Dkt. Mwigulu: Tutabana Matumizi kwenye chai, vitafunwa, safari ndani na nje ya nchi na semina. Viongozi watumie usafiri wa pamoja ziarani!

Dkt. Mwigulu: Tutabana Matumizi kwenye chai, vitafunwa, safari ndani na nje ya nchi na semina. Viongozi watumie usafiri wa pamoja ziarani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake.

Source: TBC
 
Baada ya kuona boss kapandishwa kimbinyiko akili ndo inakaa sawa siyo? Malkia kajaza ukuta dhahabu lakin kawapandisha kimbinyiko nyie maskini kila mtu na viete yake
Unajua watu wanasema huyu jamaa ni kichwa,hivyo kwenye hili kaweza kusoma alama za nyakati Kwa haraka na kuibukiamo kwenye kupanda kimbinyiko couch Kwa safari ya pamoja yenye lengo Moja🤔
 
Tanesco Dodoma na NSSF dom hapo kwa siku wanatumia chai ya laki 4 kwa asubuhi moja kila mmoja wao. Jamani nyie nyie nilikuwa napeleka hiyo chai na vitafunwa nabaki kinywa wazi. Huku nilipo shule ya sekondari chai ya elfu 10 waalimu wanaipigania ngumi
Acha uongo wewe, nssf wanunue chai kwako, nimefanya field nssf mwanza chai wanajinunulia
 
Somo wameshapewa Tena na matajili wenye kila kitu.

Hizo V8 kwanza ziuzwe zote watumie Land cruiser GX zinawatosha na wengine watumie Toyota Rav 4J.

B30BF26A-40A9-4592-86FF-266B6E2EFDDC.jpeg
C3AB178A-D10F-4141-B1DB-53E448FF0794.jpeg
 
Kubana matumzi pia wabunge wakatwe kodi na kupunguza posho ya vikao kwenye bunge vikao vinavyochukua m,uda mrefu mfano bunge la bajeti ni karibu miezi minne badala ya kulipwa 300k walipwe 150k tu na mafuta wasiwekewe maana wanaishi pale pale.
 
Lini chai na vitafunwa vilikuwepo kwa watumishi, labda nyie mnaotumia viieite....jibaneni wenyewe huko, wengine hiyo chai na vitafunwa hatujawahi kuviona na hizo safari za ndani na nje mnazo nyie wapanda viieite.
We ni mwalimu labda,ofisi zote za umma chaii ipo
 
Tanesco Dodoma na NSSF dom hapo kwa siku wanatumia chai ya laki 4 kwa asubuhi moja kila mmoja wao. Jamani nyie nyie nilikuwa napeleka hiyo chai na vitafunwa nabaki kinywa wazi. Huku nilipo shule ya sekondari chai ya elfu 10 waalimu wanaipigania ngumi
Acha uongo weweeee. Hiv unaelewa chai mtu atoke akaitafutie wap? Sabasaba au nyerere Square arud aende tena. Chai gan ya lak nne wanayotumia eeeh?
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake

Source: TBC
Kilichowakuta London kinarasimishwa kuwapunguzia machungu waliopigwa tukio 😁
 
Haya mataga mliokuwa mnatetea Tozo inabidi tena mbadili gia angani muanze kupongeza kwa haya mabadiliko madogo ya tozo.
Tumewaambia toka siku nyingi, CCM ni janga la taifa. Hayo mataga toka lini yakawa na akili? Si ajabu waliokuwa wanatutukana wakitetea tozo kujenga vituo eti vya afya nao ukawaona humu wakitoa pongezi.

Huwezi ukapanda mchicha ukavuna nyanya. Ukishamuopoa kiongozi ndani ya huo uozo unaoitwa CCM na kumsukumizia madaraka yanayomzidi kimo unategemea nini? Lazima binadamu avune alichopanda, hakuna namna.
 
Back
Top Bottom