PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo Bandari Jumuishi ya Mangapwani itakuwa imekamilika kwa lengo la kuinua uchumi wa Zanzibar na kufungua fursa pana za biashara, ajira na uwekezaji.
Akizungumza katika moja ya mikutano yake ya kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Bumbwini Mkoa Kaskazin Unguja, Dkt. Mwinyi amesema bandari hiyo itakuwa na sehemu maalum ya kuhifadhi mafuta, jambo litakaloondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa mafuta nchini na kuimarisha huduma muhimu kwa wananchi.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kwa umakini mkubwa kuhakikisha miradi hiyo ya kimkakati inaleta tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika hotuba yake, Dkt. Mwinyi ameahidi kwamba wananchi wote watakaoathiriwa na ujenzi wa bandari hiyo na barabara zinazohusiana, watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria.
Amebainisha kuwa tayari Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 11 kwa ajili ya malipo hayo, ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayepata hasara kutokana na maendeleo hayo makubwa.
Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Mwinyi amewataka wananchi kutojali maneno ya upinzani, badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba, siku rasmi ya uchaguzi.
Soma pia