Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani Serikali ngapi zimepita na hazikufanya zaidi ya kuvurunda ? Uliwahi sikia Ajira awamu ya 5? Mnajitoa ufahamu si ndio? 🀣🀣🀣🀣
Kwahiyo serikali hii inachofanya ni hisani? Halafu hayo ya kuvurunda utayasema wewe ila ccm kama chama tawala cha Rais Samia ndio kimekuwa madarakani kwa miaka yote hiyo sidhani kama watakubaliana na wewe kwamba huko nyuma serikali zilizoundwa na chama chao zilikuwa zikivurunda.
 
Hakuna mwaka ambao serikali uliacha kufanya shughuli za maendeleo, Samia muda wake utaisha atakuja mwengine nae atakuta changamoto zilezile za miaka yote. Unachokifanya wewe hapa ni kujikita kumpa sifa zote Samia kwa shughuli za maendeleo ya serikali kuwa hayo yeye ndio anafanya ila kwenye mapungufu ya hii serikali yeye hahusiki wanahusika wasaidizi wake.

Ni utoto.
 
Changamoto haziwezi kuwa zile zile.Mfano Kwamba mwaka 2030 Rais mwingine atakuta import ya ngano imepungua kutoka 98% Hadi 20% tuu Kwa uwekezaji unaofanywa na Samia.

Likewise Rais mwingine atakuja atakuta shida ya Maji haipo,shida ya umeme hakuna,shida ya mashule hakuna na shida zingine kama hizo.

Moja ya mambo ambayo ni kama maendeleo ya Kudumu ni swala la Barabara,hili haliwezi kuisha maana hata robo ya mtandao wa Barabara hapa Tanzania haujawekwa.lami.

Kazi zinaongea πŸ‘‡

View: https://twitter.com/SuluhuSamia/status/1788567211105235450?t=n07wbC43vuWwzI6giU2ztA&s=19
View: https://www.instagram.com/reel/C6v35Odtzt7/?igsh=NnJhMzV2YzA4MDVu
 
Sa
Basi na Wazee Wastaafu Walipwe Kiunua Mgongo chao kama ilivyokuwa Zamani. Kwa nini mliharakisha Kikokotoo kwa Wastaafu ilhali Magufuli alisema kianze July 2024? RIP John Magufuli. Uchumi uliokua na Miradi inayotekelezwa si inaleta faida?
 
Kama sasa hivi wewe unaona serikali za kabla ya Samia hakuna zilichofanya hadi alipokuja Samia basi ni wazi hata akiondoka Samia itaonekana hakuna serikali yake ilichofanya, ndio maana nakwambia kuwa hakuna mwaka ambao serikali iliacha kufanya shughuli za maendeleo.
 
Kilifanyika Kwa kiwango.kiasi.na zaidi kushinda zilizotangulia lakini Samia nae amefanya zaidi ya hiyo ya awamu ya 5.

Kila awamu iwe inatumia nyingine kama.benchmarak.Samia alisema.anawajibika kufanya mara 2 zaidi ya mtangulizi.wake Ili kuwaaminisha watu kwamba Wanawake wanaweza tofauti na walivyokaririshwa.

View: https://www.instagram.com/reel/C6v-dg9M2BB/?igsh=ZjdxbG5yanF0aGt4
 
Yote haya hayana maana kwa baadhi yetu kwa sababu kwanza ni Mwanamke anayechukuliwa kuwa ni dhaifu tu hata akishusha mwezi ukawa karibu kabisa na dunia na pili ni mzenji kutoka Kizimkazi na yote anayoyafanya yanatazamwa kwanza kwa mtazamo wa kibaguzi.

Tuna nchi yenye wajinga wengi sana.
 
Siku za Mwanzo kabisa za Rais Samia kuingia madarakani,mwanaf mmja alisema kitakachomtatiza Samia ni upande anaotokea,dini yake na jinsia.

Na Kuna mchangiaji mmja aliwahi sema kwamba hata kama Samia aweke tiles Barabara zote eti wao hawampendiπŸ™„πŸ™„

Ndio maana mara nyingi Huwa nasema Hakuna vyombo Vya Dola timamu vinaweza mpoteza Rais kama Samia eti kisa kundi kubwa la wajinga wanaoleta chuki binafsi badala ya kuangalia anachofanya.

Samia yupo Kwa maslahi ya Nchi na sio punguani kadhaa bila kujali uwingi wao.

Kazi zinaongea πŸ‘‡

View: https://twitter.com/mamanafanikisha/status/1789178523736740249?t=D1CHzGYbE05a29IzZqPyyg&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…