Dkt Nchimbi: CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe

Dkt Nchimbi: CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe

Sikutegemea waandishi wa habari wangeuliza maswali kama yale bila hofu.

Hasa yule mbaba mweusi mrefu mnene aliuliza swali lake kwa hisia sana..
 
Ila huyu jamaa (Nchimbi) ni bonge la kiongozi.
Na anamisimamo refer enzi za lowasa. Ila pia ana busara na hekima refer the way anavowajibu wapinzani.
 
Ana busara sana katika kuongea.Hata hivyo inawezekana aliyoahidi anaweza asitekeleze.
Ningependa CCM tumsimamishe yeye mwaka 2025.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Emmanuel Nchimbi ,amesema CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya aliyekuwa Mshauri wa CHADEMA Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe.

"Chama chetu kinaunga mkono kauli ya Rais wetu yakutaka uchunguzi wa haraka ufanyike, watuhumiwa wapatikane na hatua zichukuliwe. Rais ametoa kauli hile kwa ukali kabisa ameeleza wazi ambavyo amekerwa na jambo ambalo limetokea."Nchimbi

"Mimi binafsi ni waambieni tu nilipopata taarifa ya hule Msiba, Mbowe alinipigia simu zaidi ya mara tano najuwa atakacho niambia ni habari ya msiba imekuwaje najuwa kama chama tawala na wajibu anapo ongea hivyo ila ujasiri wa kupokea simu nilikosa"

"Na baadae nikamuandikia meseji nikamwambia nakuomba radhi jambo lile lilinivuruga sana nikashindwa kupokea simu yako"Nchimbi

Soma Pia:
a
 
Back
Top Bottom