Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Nikiwa Kama Mwanachama wa CCM binafsi sikuwa namuunga mkono kabisa na sikuwahi kumuelewa, Binafsi Nilikuwa naona kabisa Mbarawa ndio anafaa kupeperusha bendera kwakuwa ameshapita hatuna budi kumuunga tu mkono!!!
 
Kuna kauli moja hapa JF mimi huwa inanishangaza sana, hii ya kusema una uwezo mdogo wa kupambanua mambo! Hivi mtu kawa mbunge kwa zaidi ya miaka 15, kawa waziri wa secta nyeti kabisa ya Ulinzi kwa miaka 11 kwa Marais wawili tofauti alafu eti unakuja hapa kusema ana uwezo mdogo wa kupambanua mambo? Tena inawezekana mtu mwenyewe unaye ongea hivo hapa enzi za shule huko hukuwahi kuwa hata kiongozi wa darasa achilia mbali ujumbe wa nyumba kumi au hata kwenye familia tu hupewi kuongoza kikao cha familia.
 
Kuna wadau wanasema hata kwenye CABINET alikuwa hawezi kuchangia mada

"'kama walivyosema wajumbe waliotangulia'"
 
Sisi wa Zanzibar kampeni yetu moja tu Zanzibar kwanza halafu twaingia na gia ya mashehe wetu walio waweka ndani huu ni mwaka wa 8
 
Huyu ndiye alishauri kua kidato cha sita kisiwe kigezo cha mtu kwenda Chuo?
Ila apa naona tumewakomoa wenzetu kwenye Muungano.. Rais wote wanatokea Bara...aisee
 
Kwa akili yako unafikiri rais wa bara siyo rais wa Zanzibar?
 
Dr Mwinyi amehudumi pale Kariuki hospital kwa muda mrefu tu acheni uzushi jamani!
Mkuu Kuna watu wana roho mbaya sana, eti mweupe kichwani! Hivi kati ya huyu mleta mada na huyo Mwinyi nani mweupe kichwani sasa? Mtu anapewa nafasi ya kuongoza wazara ya Ulinzi kwa miaka 11 kwa ufanisi mkubwa kabisa na watanzania tunajua tena kwa Marais wawili tofauti alafu mtu anakurupuka tu huko anakuja kumshambulia kwa chuki binafsi zake.
 
Katika nchi zinazowajibisha wanasiasa, Hussein Mwinyi alitakiwa kujiuzulu siku nyingi tu, baada ya mabomu kulipuka kwenye ghala za silaha za jeshi.

Ni nchi kama Tanzania tu unaweza kuwa na tukio kama like halafu Waziri wa Ulinzi aka survive.
 
Huyu jamaa watu wanategemea mengi sana kutoka kwake, ana kazi kubwa sana kutimiza shauku za wengi.

Lakini kubwa zaidi ni kuleta umoja kwa Wazanzibar.

Changamoto ya kwanza naona sio muongeaji mzuri. Amejipatia umaarufu sana kwa kuwa nafasi aliyokuwa nayo awali haikuwa ya kuzungumza na wananchi. Kwa kipindi kifupi naona hapa kuna shida, inabidi ajifunze kuongea kisiasa na kidiplomasia.

Ndipo nikakumbuka ule usemi kwamba hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima.
 
Kuna wadau wanasema hata kwenye CABINET alikuwa hawezi kuchangia mada

"'kama walivyosema wajumbe waliotangulia'"
Kauli hiyo si lazima iwe ya mtu ambaye hawezi kuchangia mada.

Inaweza kuwa.

1. Mtu anachangia mada kwa kuunga mkono, kwa kuanzia walivyosema waliomtangulia na kuchangia yake.

2. Ku build consensus.

3. Hata kupandikiza yake kijanja kwa kutumia muhuri wa "waliomtangulia".

4. Kuji align na authority.

5. Kufupisha maneno adirudie yaliyokwishasemwa ajazie zaidi tu.

Acceptance speech ya Mwinyi haikuwa mbaya. In fact kwa zama hizi za Magufuli ni kazi ngumu sana kutoa speech mbaya zaidi ya za Magufuli.

Mimi tatizo langu kwa Mwinyi ni utendaji zaidi.

Sijaona lolote alilolifanya. Amekuwa kama wallflower aliyekaa akisubiri promotion tu.

Na scandals kibao, ikiwamo ya milipuko ya mabomu, tena mara mbili (2009 Mbagala na 2014 Gongo la Mboto), si mara moja, zilitakiwa zimfanye ajiuzulu.
 
Kuna kauli moja hapa JF mimi huwa inanishangaza sana, hii ya kusema una uwezo mdogo wa kupambanua mambo! Hivi mtu kawa mbunge kwa zaidi ya miaka 15, kawa waziri wa secta nyeti kabisa ya Ulinzi kwa miaka 11 kwa Marais wawili tofauti alafu eti unakuja hapa kusema ana uwezo mdogo wa kupambanua mambo? Tena inawezekana mtu mwenyewe unaye ongea hivo hapa enzi za shule huko hukuwahi kuwa hata kiongozi wa darasa achilia mbali ujumbe wa nyumba kumi au hata kwenye familia tu hupewi kuongoza kikao cha familia.
Sasa unajisemea wewe au unamsemea yeye?
 
Mbona kajibu vizuri sana tena kitakwimu hasa hilo hakupigiwa kura na wazanzibar kajibu kitakwimu kwamba alipata zaidi ya nusu ya kura zote toka zanzibar na kuwaziba vidomo domo wazushi.
Ila sasa cha ajabu eti wanataka asinhejibu kitakwimu ili waendeleze propaganda zao!

Seif ajiandae kwa kipigo.
Chadema ni fungu la kukosa.
 
Kua mbunge miaka zaidi ya 10 , sijui waziri sijui nn.. hakumfanyi mtu awe na uwezo wa kupambanua mambo.

Kuna watu ukiwasikiliza tu unajua hamna kitu unazima na TV

Kuna mtu ukimsikikiza tu unajikuta umekesha kwa kumsikiliza.
 
Mbona kajibu vizuri sana tena kitakwimu hasa hilo hakupigiwa kura na wazanzibar kajibu kitakwimu kwamba alipata zaidi ya nusu ya kura zote toka zanzibar na kuwaziba vidomo domo wazushi.
Ila sasa cha ajabu eti wanataka asinhejibu kitakwimu ili waendeleze propaganda zao!

Seif ajiandae kwa kipigo.
Chadema ni fungu la kukosa.
Hujui madhara ya majibu yake! Kwani unafikiri waliozua kuwa wapiga kura wa Zanzibari walikuwa 35 unafikiri walikuwa hawajui?
 
Back
Top Bottom