Dkt. Mwigulu: Tutabana Matumizi kwenye chai, vitafunwa, safari ndani na nje ya nchi na semina. Viongozi watumie usafiri wa pamoja ziarani!

Hata uso wake haukushabihiana na matamshi yake, hata ainisho la ubanaji bajeti amefanya mzaha hajaweka bayana maeneo muhimu yanayobeba pesa nyingi mfano ununuzi wa magari, na etc., He hasn't been that serious. Too much reading ndio usomi gani huo?
Ni kama mwanafunzi alikuwa anajisahihishia mtihani wake mwenyewe
 
TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.

=====

1). Rais Samia afanya ziara yake ya kwanza nchini Uganda mnamo 11 Aprili 2021 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda.

2). Rais Samia afanya Ziara ya Siku Mbili Nchini Kenya, kuanzia 04 Mei 2021

3). Rais Samia tarehe 16 Julai, 2021 afanya ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.

4). Rais Samia tarehe 02 Agosti, 2021 afanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

5). Rais Samia tarehe 16 Agosti, 2021 aelekea nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.

6). Rais Samia Tarehe 24 Agosti, 2021 aelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kwa Rais Mteule wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.

7). Rais Samia tarehe 18 Septemba, 2021 aondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

8). Rais Samia tarehe 30 Oktoba, 2021 aelekea Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

9). Rais Samia tarehe 10 Novemba, 2021 aelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

10). Rais Samia tarehe Januari 28, 2022, atembelea Msumbiji. Akiwa Pemba-Msumbiji, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu ameeleza kuwa lengo ya ziara hiyo ni kudumisha Diplomasia kati ya nchi hizo mbili.

11). Rais Samia afanya ziara ya Kikazi Nchini Ufaransa na Ubelgiji kuanzia tarehe 09-19 Februari 2022.

12). Rais Samia Februari 24, 2022 aelekea Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki maonyesho ya Expo 2020

13). Rais Samia Aprili 13, 2022 aenda Marekani kwa ziara ya kikazi. Pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ itakayozinduliwa Aprili 18, 2022 jijini New York. Alikaa siku 8

14). Rais Samia 10 May 2022 afanya ziara ya Kiserikali nchini Uganda kwa siku mbili

15). Rais Samia 23 Mei 2022 ameondoka Nchini Kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya Ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Humo

16). Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Muscat nchini Oman kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya Siku tatu tarehe 12 Juni, 2022

17). Leo tarehe 06 Julai, 2022 Rais Samia aelekea Dakar Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)"

18). Rais Samia 16 Agost 2022, aondoka Nchini kwenda DR Congo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

19. Septemba 17, Rais Samia
alifika Uingereza ili kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika September 19. Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II
Nimebaini watu wenye akili za kawaida mnanionea gere kila ninaposafiri kwenda nje, lakini mtaipata fresh siku moikamatwa maana nimemwagiza Mwanangu IGP Wambura kuwa mtu yoyote anaye niparura mtaani na mitandaoni mkamateni na mumpe kesi ya Panyaroad.
Bado ningali nikiwatizama kwa jicho langu legevu,endeleeni!
 
Kinachoniuma mbona wabunge wao hawakatwi pesa zao?
Nao wakatwe kila wanachopata kama wengine kama kweli ni wazalendo wa nchi yao!
Waache tabia za "mafarisayo' za kuwatwisha watu wengine mizigO ambayo wao hawaigusi hata kwa ncha ya vidole vyao!
 
Mwambieni arudi chapu bongo Ili kupunguza MATUMIZI huko alipo
 
Acha uongo wewe, nssf wanunue chai kwako, nimefanya field nssf mwanza chai wanajinunulia
Mmmh we ndio nina walakini na ww, mm nilifanya field nssf shinyanga, chai ilikuwa ni juu ya ofisi. Hakuna aliekuwa ananunua kwa pesa yake
 
Safi sana ila kutumia usafiri wa pamoja hapo ikiwa ni ajali tutapoteza viongozi kwa pamoja.
Vipi Uingereza,imepoteza viongozi wangapi,jana WALE uliowaona unataarifa ya hata mmoja wao kupotea?
 
Kwani huko majumbani kwenu hampiki chai mpaka mje kutegemea za maofisini??
 
