Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Ndio maana walimficha kule kwny ile wizara ya wazee wa doso kwa miaka 11 maana angekua amepewa uwaziri kwny hizi wizara zenye changamoto angekua amesha chemka mapema sana na mapungufu yake kua hadharani lkn kule alikokua amefichwa isingekua rahisi kumsikia sana maana kashikashi zake hazihusishi wananchi wa kawaida directly.
 
Cheo pekee kinachomfaa Hussein Mwinyi huko Zanzibar ni cheo kama cha Jecha!

CCM inalea Usultani!
Hahaha .... unanikumbusha ya Jecha. Yani Jecha kwa akili yake alifikiri CCM watamfanyia hisani kwa jinsi alivyokisaidia chama kwenye uchaguzi wa 2015. Atashangaa hata Uwaziri hawampi ... Labda Uwenyekiti wa Bodi ya Kampuni Flani!!
 
Ataweweseka sn mpaka amwambie baba yake awaombe msamaha watz kwa kauli yake ile ya kipumbavu.....hizi ndo tabia Mwal alikua anazikemea na kuziita tabia za kimalayamalaya......
Wazanzibari hawamtaki kabisa mwinyi na kwa pamoja kura zote watampa MAALIM SEIF
 
Akijibu kama unavyotaka hatakua yeye sasa, atakua ni wewe, na kwanini umpangilie mtu ajibu jinsi unavyotarajia wewe,
 
Akijibu kama unavyotaka hatakua yeye sasa, atakua ni wewe, na kwanini umpangilie mtu ajibu jinsi unavyotarajia wewe,
Sijataka lazima ajibu kama mimi ila ninaelewesha tu madhara ya namna anavyojibu! Awe makini! Atajichimbia kaburi!
 
Ni rais mtarajiwa wa wapi?????
Mboga mboga mna matatizo Sana ninyi!
Mchezo mliozoea kuucheza Zanzibar (Jecha Game) mwisho 2015!

This time tunawanyunyizia dawa ya kuua wadudu! Mbogamboga nyie!
 
Kiukweli kuna wizara nyingine mtu anapewa siyo kwa kuwa ana uelewa, bali ni mweupe peee kichwani na ili kuficha aibu yake kutokana na kutimiza malengo fulani basi anapewa wizara ambayo ni vigumu kumgundua.

Mfano hai ni wizara ya ulinzi ambayo inaongoza majeshi ya ulinzi na usalama na waziri wake Dkt. Hussein Mwinyi. Hii wizara kwakuwa waziri wake ni kama hana kazi ya kumuweka kwenye vyombo vya habari mara nyingi basi ni vigumu kuutambua uelewa wa waziri husika.

Kiukweli sikujua kama waziri Hussein kichwani ni mweupe hivi hadi alipoanza kufuatwa fuatwa kwenye vyombo vya habari kutokana na hadhi yake aliyo nayo sasa. Itoshe kusema Hussein ni kama mgeni fulani asiyejua chochote kwenye siasa.

Amehojiwa sana na wana habari, majibu anayotoa ni kama mtoto anayelia lia! Hana hoja. Mfano kitendo chake cha kuelezea kura za wajumbe alizopata na jinsi alivyochanganua ni kama hajui jinsi anavyochimba kaburi lake kisiasa huko Zanzibar! Huyu angekuwa mfano waziri wa ardhi asingemaliza hata miezi sita ndani ya wizara hiyo.

Naamini kuwa, kama Hussein atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Magufuli kuwa Rais wa Bara basi Rais halisi wa Zanzibar atakuwa John Magufuli. Kwa mara ya kwanza kabisa Zanzibar itakuwa imepata Rais kamili kutokea Bara.

Aidha nimegundua kuwa ni kosa kubwa sana kumchagua Rais wa Zanzibar ambaye ametumika kwa muda mrefu ndani ya serikali ya Bara! Huyo ni kilaza kamili!

Ilikuwa ni vigumu sana kugundua competent ya Dkt. Hussein akiwa waziri wa majeshi maana waamuzi wakuu wa majeshi ni mkuu wa majeshi na Rais na ndiyo maana mkuu wa majeshi anapata heshima na ulinzi kuliko waziri wake ambaye kiitifaki ni boss wake! Wonders!

Namalizia kwa kusema, Waziri wa ulinzi na JKT wa Tanzania ndiye waziri asiye na kazi yoyote ya kimaamuzi ndani ya wizara zaidi ya kuwawakilisha bungeni! Na mbaya zaidi ulemavu mkubwa wa waziri husika unachangiwa na kauli ya "Majeshi yetu hayasemwi" Kwahiyo ni vigumu hata ndani ya bunge kujua uelewa wa waziri huyu kisiasa na kiuongozi kwa kuwa tu majeshi yetu hayajadiliwi!
 
ccm wanajijua wenyewe ndugu yangu, huoni watoto wa akina lowasa hao wanaibuka, watoto wa akina kikwete wale, yaani angalia vizuri n jicho la huku nyuma uone. Hatari....ni bora akina Shilla na Gwajima wamegundua michezo hii nao wanataka kupenyeza rupia angalau watoe tongotongo
 
Back
Top Bottom