Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Ni rais mtarajiwa wa wapi?????
Mboga mboga mna matatizo Sana ninyi!
Mchezo mliozoea kuucheza Zanzibar (Jecha Game) mwisho 2015!

This time tunawanyunyizia dawa ya kuua wadudu! Mbogamboga nyie!
Tehe tehe. Alitakiwa Vuai nini?
 
Hi
Katika nchi zinazowajibisha wanasiasa, Hussein Mwinyi alitakiwa kujiuzulu siku nyingi tu, baada ya mabomu kulipuka kwenye ghala za silaha za jeshi.

Ni nchi kama Tanzania tu unaweza kuwa na tukio kama like halafu Waziri wa Ulinzi aka survive.
Kama Waziri mwenye dhamana alishindwa hata kuitisha press conference juu ya tukio lile.
 
Tuishi tuu kwa fitna majungu na roho mbaya lakini ya Mungu ni mengine...
Ndio kesha kuwa sasa na Wazanzibar mkimchagua Hussein Mungu atazidi kuwaonyesha neema zilipo..
 
Kachukue form bwana tena kwa ticket ya CCM. Wewe hautaki u RC ?Acha ku overthink.Kachukue form walau Pombe apate CV yako. Maisha raha sana ukiacha kuoverthink.
Nishakwambia kamwe siwezi kufanywa kilaza hahahahaaaaa nishashindwa aisee!
 
Fatilia live channel ten, Tbc , clouds tv
=======
Mahojiano mafupi ya mgombe Urais Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi, Hussein Mwinyi na mtangazaji wa TBC, Shaaban Kisu.

Mtangazaji: Hili jambo ulikuwa nalo tangu zamani au limekuja hivi karibuni? Na nini kimekusuma kugombea?

Mwinyi: Kiuzoefu nimeona wakati umefika wa mimi kuhudumia wananchi kwa ngazi ya juu hususani wazanzibari wote kwa ujumla wao.

Mtangazi: Vipaumbele vyako ni vipi hasa?

Mwinyi: Serikali ya awamu ya saba wamefanya kazi nzuri na kuna mambo ambayo wameanza hawayajamaliza na yapo ambayo hayajakamilika, walipoishia mimi ndio ndio ntaanza. Vipaumbele viko vingi ntapata fursa ya kuvieleza baadae.

Mtangazaji: Umesema umejifunza kwa JPM utakuwa mkali, watu wameanza kuogopa hawakuzoea kuongozwa kwa ukali ukali, unalizungumzaje?

Mwinyi: Wasiwe na hofu kwa wale ambao hawana tabia hizo za rushwa, uzembe, ubadhirifu hawana sababu ya kuwa na hofu ila kwa wale ambao wana tatizo hilo kwa kweli wawe na hofu kwa sababu ndio hasa tutakapoweka mkazo wetu.

Mtangazaji: Tunapoingia kwenye uchaguzi hata mabeberu huingiza mikono yao na kama hatutakuwa makini hata amani itatetereka, wito wako ni upi kwa wazanzibari?

Mwinyi: Tumeishi kwenye kipindi cha miaka kumi kwa amani na ustahilivu jambo ambalo limetuwezesha kupata mafanikio ya kimaendeleo kwa hio tukiondoa amani hatutapata maendeleo. Wito wangu kwa wananchi wote tudumishe amani ili tuweze kupata maendeleo ya haraka.

Mtangazaji: Kauli uliyozungumza kwamba utakuwa mkali sasa kama Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwanini ulizungumza kauli ile?

Mwinyi: Unapotaka kutekeleza program zako za kiserikali lazima program zako za kiserikali ni lazima watu wote muende sambamba, wale ambao ni wazembe, wala rushwa watakurudisha nyuma ukiendelea kuwachekea ndio maana nikasema hivyo kwa sababu nataka tuwe na maendeleo ya haraka.


 
Back
Top Bottom