Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Juni 27, 2026 akizungumza na wananchi wa Ikungi, Mkoani Singida amesema kuwa Serikali haina ugomvi na chama chochote cha siasa, bali inaweka mbele kipaumbele cha usalama kwa Watanzania na Taifa kwanza.
Pia soma > Waziri Katambi apiga marufuku mikutano ya siasa kwa vyama vyote
Waziri Mkuu Mwigulu amesema...
Jambo ambalo hatuna mzaha nalo, ni kuhusu ulinzi wa nchi yetu, ulinzi wa Watanzania, na ulinzi wa rasilimali za Tanzania. Haya si mambo ya mzaha, wala hayana upande wala hayana pande mbili. Haya ni mambo ya aina moja tu yanayohusu yanaihusua Tanzania na Watanzania wake. Kwenye hili hatuna makundi. Jambo la usalama wa nchi yetu hili halina halina pande.
Tanzania ina vyama vya siasa, lakini hivi vyama vya siasa vipo tu kwa sababu kuna Tanzania. Hata dini zetu, tunaweza kufanya hizo ibada kama kuna amani, pakichafuka, waulizeni walioko kwenye machafuko kama wanakumbukaga ibada.
Kwa hiyo panapokuwepo na viashiria vya kukosekana kwa usalama wa nchi, hicho ndicho kipaumbele, lazima tushughulikie kwanza jambo hilo. Lazima tushughulikie kwanza jambo hilo. Sisi kama serikali wala hatuna ugomvi na vyama vya siasa, hata mimi mwenyewe nina chama changu, hatuna ugomvi.
Hatuna ugomvi na chama chochote cha siasa, hatuna ugomvi, na vyama vya siasa viko kikatiba, wala watu wasije wakachanganya haya mambo, hatuna ugomvi na vyama vya siasa. Lakini tuna jambo ambalo tuna wajibu nalo la kuhakikisha nchi yetu iko salama na Watanzania wako salama na hilo ni jambo la kipaumbele.
Hilo ni jambo la kipaumbele, hatupuzi hatupuzi hata chembechembe yoyote inapokuja jambo la usalama wa nchi yetu na usalama wa wananchi wake."