

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo

Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

View attachment 1826377
a hao watatu tuu... kwani hao ni katika wengi au ndio timu imekamilika
 
Hapo kumwembe na samatta wameongezewa tu ila kuua so hizi mambo tunazijua sana mwenye kazi hapo ni mobeto
Ni ajabu na nikweli mtu anamshauli mwenzake aoge maji yenye baridi Kali na ni kipindi Cha baridi huku yeye kavaa koti la manyoya kujikinga na baridi
Sina Imani Kama ushauri wake utapokelewa vuzuri
 
Nchi nyingi tu hutumia influencer kufikisha baadhi ya Mambo, waweza kuwa na shule lakini hamna anayekujua na sikuhizi ma socialite ndo Wana followers wengi, mfano christiano Ronaldo alivo weza affect kampuni ya coca-cola, so tusiye tuna ignore hawa ma celeb hasa kwa vichwa au vijana wa zama hzi
Kaka hapa tunazungumzia serikali wewe unaleta mambo ya cocakola!!! Em kuwa serious isee. Hivi wajua kuwa mambo ya Taxation particularly tax compliance ni mambo complex hayahitajii midemko???
 
Back
Top Bottom