Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

Source Swahili times

Maendeleo hayana vyama!
Amewauliza kwamba walimpigia wakasema Ndio..!?? Hizi ndo michezo michafu.. TAKUKURU kamateni hii..
 
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

Source Swahili times

Maendeleo hayana vyama!
Busara ingemwongoza akae kimya
 
Hakuna Kamati Kuu ya Wa Zanzibar kuna Kamati Kuu ya CCM

kamati kuu ya CCM iendelee kuchagua Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ( Zanzibar + Tanganyika) with balance members wa pande zote.... Wazinzabar waachwe wachague mgombea wao wa Zanzibar huku Watanganyika nao wakichagua Rais wao wa Tanganyika otherwise Zanzibar ni mkoa wenye wilaya tano..
 
Busara ingemwongoza akae kimya

Hakusema ayo ni mbwembwe za wapinzani wake, Mwinyi ndiyo Rais wa Zanzibar kwa miaka mitano ijayo mengine ni Maneno tu, sharif na membe wameingia kwanye SPV na dereva ni zitto na ndiyo mwisho wa upinzani Zanzibar,muda utasema
 
Nenda YouTube Azam two utaona mahojiano yote na Tido Mhando.

14 Julai 2020
Dar es Salaam / Dodoma, Tanzania

LIVE: MAHOJIANO MAHSUSI KATI YA TIDO MHANDO NA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CCM, Dr. HUSSEIN MWINYI

Mahojiano kati ya mgombea aliyechaguliwa kwa tiketi CCM kugombea Urais Zanzibar na kituo cha televisheni cha Azam cha Dar es Salaam, Tanzania.
Source : Azam TV
 
Umeshafeli nawewe. Lini umeshawahi kusikia Tanzania Bara tunapiga kura kumchagua Rais wa Zanzibar. Huu ni uteuzi ndani ya chama (CCM). Kumbuka Afro Shiraz na TANU ziliungana kikazaliwa Chama kimoja kinachoitwa CCM. Chama hiki hakina upande huu wala ule, isipokua nchi ndo ina Serikali mbili. Usichanganye mambo.
Kichwa maji wewe!! chama kama hakina upande inatakiwa uchaguzi ufanyike kwa kiongozi wa chama kwasababu uwiano wa wajumbe haupo sawa kwa pande zote. Inakua haramu kwa uchaguzi wa kiongozi wa nchi nyingine mpaka na wajumbe wasioongozwa na huyo kiongozi.
Huu ujinga mtaacha lini? jifunzeni ata kufanyia marekebisho hayo makosa yaliyofanyika mwanzo siyo kuyasifia tu.

Acha ujinga tena.
 
Kati ya michezo walio cheza hovyo ccm ni huu na inawezekana ni nguvu ya mungu imetumika ili kuiondoa ccm madarakani
14 Julai 2020
Dar es Salaam, Tanzania

LIVE: MAHOJIANO MAHSUSI KATI YA TIDO MHANDO NA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CCM, Dr. HUSSEIN MWINYI

Source : Azam TV
 
kamati kuu ya CCM iendelee kuchagua Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ( Zanzibar + Tanganyika) with balance members wa pande zote.... Wazinzabar waachwe wachague mgombea wao wa Zanzibar huku Watanganyika nao wakichagua Rais wao wa Tanganyika otherwise Zanzibar ni mkoa wenye wilaya tano..
Kwahiyo unataka chama kiwe na vyombo viwili vya maamuzi kimoja Zanzibar na kingine Bara. Kumbuka chama hakichagui Rais, kinachagua mgombea wake kwenda kushindana na wagombea wa vyama vingine. Wazanzibar ndo wanaochagua Rais.
 
Ngoja nile nishibe nije kuendelea kukuelewesha, kipi kigumu hapo usichoelewa, RIP Mzee wangu Mtikila na serikali zako tatu..
 
Back
Top Bottom