THOMASS SANKARA
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,055
- 4,695
Tujiandae saa tatu kamili kutazama mahojiano mahsusi Kati Dr. Hussein Mwinyi(Rais mtarajiwa wa Zanzibar) na Tido Muhando UTv(Channel 108 azam tv)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani hawa wazanzibar wanatokea mbinguni? Si wapo kwenye chama na Serikali. Sifa na ubora wao si unajulikana, sasa wanachama wote wakichagua mgombea wao kwa kuzingatia sifa zao kuna shida gani?Kwamba mwanaccm kutoka Bukoba anachagua mtu anaeenda kuongoza nchi ya Zanzibar!! shida ni kua unatetea ujinga lakini kibaya zaidi Mh Rais/m.kiti akasema itenguliwe ili wananchi wa Z bar ndo wafanye uchaguzi pekeyao napo utatetea na kusema sawa.
Mwinyi ni bonge la rais Zanzibar hawatajutiaKwani hawa wazanzibar wanatokea mbinguni? Si wapo kwenye chama na Serikali. Sifa na ubora wao si unajulikana, sasa wanachama wote wakichagua mgombea wao kwa kuzingatia sifa zao kuna shida gani?
Hiki chama kiliungana kikawa chama kimoja, lazima mambo yake yafanyike kwa pamoja. Otherwise labda Afro Shiraz irudi iwe inachagua wagombea wake. Lakini kwasasa utaratibu ndo huo.
Ukitaka kuziona nyeti za kuku basi subiria upepo.... Kwenye sauti ya mzee wetu pale kahama
Asianze tabia ya Trump ya kujisifia na kulalamika hata pasipokuwa na ulazima. Maneno hayo hayakutakiwa kutolewa na yeye.Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.
Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.
Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.
Source Swahili times
Maendeleo hayana vyama!
Kweli kabisa.Si vibaya majina ya wajumbe wa Zanzibar yakiwekwa hapa ili tujirodhishe na huo utetezi. Vinginevyo wanaosema ni wajumbe 35, au yeye anayesema 68, wote ni waongo.
Vijana wa lumumba mmeanza propaganda tena? Wajumbe wa Zanzibar walikua 35 na Bara 129, yeye alijipatia kura zote 129 kutoka bara. Iko hivyo, hata mtoto wangu mdogo hapa amekucheka sana. Unakwama wapi kwenye mahesabu ya kujumlisha na kutoa tu?Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.
Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.
Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.
Source Swahili times
Maendeleo hayana vyama!
Orodhesha hapa majina yao, usitufanye sisi watoto.Wajumbe wa Zanzibar ni 68.....sisi ndio CCM tunaokwambia!
Kayasemea wapi haya.. kishajichnaganya.Ameshafeli kama ameanza mapema kuingia kwenye huu mtego, CCM wanafanya makosa sana kuacha kura za visiwani zipigwe bara na wabara pia..
Kura za Urais Zenji zilipashwa zipigwe na wazenji tena wakiwa kisiwandui pale au bwawani hoteli, kura za wazenji kupigwa dom tena wapiga kura wengi wakiwa wabara ni dhahiri kunathibitisha wazenji hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe na kila kitu lazima kifanywe bara..
Wazanzibar simameni pamoja kuwaonyesha wabara nyie ni wazenji na Rais wenu lazima atoke zenji kwa kura za wazenji..
Rais wa Tanzania ni wa wote kwa maana ya Bara na Zenji hivyo kura lazima zipigwe na wote labda tulete serikali tatu, Zenji rais wao, bara rais wao na Tanganyika rais wake au zenji na bara ziwe na Mawaziri wakuu na Rais awe mmoja, au makamu wa Rais awe Rais wazenji na huku bara kuwe na waziri mkuu tu....
Uliyosema ni kweli kabisa nilimuona Nahodha tangu siku ya uchaguzi amenuna mpaka leo hajacheka kati ya wagombea wote huyu ameumia kweli. Lakini napenda kumfahamisha kwamba duniani hakuna haki akitaka haki basi ataikuta mbinguni akubali yaishe na maisha yaendelee.Dkt Mwinyi anapaswa kuwa makini mno kwa sasa kwa kauli zake, anapaswa kuwa na timu kabambe sana ya kampeni tena yenye kujumuisha watu waliokuwa kambi tofauti naye. Ili pale zitolewapo kauli za mitego kama hizo, wawe ndiyo wa kwanza kuzitolea majibu ya kuzikanusha.
Nyufa zipo kubwa sana kwa upande wa CCM Zanzibar, akumbuke matokeo yaliyompatia yeye ushindi yameaacha si makovu tu mioyoni mwa waliokuwa wajumbe na kambi zao bali vidonda halisi. Matokeo yale yaliliza baadhi ya wajumbe, kwa hiyo kitu muhimu sasa ni kutumia kila njia awezayo ili kuleta maafiakiano na kujenga umoja ndani ya chama chake. Ili kufanya pale anapokwenda kukabiliana na Maalim Seif, awe amejizatiti kweli kweli.
Hata kujieleza alishindwa maskini!!Uliyosema ni kweli kabisa nilimuona Nahodha tangu siku ya uchaguzi amenuna mpaka leo hajacheka kati ya wagombea wote huyu ameumia kweli. Lakini napenda kumfahamisha kwamba duniani hakuna haki akitaka haki basi ataikuta mbinguni akubali yaishe na maisha yaendelee.
Ndiyo anafaulu mtihani! Sasa ajibuje nje ya marking scheme yangu!Yaani unataka ajibu maswali kama wewe unavyotaka.
Nyie ndio kama wale walimu mnaotaka mwanafunzi ajibu kama ulivyomkremisha