Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33


Sijashangaa kumsikia Rais Mwinyi akitaka Rais Magufuli aongezewe muda.

Tayari Rais Mwinyi ana historia ya kuikiuka katiba waziwazi.

Ni Rais Mwinyi aliyemteua Agustino Mrema mwaka 1993 [kama sijakosea mwaka] kuwa naibu waziri mkuu.

Cheo ambacho hakipo kwenye katiba.

Hivyo Rais Mwinyi kutaka Rais Magufuli aongezewe muda, halafu akimaliza muda alioongezewa turudi tena kwenye utaratibu ulioainishwa na katiba, si jambo la kushangaza kivile.

Tayari Rais Mwinyi alishatuonyesha kuwa yeye si ‘constitutionalist’.

Kwake katiba haina maana kivile...
 
Angalia kati ya waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi nani anayelindwa zaidi, angalia msafara wa mkuu wa majeshi walinzi kila mahali, mpaka nyumbani ,alafu angalia waziri na ile gari moja. Nahisi hadi mishahara tafauti ni kubwa sana. Ndio maana kwa wenzetu huko wizara hii inaongozwa na wao wenyewe wanajeshi..
Sasa wizara kama hii huwezi tegemea waziri ataongeaongea tu. Wanamtafuta mtu mpole wanamweka , anakuwa kama symbol tu ya serikali kwamba ipo inalitazama jeshi kwa jicho la pembeni.
Lakini huyu Mwinyi upole umemzidi sana, angefaa sana angeendelea kwenye proffessional yake ya udaktari tena upande wa upasuaji ubongo ungemfaa sana, lakini huku kwenye siasa hapawezi ila historia ya baba imembeba sana.
 
Ila hujafanya comparison ya Mzee Mwinyi na mwanae? Inawezekana naye akawa kama ulivyosema?
 
Katika nchi zinazowajibisha wanasiasa, Hussein Mwinyi alitakiwa kujiuzulu siku nyingi tu, baada ya mabomu kulipuka kwenye ghala za silaha za jeshi.

Ni nchi kama Tanzania tu unaweza kuwa na tukio kama like halafu Waziri wa Ulinzi aka survive.
Je mwamunyange naye alipaswa kujiuzulu ama vipi
 
Punguza munkari mkuu huijui ccm wewe mbogamboga...

Kizazi hiki kinataka ushahidi!!!!!....Uchaguzi ukiwa huru na haki mwinyi hawezi kua rais wa zanzibar, hizo za mwinyi zimeibiwa tu ndio maana wazanzibari wote walitoka kwenye kikao wanalia.....
Zamani ccm ilikua na wenyewe lkn siku hizi ccm ina mwenyewe anayeamua kila kitu. Haya mambo ya ndani huwezi kuyajua ww endelea kulamba makalio tu utapata cheo
 
Ni kilaza mmoja kasoma MD Uturuki sidhani hata kama alimaliza ikute alinunua cheti. Hajawahi kusoma chuo bongo. Hajawahi kupractice u daktari.

Hata kama atakuwa na madhaifu yake kwenye siasa lakini Professionally hujamtendea haki.

Dr Hussein Mwinyi amesoma MD uturuki akamaliza na Uturuki wako mbele zaidi kuliko Bongo tuache kujitukuza. Kisha Dr Hussein Mwinyi amefanya Mmed Internal Medicine London na Internship amefanya pale MNH huwezi kumuita mtu huyu ni Kilaza.

By the way Mimi CCM hata isimamishe mgombea mzuri kiasi simchagui,ili nchi hii iendelee hili lichama chakavu lichama Dola lazima life. Hata Shetani ikisaidia kuliua hili lichama pouwa tu.
 
Je mwamunyange naye alipaswa kujiuzulu ama vipi
Nchi haipo kwenye vita mabomu ya jeshi kujilipua yenyewe, tena si mara moja useme bahati mbaya, mara mbili. Maana yake ilivyotokea mara ya kwanza hawakujifunza. Watu wanaotakiwa kuwa wanafanya kazi kwa umakini wote wa military intelligence!

Iitakiwa angalau mtu mmoja top upande wa siasa na mtu mmoja top upande wa majeshi wajiuzulu.

Na wengine waliowazunguka wabaki na wingu zito la scandal kwamba wameharibu kazi.

Baba yake Hussein Mwinyi, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alionesha mfano mzuri kwa kujiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani, kwa vile wazee waliuawa Shinyanga kwa tuhuma za uchawi na Polisi wakavuka mipaka katika kamatakamata yao. Akaona kwamba anawajibika kujiuzulu. Hussein kwa nini hakufuata mfano wa baba yake?

Barua ya kujiuzulu ya Mwinyi hii hapa

WANABIDII BLOG: [wanabidii] Barua ya kujiuzulu aliyoiandika Mwinyi kwenda kwa Nyerere

 
Hapa hasa ndio kiini cha Mada hii
Wazanzibari kama wanataka Mabadiliko na maendeleo ya Uhakika wamchague Maalim Seif
Kama wanataka Mapambio ya siasa yaliyozoeleka na kuendelea na Shida zao wamchague Mwinyi.

Vipa umbele vya Mwinyi ( Kayasema leo Kisiwandui Zanzibar alipo pokelewa Rasmi kama Mgombea wa CCM ).

  1. kuyalinda mapinduzi
  2. kuulinda muungano
  3. kuwashughulikia wala rushwa na wazembe.
  4. kuendeleza yote aliyoyaanzisha Dr. Shein
  5. Kuemdeleza uvuvi.
Vipa umbele vya Maalim Seif Sharif Hamad (bado havijawekwa hadharani)
  1. Kuwapa wazanzibari Mamlaka kamiliya Nchi yao ili wajipangie Maendeleo wayatakayo.
  2. Kuimarisha Muungano wenye kuleta haki pande zote mbili na kuheshimiana kama nchi washirika.
  3. Kutengeneza ajira kwa kuzinduauwekezaji wa Rasilimali za Bahari na za Uvuvi na kuwekeza kwenye Uvuvi wa viwanda.
  4. Safari ya Singapore ipo pale pale.
  5. Kuanza Kuchimba Mafuta na Gesi bila ya kumuogopa yeyote yule au kusubiri kibali cha Tanganyika.
  6. Kujenga Bandari Kubwa ya kisasa ili kuigeuza Zanzibar kuwa kituo kikuu cha biashara ukanda wa A,Mashariki.
  7. Utalii wa Kitajiri,sio huu wa Back pakers na Makanjanja na watakatishaji fedha wa Italy.
  8. Kuboresha Elimu kwa Kuanzisha Mfumo mpya wa elimu na unaokidhi haja ya Waznzibari yenye viwango vya kimataifa ikiwemo kuanzisha rasmi Baraza La Mitihani la Zanzibar ( Kwa level zote hadi vyuo)
Wazanzibar khiyari yenu kupanga ni kuchagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…