JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) - Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa amewataka Waandishi wa Habari nchini kuwa Mabalozi kwa kuandika habari zinazohusu masuala ya Wanawake na uongozi.
Wito huo ameutoa leo Oktoba 8, 2024 wakati akifungua warsha ya siku ya mbili ya Waandishi Habari zaidi ya 25 kutoka vyombo mbalimbali iliyofanyika katika ofisi za chama hicho Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kuwa, hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mitazamo hasi katika Jamii ya Wanawake kutokuwa Viongozi katika mamlaka mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) - Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa.
Dkt. Mzuri amewaeleza kuwa Waandishi wa Habari wanapaswa kuwa wajasiri na wabunifu katika kuibua changamoto ambazo zinawakakabili Wanawake kuishika nafasi ya uongozi.
"Humu ndani ninawaona Waandishi wengi ni vijana mnapaswa kuwa 'active', kuwa hamu ya kuandika habari ambazo zinahusu Wanawake na uongozi na kuibua changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo Sera na hata sheria," ameeleza.
Hata hivyo, amewataka Waandishi hao kutumia vyema mafunzo waliyoyapata na kuibua changamoto na mafanikio katika kumuwezesha Mwanamke kufikia nafasi mbalimbali za uongozi.
"Naomba msikilize vyema mafunzo haya na baada ya mafunzo muende kuyatumia ili yalete tija kwa Taifa," amesema.
Naye Mkufunzi katika mafunzo hayo Almasi Ali kutoka ZYF amewataka Waandishi wa Habari vijana kuchangamkia fursa mbalimbali wanazozipata ili kuleta mabadiliko katika Jamii.
"Ndugu zangu Waandishi wa habari hususani vijana mnatakiwa kucHangamkia fursa yoyote ambayo mnaipata ili mlete mabadiliko katika jamii na hata mabadiliko yenu binafsi," ameeleza.
Warsa hiyo ya siku mbili imewahusisha Waandishi wa Habari za Mitandao ya Kijamii, Magazeti Redio na Televisheni.
Chanzo: NA THABIT MADAI, ZANZIBAR