Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
๐๐ธ๐. ๐ ๐๐ถ๐ด๐๐น๐ ๐ก๐ฐ๐ต๐ฒ๐บ๐ฏ๐ฎ: ๐๐ถ๐ผ๐ป๐ด๐ผ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐๐ถ, ๐๐ฎ๐๐ถ ๐ป๐ฎ ๐ ๐๐ฎ๐น๐ฒ๐ป๐ฑ๐ผ ๐ฎ๐๐ถ๐๐ฒ๐ฐ๐ต๐ผ๐ธ๐ฎ
Mussa Saidi-Dar es Salaam
Katika kipindi cha siku chache tu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba ameendelea kudhihirisha mfano wa uongozi wa vitendo, uchapakazi na kujituma kwa kiwango cha juu katika kuwahudumia Watanzania. Ratiba yake ya kuanzia Mei 8 hadi Mei 13, 2026 imeonyesha wazi namna alivyojitoa kuhakikisha anatimiza wajibu wake wa kitaifa bila kuchoka, bila kusita na kwa uzalendo mkubwa.
Mei 8, 2026 Waziri Mkuu alikuwa mkoani Morogoro ambapo alifanya ziara ya kikazi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi. Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha Serikali inawafikia wananchi moja kwa moja na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yenye tija kwa taifa.
Kesho yake, Mei 9, Waziri Mkuu aliendelea na ziara yake mkoani Dodoma katika maeneo ya Kibakwe na Mpwapwa ambako alikagua miradi ya maendeleo pamojanna kuzungumza na wananchi na viongozi.
Licha ya ratiba nzito ya mchana kutwa, jioni ya siku hiyo alisafiri kuelekea Dar es Salaam na usiku huo huo akashiriki hafla ya utoaji wa tuzo za wanamichezo, zilizoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jambo lililoonyesha namna anavyothamini sekta ya michezo na mchango wake katika kuunganisha taifa na kukuza vipaji vya vijana.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Mei 10, 2026 Waziri Mkuu aliondoka kuelekea Nairobi nchini Kenya kushiriki Mkutano wa Africa Forward uliowakutanisha viongozi wa Afrika na Ufaransa kujadili masuala ya maendeleo, uwekezaji, biashara na ushirikiano wa kimkakati kwa ajili ya mustakabali wa bara la Afrika.
Katika mkutano huo wa Mei 11 na 12, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliupeleka ujumbe wa Tanzania kimataifa, huku Waziri Mkuu aliendelea kuitangaza nchi kimataifa na kutafuta fursa zenye manufaa kwa Watanzania.
Kilichowavutia wengi zaidi ni namna baada ya kurejea nchini Mei 13, 2026, Waziri Mkuu hakupumzika wala kuchelewa, bali aliingia moja kwa moja bungeni kuendelea na majukumu ya kitaifa. Huu ni ushahidi wa wazi wa kiongozi anayeelewa uzito wa dhamana aliyopewa na anayejitoa kwa moyo wote kuhakikisha gurudumu la maendeleo linasonga mbele kila wakati.
Hakika, mwenendo huu wa Dkt. Mwigulu Nchemba ni somo kwa viongozi wengi kuhusu maana halisi ya uongozi wa kuwajibika. Katika nyakati ambazo wananchi wanahitaji matokeo, kasi na uthubutu, Waziri Mkuu ameendelea kuonyesha kuwa maendeleo ya taifa yanahitaji viongozi wanaofanya kazi kwa bidii, wenye uthubutu wa kusafiri, kusikiliza wananchi, kuiwakilisha nchi kimataifa na kurejea kazini bila kuchoka. Uchapa kazi wake ni alama ya uzalendo na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa.

Attachments
-
IMG-20260508-WA0032.jpg447.5 KB · Views: 13 -
IMG-20260509-WA0093.jpg404.3 KB · Views: 15 -
IMG-20260510-WA0049.jpg295.3 KB · Views: 9 -
IMG-20260511-WA0034.jpg281.4 KB · Views: 11 -
IMG-20260512-WA0006.jpg76.3 KB · Views: 12 -
IMG-20260512-WA0044.jpg491.7 KB · Views: 15 -
IMG-20260512-WA0058.jpg376.5 KB · Views: 15 -
IMG-20260512-WA0055.jpg324.8 KB · Views: 11 -
IMG-20260512-WA0053.jpg427.7 KB · Views: 9 -
IMG-20260513-WA0067.jpg348.2 KB · Views: 14 -
IMG-20260513-WA0063.jpg316.2 KB · Views: 13 -
IMG-20260513-WA0123.jpg1.1 MB · Views: 12 -
IMG-20260513-WA0131.jpg1 MB · Views: 9 -
IMG-20260513-WA0126.jpg913.7 KB · Views: 13