Dkt. Mwigulu: Tutabana Matumizi kwenye chai, vitafunwa, safari ndani na nje ya nchi na semina. Viongozi watumie usafiri wa pamoja ziarani!

Dkt. Mwigulu: Tutabana Matumizi kwenye chai, vitafunwa, safari ndani na nje ya nchi na semina. Viongozi watumie usafiri wa pamoja ziarani!

Tanesco Dodoma na NSSF dom hapo kwa siku wanatumia chai ya laki 4 kwa asubuhi moja kila mmoja wao. Jamani nyie nyie nilikuwa napeleka hiyo chai na vitafunwa nabaki kinywa wazi. Huku nilipo shule ya sekondari chai ya elfu 10 waalimu wanaipigania ngumi
Achaa watu wapige pesa,ili pesa ije kwenye mzunguko!!!
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake

Source: TBC
Hivi kuna viongozi huko serikalini .....!! Hao viongozi ni kuanzia ngazi gani ...!!?

Halafu hili la chai ..... duh. Yaani serikali inalipa watu mishahara halafu bado inawanunulia chai na vitumbua .... Hii Tanzania kweli bado ipo zile enzi za Ujamaa na Kujitegemea.
 
Kama serikali ikibana matumizi kwa kumaanisha maisha yatapungua makali kwa kiasi kikubwa kwetu sisi wananchi wa kawaida, wafute baadhi ya vyeo visivyokua na maana
 
Nataka wabunge wasiwe na vitambi, ndipo nitaamini serkali inabana matumizi
 
kubana matumzi pia wabunge wakatwe kodi na kupunguza posho ya vikao kwenye bunge vikao vinavyochukua m,uda mrefu mfano bunge la bajeti ni karibu miezi minne badala ya kulipwa 300k walipwe 150k tu na mafuta wasiwekewe maana wanaishi pale pale
Ndiyo maana hawa wabunge siku wakiukosa au muda wao kwisha basi huchanganyikiwa. Katika kipindi cha ubunge huwa wanaishi maisha ambayo siyo ya uhaisia.
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake

Source: TBC
Tulishazoea kusikia ngonjera tamu lkn inapokuja kwenye utekelezaji mambo hubaki yale yale ya siku zote.
 
Somo wameshapewa Tena na matajili wenye kila kitu.

Hizo V8 kwanza ziuzwe zote watumie Land cruiser GX zinawatosha na wengine watumie Toyota Rav 4J.View attachment 2362435View attachment 2362436
Afadhali umeweka hii picha inaonyesha wazungu na waafrika kwenye basi maana maneno yamekuwa mengi kuhusu maraisi waafrika kupandishwa basi kumbe ni wageni karibia wote ndiyo wamepangiwa hivyo. Nimeona kwenye BBC news hata Waziri Mkuu wa Canada naye alikuwa kwenye basi
 
Hao madereva wenu walivyo hamnazo soon tutapeperusha bendera nusu mlingoti.
 
Enzi za chama kimoja swali langu lisingekuwa na maana sana ila tuko mfumo wa vyama vingi.

Sijaelewa baada ya Waziri Dr Mwigullu kutoa tamko la marekebisho ya Tozo ndio imeisha au Bunge litajadili na kuazimia?!

God bless us!
Kwa taarifa yako hizi tozo ni yeye Mwigulu alizipanga kwa kutumia kanuni alizojitungia, hivyo bunge hapa halihusiki.

Bunge lilihusika kutunga sheria ya kuruhusu kuwepo kwa tozo lakini likampa uwezo wa kutunga kanuni na kuweka viwango vya tozo.
 
Afadhali umeweka hii picha inaonyesha wazungu na waafrika kwenye basi maana maneno yamekuwa mengi kuhusu maraisi waafrika kupandishwa basi kumbe ni wageni karibia wote ndiyo wamepangiwa hivyo. Nimeona kwenye BBC news hata Waziri Mkuu wa Canada naye alikuwa kwenye basi
Ni watu wawili tu waliowekewa protokali tofauti

1. Waziri Mkuu wa Taifa Takatifu la Mungu Israel

2. Rais wa Dunia mh Biden
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake

Source: TBC
Anamsema Boss wake
 
Hajafanya kitu. Alitakiwa afute tozo zote. Hii hel tuliyoweka benki mbona tumeshailipia kodi!!!!! Hamna kitu hapa.
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake

Source: TBC
TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.

=====

1). Rais Samia afanya ziara yake ya kwanza nchini Uganda mnamo 11 Aprili 2021 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda.

2). Rais Samia afanya Ziara ya Siku Mbili Nchini Kenya, kuanzia 04 Mei 2021

3). Rais Samia tarehe 16 Julai, 2021 afanya ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.

4). Rais Samia tarehe 02 Agosti, 2021 afanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

5). Rais Samia tarehe 16 Agosti, 2021 aelekea nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.

6). Rais Samia Tarehe 24 Agosti, 2021 aelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kwa Rais Mteule wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.

7). Rais Samia tarehe 18 Septemba, 2021 aondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

8). Rais Samia tarehe 30 Oktoba, 2021 aelekea Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

9). Rais Samia tarehe 10 Novemba, 2021 aelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

10). Rais Samia tarehe Januari 28, 2022, atembelea Msumbiji. Akiwa Pemba-Msumbiji, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu ameeleza kuwa lengo ya ziara hiyo ni kudumisha Diplomasia kati ya nchi hizo mbili.

11). Rais Samia afanya ziara ya Kikazi Nchini Ufaransa na Ubelgiji kuanzia tarehe 09-19 Februari 2022.

12). Rais Samia Februari 24, 2022 aelekea Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki maonyesho ya Expo 2020

13). Rais Samia Aprili 13, 2022 aenda Marekani kwa ziara ya kikazi. Pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ itakayozinduliwa Aprili 18, 2022 jijini New York. Alikaa siku 8

14). Rais Samia 10 May 2022 afanya ziara ya Kiserikali nchini Uganda kwa siku mbili

15). Rais Samia 23 Mei 2022 ameondoka Nchini Kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya Ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Humo

16). Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Muscat nchini Oman kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya Siku tatu tarehe 12 Juni, 2022

17). Leo tarehe 06 Julai, 2022 Rais Samia aelekea Dakar Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)"

18). Rais Samia 16 Agost 2022, aondoka Nchini kwenda DR Congo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

19. Septemba 17, Rais Samia
alifika Uingereza ili kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika September 19. Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II
 
Wenzenu huku wanaendesha kwa nidhamu ya hali ya juu
Mtakanyagwa na Tipper huko mufwee

Eti wapande usafiri wa pamoja daa
Mwigulu utauwaaaa
 
Back
Top Bottom