Hivi kuna viongozi huko serikalini .....!! Hao viongozi ni kuanzia ngazi gani ...!!?

Halafu hili la chai ..... duh. Yaani serikali inalipa watu mishahara halafu bado inawanunulia chai na vitumbua .... Hii Tanzania kweli bado ipo zile enzi za Ujamaa na Kujitegemea.
Aisee tena mpaka uone inaongelewa hivi ni chai heavy weight si mchezo mchezo
 
Na mabasi yake tupande bure kwa muda wa mwezi mmoja kufidia tozo tulizo minywa kipindi chote hicho ....

Jokes
 
Tanesco Dodoma na NSSF dom hapo kwa siku wanatumia chai ya laki 4 kwa asubuhi moja kila mmoja wao. Jamani nyie nyie nilikuwa napeleka hiyo chai na vitafunwa nabaki kinywa wazi. Huku nilipo shule ya sekondari chai ya elfu 10 waalimu wanaipigania ngumi.
Mtaani tunakula chai ya maziwa maharage na chapati mbili inatosha kabisa halafu hatupatipati yale maradhi yasiyo ya kuambukiza !! Kweli Mungu ni fundi sana. !!
 
Waziri wa Fedha Dr Mwigullu ameagiza maafisa maduhuli kuanza kubana Matumizi kwenye Chai Vitafunwa Safari ndani na nje ya nchi na Semina.

Kadhalika viongozi wanapokuwa kwenye safari yenye lengo moja basi watumie usafiri wa pamoja badala ya kila mmoja kwenda na gari yake.

Source: TBC
Mbo kuhusu v8 hazungumzii..na mishahara ya wabunge anakwepa kwepa tu..wakati huko ndio kwenye matumizi makubwa sana ya hela ya walipa kodi.

#MaendeleoHayanaChama
 
TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.

=====

1). Rais Samia afanya ziara yake ya kwanza nchini Uganda mnamo 11 Aprili 2021 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda.

2). Rais Samia afanya Ziara ya Siku Mbili Nchini Kenya, kuanzia 04 Mei 2021

3). Rais Samia tarehe 16 Julai, 2021 afanya ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.

4). Rais Samia tarehe 02 Agosti, 2021 afanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

5). Rais Samia tarehe 16 Agosti, 2021 aelekea nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.

6). Rais Samia Tarehe 24 Agosti, 2021 aelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kwa Rais Mteule wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.

7). Rais Samia tarehe 18 Septemba, 2021 aondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

8). Rais Samia tarehe 30 Oktoba, 2021 aelekea Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

9). Rais Samia tarehe 10 Novemba, 2021 aelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

10). Rais Samia tarehe Januari 28, 2022, atembelea Msumbiji. Akiwa Pemba-Msumbiji, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu ameeleza kuwa lengo ya ziara hiyo ni kudumisha Diplomasia kati ya nchi hizo mbili.

11). Rais Samia afanya ziara ya Kikazi Nchini Ufaransa na Ubelgiji kuanzia tarehe 09-19 Februari 2022.

12). Rais Samia Februari 24, 2022 aelekea Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki maonyesho ya Expo 2020

13). Rais Samia Aprili 13, 2022 aenda Marekani kwa ziara ya kikazi. Pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ itakayozinduliwa Aprili 18, 2022 jijini New York. Alikaa siku 8

14). Rais Samia 10 May 2022 afanya ziara ya Kiserikali nchini Uganda kwa siku mbili

15). Rais Samia 23 Mei 2022 ameondoka Nchini Kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya Ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Humo

16). Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Muscat nchini Oman kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya Siku tatu tarehe 12 Juni, 2022

17). Leo tarehe 06 Julai, 2022 Rais Samia aelekea Dakar Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)"

18). Rais Samia 16 Agost 2022, aondoka Nchini kwenda DR Congo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

19. Septemba 17, Rais Samia
alifika Uingereza ili kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika September 19. Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II
Mkuu naomba hizi taarifa za safari zitengenezee uzi wake na uwe unapata updates kila akisafiri nje ya nchi ili kuweka kumbukumbu vizuri.

Ili wanachi waone tofauti kati ya raisi na mlamba asali

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom